Nani anafaa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kifo cha Balozi John Kijazi?

"Mimi sipangiwi, ukinipangia ndo' unaharibu kabisaa.." alisikika jeipiem
 
Wadau japo ni mapema sana, ila tutambue katibu mkuu kiongozi lazima/kawaida atakuwa ni mtumishi wa umma, kwahiyo tusitaje majina ya wanasiasa.
Nini tofauti ya mwanasiasa na mtumishi wa umma, aliyepita aliteuliwa akiwa balozi, kwa cheo hicho alikuwa mwanasiasa au mtumishi wa umma..
 
Daudi Albert Bashite, tayari anashinda tu Ikulu kila siku ukute ndo kamloga Kijazi
 
Nafasi hiyo inawafaa zaidi Makatibu wa Wizara wenye uzoefu Mkubwa. Hapo Katibu Mkuu wa TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga anafit vizuri
 
Kwanza poleni sana kwa misiba iliyoikumba nchi yetu.

Pili, watu huelewa uchapakazi wako bila wewe kuwaambia.

Wanaweza wakakupendekeza kama uchapakazi wako ni mzuri au wasikupendekeze kulingana na uchapakazi wako wa hovyo hovyo.

Ile watu wakisema fulani anafaa basi hata usipopewa nafasi hiyo elewa kuwa unafaa na jamii inakukubali hivyo unapaswa kuendeleza imani hiyo kwa jamii inayokuzunguka.

Swali liko hapo juu, wewe wadhani nani anaweza kuvaa kiatu cha Injinia na kwa nini unamfikiria huyo?

Ingawa umri wake imeenda lakini binafsi namfikiria Katibu mkuu wa utumishi Dr. Laurian Ndumbaro

Kwanini:-

Ni mchapa kazi, ana uzoefu wa muda mrefu kazini na ametulia-hana mapepe mapepe.

2........

3........

4......

Profesa Kamuzora kwa sasa ni Katibu Tawala Kagera​

Nini tofauti ya mwanasiasa na mtumishi wa umma, aliyepita aliteuliwa akiwa balozi, kwa cheo hicho alikuwa mwanasiasa au mtumishi wa umma..
Mkuu, kuna mabalozi wanaoteuliwa kutoka maeneo mawili tofauti, kuna wanaoteuliwa kutokea kwenye siasa na kuna wanaoteuliwa kutokea ndani ya serikali (watumishi wa umma). Balozi Kijazi kabla ya kuwa balozi alikuwa ni mtumishi wa umma kwenye wizara ya miundombinu/ujenzi, ndio baadaye akateuliwa kuwa balozi. Kwahiyo, mzee Kijazi hakuwa mwanasiasa. Chikawe, Nchimbi, Dr. Nsekela, Dr. Slaa n.k. hawa ni mfano wa mabalozi walioteuliwa kutokea kwenye siasa, kwahiyo sio rahisi watu kama hawa kuwa katibu mkuu kiongozi. Mberwa Kairuki, Ramadhani Dau na Ernest Mangu ni mfano wa mabalozi walioteuliwa kutokea kwenye utumishi wa umma. Hope umenipata.
 
Kwanza poleni sana kwa misiba iliyoikumba nchi yetu.

Pili, watu huelewa uchapakazi wako bila wewe kuwaambia.

Wanaweza wakakupendekeza kama uchapakazi wako ni mzuri au wasikupendekeze kulingana na uchapakazi wako wa hovyo hovyo.

Ile watu wakisema fulani anafaa basi hata usipopewa nafasi hiyo elewa kuwa unafaa na jamii inakukubali hivyo unapaswa kuendeleza imani hiyo kwa jamii inayokuzunguka.

Swali liko hapo juu, wewe wadhani nani anaweza kuvaa kiatu cha Injinia na kwa nini unamfikiria huyo?

