1. Makubaliano yenu yakoje?
2. Kwa nini utafute Dalali Wakati nyumba zipo nyingi? Hiyo sababu inayokufanya umtafute Dalali ndio hiyo itakayokufanya umlipe.
3. Kama ni mwenye nyumba, Kwa nini usitafute mwenyewe wateja, hiyo si ni biashara yako? Sababu uliyoona ya kutafuta Dalali wa kukukodishia nyumba yako ndio hiyo itakayokufanya umlipe.
Maswali ya namna hiyo huulizwa na watu wa Aina ifuatavyo;
1. Washamba, ambao hawajakulia mijini.
Kijijini huwezi kuta mambo ya hivyo.
Ila Miji mikubwa hayo ni mambo ya kawaida.
2. Wanaroho ya korosho.
Roho Mbaya ndio inaweza kukufanya uulize maswali ya kijinga kama hayo.
Mkataba WA Dalali na mwenye nyumba unakuhusu nini wewe mpangaji?
Wewe umekutana na Dalali mkaingia makubaliano yenu, kwamba labda utamlipa kiwango Fulani Kwa kazi ya kukutafutia Apartment. Bali kwenye makubaliano yenu. Masuala ya kuuliza mwenye nyumba mbona anamlipa Dalali au hamlipi hiyo haikuhusu.
Labda kama na wewe unataka kuwa Dalali.
Ni Sawa na udalali wa kuuza magari, umemuambia mtu akuuzie Gari yako au umepeleka kwenye Kampuni la kuuza magari ya mtumba. Mmepatana Bei kuwa aliuze Kwa milioni 10, alafu umekabidhi Kadi na kila kitu. Alafu Dalali akapatana na mteja aliyemtafuta kwamba Gari milioni 20 alafu wewe Kwa Roho Mbaya unaona mbona amechukua nyingi. Come on!
Hizo ni Akili za Roho Mbaya, husda na Wivu wa kijinga.