Nani anafaa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kifo cha Balozi John Kijazi?

Mchango wako mzuri ila ilipoweka makabila tu maeneo waonatoka ndo ukaharibu kabisa. Umetutoa katika utaifa ukatugawa, mbona hujaongelea na dini ili ukamilishe zoezi lako na adhma yako.
 
Lete hii orodha tusaidie kurekebisha!!
 
Punguzeni vitimbi na chukulia msiba wa mwenzio kama vile ungeombeleza ukifikwa na msiba wa mtu wako wa karibu.
Alipofariki Balozi Mahiga kesho yake Mwigulu akateuliwa kushika nafasi yake ulikuwa bado hujazaliwa??
 
Dr. Slaaa
 
Mchango wako mzuri ila ilipoweka makabila tu maeneo waonatoka ndo ukaharibu kabisa. Umetutoa katika utaifa ukatugawa, mbona hujaongelea na dini ili ukamilishe zoezi lako na adhma yako.
Mkuu kwenye swala la hizo nafasi, hilo haliepukiki. Lazima ujulikane ndani nje. Kabila lako, dini yako na unakotoka. Kutotaja ni kujidanganya tu.
 
No 04 Eng. Prof. David Mfinanga anafaa kwa nafasi hiyo . Ni mtu smart na mtaratibu katika maamuzi.
Ana maamuzi yanayozingatia taratibu na sheria na sio mtu wa kuyumbishwa.
 
Makabila yetu yapo, kanda, mikoa yetu ipo, wilaya, tarafa, kata, vijiji, vitongoji, shina na hata familia. Haziepukiki. Tatizo tu ni pale tunapotumia nguvu inayotokana na kabila, kanda, mkoa, wilaya au hata familia kuwaumiza wengine au kutengeneza kajamhuri ka kabla lako ndani ya Jamhuri moja ya Tanzania.
 
Hata maiti hajaoshwa mmeshaanza kuvizia nafasi?
Mkuu watu wanasubiriana watu waugue wafe, wachukue vyeo...kutakuwa na kurogana kwa kasi ya 5G sasa hivi.
Pathetic! ila unemployment imetutoa utu!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…