Nani anapaswa kulipa hela ya udalali kati ya mwenye nyumba na mpangaji?

Nani anapaswa kulipa hela ya udalali kati ya mwenye nyumba na mpangaji?

Nchi ya ajabu hii kuna vitu ukiwaza mpaka unakuta kuishi TZ mambo ya hovyo ni mengi alafu serikali imekaa kimya yani wanaona ni moja ya ajira kwa wananchi wizi mtupu.
Serikali ilipaswa kuliona hili na kulikemea kwasababu linaumiza wananchi lakini kwasababu tumezoea kuishi kwa maziwa ndio ivyo ukitafuta nyumba ya kupanga Leo kichwa kitakuuma shida kila kona kwenye hii nchi
Lukuvi aliwahi kutoa tamko suala la madalali kwenye upangishaji likome, ila kama kawaida matamko yanatoka kama vile hakuna kilichosemwa
 
mwenye nyumba halipi mwenye nyumba anampa dalali mchongo ili apate pesa kupitia nyumba yake vipi tena amlipe
 
Salaam wakuu,
Jambo ni hili"Ni nani anaepaswa au mwenye haki ya kumlipa Dalali kati ya mwenye nyumba na mpangaji?
Mpaka sasa anaemlipa dalali ni mpangaji lakini kwa mtazamo wangu hii si sawa, nionavyo mimi anaestahili kumlipa dalali ni mwenye nyumba kwasababu yeye ndie anaefanya biashara na dalali anatafuta wateja (wapangaji)kwa niaba yake hivyo dalali ni mtumishi wa mwenye nyumba na ndio sababu mawasiliano ya dalali na mpangaji yanaisha palepale mara tu baada ya kupata nyumba lakini mawasiliano ya mwenye nyumba na dalali yanaendelea kwasababu ni washirika.mpangaji kumlipa dalali ni "Uhuni"tu unaoendelezwa kienyeji labda kwasababu si kazi yenye utaratibu au muongozo rasmi unaoeleweka.Ni sawa tu na mpigadebe wa daladala anaemfuata abiria kumdai pesa "eti"kwasababu tu amemuonyesha siti ya kukaa badala ya kwenda kumdai konda kwa kumkusanyia abiria. wanachokifanya madalali kwa kushirikiana na wenye nyumba ni UHUNI.
 
Hivi unawezaje kumtafuta mtu akutafutie nyumba alafu useme mwenye nyumba ndio alipe. Mm nilikua nakubaliana na dalali kulingana na tulivyozunguka kama kodi ni 50k nikimpa 20k ya kuzunguka nae sioni tabu ila sio kuanza kumlipa kodi ya mwezi mmoja juu na hili na mwambia mapemaa kabla hajaanza kazi wapo waliokua wanakataa na wengine wanakubali
 
Dalali hatafutwi bali anafuatwa,wana maskani zao kama sio Ofisi kabisa, wanamtandao wao na wanamawasiliano na wenye nyumba,hawaanzi kutafuta nyumba wakati unapowafuata bali wanakuwa tayari wanajua wapi nyumba ilipo. kazi yao ni kukupeleka kwenda kuona,mzunguko unatokea pale ambapo utakuwa hujarishwa na nyumba uliyopelekwa na kutaka kuonyeshwa nyingine na hili ni sehemu ya kazi na kuchagua ni haki ya mteja.
 
Wote kivipi mkuu!?
Basi wachange kama malipo ya dalali ni laki moja mwenye nyumba atoe hamsini elfu na mpangaji atoe hamsini elfu,p dalali apewe laki yake lakini sio achukue laki kwa mwenye nyumba halafu akachukue laki nyingine kwa mpangaji, Huo ni Uhuni.
 
Dalali hatafutwi bali anafuatwa,wana maskani zao kama sio Ofisi kabisa, wanamtandao wao na wanamawasiliano na wenye nyumba,hawaanzi kutafuta nyumba wakati unapowafuata bali wanakuwa tayari wanajua wapi nyumba ilipo. kazi yao ni kukupeleka kwenda kuona,mzunguko unatokea pale ambapo utakuwa hujarishwa na nyumba uliyopelekwa na kutaka kuonyeshwa nyingine na hili ni sehemu ya kazi na kuchagua ni haki ya mteja.
Sawa
 
Back
Top Bottom