Nani anafaa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kifo cha Balozi John Kijazi?

Nani anafaa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kifo cha Balozi John Kijazi?

Kwangu mimi ni huyo huyo. Dr. Laurian Ndumbaro. Ana utulivu. Haonekani kuwa na mihemko. Hata kama umri umeenda lkn hiyo nafasi yenyewe inahitaji hao wenye umri mkubwa. Anaonekana ni mmatengo/mngoni wa mkoa wa Ruvuma((Mbinga.)
Wa pili ni Prof. Faustine Bee ambaye kwa sasa ni VC wa UDOM. Ameituliza udom ambayo ilianza kutokuwa na utulivu kati ya watumishi. Huyu aliwahi kuongoza chuo cha Ushirika-Moshi. Inaonekana ni muiraq wa mkoa wa Manyara/Arusha(Karatu)
3. Professor Victor Samwel Manyele. Huyu aliwahi kuwa Mkemia Mkuu wa serikali. Ni mtu wa Rukwa, wilaya ya Kalambo(Mfipa).
4. David Mfinanga; DVC-Admin UDSM- Mhandisi wa Transportation. Huyu ni mpare. Changamoto yake ni Sefue ametoka juzi tu. Sefue naye alikuwa mpare.
5; Elius Mwakalinga; Huyu ni aktekt(Arch.) Katibu mkuu-Ujenzi, Ni mnyakyusa wa Kyela.
6. Tito Mwinuka; Huyu ni mhandisi wa umeme. Ni mkurugenzi wa TANESCO kwa sasa. Ni mbena huyu.
Kazi kwenu vikosi vya vetting na kamati za uteuzi. Lakini tusubiri mdudu apoe kidogo ndio shughuli zianze.
Mchango wako mzuri ila ilipoweka makabila tu maeneo waonatoka ndo ukaharibu kabisa. Umetutoa katika utaifa ukatugawa, mbona hujaongelea na dini ili ukamilishe zoezi lako na adhma yako.
 
Dr. Laurean Ndumbaro hafai kabisaaaaa!!!. Hata nafasi aliyokalia sasa ina mpwaya kabisa.

Dr. Laurean Ndumbaro ana matatizo makuu yafuatayo ambayo yanafanya asiwe mtu sahihi kukalia hiyo nafasi ya KMK;

1. The man us very allogant

2. Mara nyingi anafanya maamuzi bila kuyafanyia analysis

3. Anapenda kutumika na baadhi ya viongozi wa taasisi za umma kuwaumiza watumishi kwa kuwahamisha kiholela

4. Kuna watu wanadai kuwa the man is corrupted to the extent kwamba akipewa fedha anaweza kumpangia mtu kazi ambayo hana ujuzi nayo na hajasomea. Mfano mzuri, kuna taasisi moja nyeti huko kusini kapelekwa mwana mama mmoja kwa nafasi ya ukurugenzi wakati hata mambo ya uhasibu hajasomea.

Nashauli atafutwe mtu mwingine kwenye hiyo nafasi lakini Dr. Laurean Ndumbaro hafai.

Mkitaka tutawaletea orodha ya baadhi ya viongozi wa taasisi za umma walioshirikiana na Dr. Laurean Ndumbaro kuwaumiza watumishi wa umma kwa matakwa binafsi.
Lete hii orodha tusaidie kurekebisha!!
 
Punguzeni vitimbi na chukulia msiba wa mwenzio kama vile ungeombeleza ukifikwa na msiba wa mtu wako wa karibu.
Alipofariki Balozi Mahiga kesho yake Mwigulu akateuliwa kushika nafasi yake ulikuwa bado hujazaliwa??
 
Wafuatao wanaweza kuteuliwa
1. Kusiluka katibu ofisi ya Rais
2. Ngusa ktb wa Rais na mniikulu
3. Prof Gabriel Km wizara mifugo
4. Ras Tabora
5- Ras mtwara
6.Kwakuwa Kijazi alitokea ubalozi india tusishange kuona Balozi mmojawapo
7. Kama ni mwanasiasa basi awe na historia ya utendaji
Dr. Slaaa
 
Mchango wako mzuri ila ilipoweka makabila tu maeneo waonatoka ndo ukaharibu kabisa. Umetutoa katika utaifa ukatugawa, mbona hujaongelea na dini ili ukamilishe zoezi lako na adhma yako.
Mkuu kwenye swala la hizo nafasi, hilo haliepukiki. Lazima ujulikane ndani nje. Kabila lako, dini yako na unakotoka. Kutotaja ni kujidanganya tu.
 
No 04 Eng. Prof. David Mfinanga anafaa kwa nafasi hiyo . Ni mtu smart na mtaratibu katika maamuzi.
Ana maamuzi yanayozingatia taratibu na sheria na sio mtu wa kuyumbishwa.
 
makonda Njoo utie neno hapa
kasomi frag.gif
 
Makabila yetu yapo, kanda, mikoa yetu ipo, wilaya, tarafa, kata, vijiji, vitongoji, shina na hata familia. Haziepukiki. Tatizo tu ni pale tunapotumia nguvu inayotokana na kabila, kanda, mkoa, wilaya au hata familia kuwaumiza wengine au kutengeneza kajamhuri ka kabla lako ndani ya Jamhuri moja ya Tanzania.
 
Hata maiti hajaoshwa mmeshaanza kuvizia nafasi?
Mkuu watu wanasubiriana watu waugue wafe, wachukue vyeo...kutakuwa na kurogana kwa kasi ya 5G sasa hivi.
Pathetic! ila unemployment imetutoa utu!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Back
Top Bottom