Ingawa umri wake imeenda lakini binafsi namfikiria Katibu mkuu wa utumishi Dr. Laurian Ndumbaro

Kwanini:-

Ni mchapa kazi, ana uzoefu wa muda mrefu kazini na ametulia-hana mapepe mapepe.

2........

3........

4......
1.Atafutwe anayejua sheria,kanuni za utumishi wa umma.maana Viongozi wamekuwa wanakiuka Sheria,kanuni na taratibu mbalimbali.
2.Awe ni mtu anajua Diplomasia na uzoefu na Ajue kuwasiliana kwa lugha hizo za uko mbelr.
 
Kwani IKAMA inasemaje??...Mkurugenzi wa Fedha ni lazima awe aliesomea mambo ya fedha na sio vinginevyo!!!
Dr. Laurean Ndumbaro kampeleka mwanamama mmoja kwenye taasisi nyeti aana ya umma huko kusini kuwa Mkurugenzi wa Fedha wakati hana hiyo sifa, hajawai kufanya hiyo kazi na wala hajawi kuwa registered na NBAA.

Watu wanajiuliza, ni kitu gani kimempata Dr. Laurean Ndumbaro??, je wahasibu na wakaguzi wa mahesabu wameisha Tz mpaka akapelekwa mtu aliyesoma Sociology???
 
Mkuu, kuna mabalozi wanaoteuliwa kutoka maeneo mawili tofauti, kuna wanaoteuliwa kutokea kwenye siasa na kuna wanaoteuliwa kutokea ndani ya serikali (watumishi wa umma). Balozi Kijazi kabla ya kuwa balozi alikuwa ni mtumishi wa umma kwenye wizara ya miundombinu/ujenzi, ndio baadaye akateuliwa kuwa balozi. Kwahiyo, mzee Kijazi hakuwa mwanasiasa. Chikawe, Nchimbi, Dr. Nsekela, Dr. Slaa n.k. hawa ni mfano wa mabalozi walioteuliwa kutokea kwenye siasa, kwahiyo sio rahisi watu kama hawa kuwa katibu mkuu kiongozi. Mberwa Kairuki, Ramadhani Dau na Ernest Mangu ni mfano wa mabalozi walioteuliwa kutokea kwenye utumishi wa umma. Hope umenipata.
Kinachoongoza kupata mtu sahihi ni mahitaji ya nafasi hiyo kwa wakati huu..au wadhifa na sifa yaani, lazima awe injinia, au daktari au mtumishi wa umma, au mganga wa tiba asili nk..kwa akili yako wewe, kitu gani cha kuangalia..fikiri zaidi ya unachoona kwa macho au kusikia, itakusaidia.
 
Dr. Laurean Ndumbaro kampeleka mwanamama mmoja kwenye taasisi nyeti aana ya umma huko kusini kuwa Mkurugenzi wa Fedha wakati hana hiyo sifa, hajawai kufanya hiyo kazi na wala hajawi kuwa registered na NBAA.

Watu wanajiuliza, ni kitu gani kimempata Dr. Laurean Ndumbaro??, je wahasibu na wakaguzi wa mahesabu wameisha Tz mpaka akapelekwa mtu aliyesoma Sociology???
Mbali ya kuwa huyo mwanamke aliyepelekwa kwenye hiyo taasisi nyeti ya umma kuwa Mkurugenzi wa Fedha, pia hana maadili ya kuwa kiongozi katika ngazi hiyo; she is too sliperly, mpenda majungu, mbabaishaji katika na mjanjamjanja tu.
 
Kwa hiyo Dr. Laurean Ndumbaro hafai kuwa KMK, hata nafasi aliyopo sasa inatakiwa liangaliwe.
 
Aliye mpole na mvumilivu mkubwa. Mwenye busara sana na asiye na papara wala mapepe. Ambaye atamuelewa vyema boss wake. Awe ni mpokea maagizo mzuri na mtekekezaji kwa wakati. Asiwe mtu wa kuhoji bali ni kutekeleza.
 
Back
Top Bottom