Nani anatakiwa kupiga goti hapa?

Nani anatakiwa kupiga goti hapa?

Hizi vitu bana tunaiga tu. Hv wazee wetu walifanya haya yote??
 
Salaam Wakuu,

Nimekutana na hii clip hapa chini. Je nani anapaswa kupiga goti kati ya mwanaume na mwanamke wanapovalishana pete?

Binafsi naona ni tamaduni za watu tu hizi vyoyote ni sawa.

Tazama clip hizi hapa chini.

View attachment 2444917

View attachment 2444922
Wote wanatakiwa kupiga goti.

1. Mwanaume atapiga goti wakati anataka kumvalisha Pete ya uchumba mwanamke. Na dhumuni la kupiga goti, ni ishara ya kuomba uchumba.

2. Mwanamke atapiga goti wakati anavalishwa Pete ya ndoa. Dhumuni la kupiga goti ni kuonesha unyenyekevu na shukrani kwa kusitiriwa (ndoa ni stara kwa wanawake).
 
Kwanza kwa anavyojitambua huu upuuzi hatafanya. Ataolewa vizuri tu
Ila tambua PENZI ni ulevi fulani hivi.
Unavyomfikiria mwanao kwa sasa , mbele ya penzi anaweza akabadilika ukashangaa.
Wengine wanafikia hata kuwakana wazazi kabisa...achana kabisa na huu uraibu unaoitwa penzi.
Wewe nafasi yako kama mzazi ni kumwombea Mungu apate mwenza mwema.
 
Naona ni uduwanzi tu
Lakini, kama linapigwa goti basi apige KE, lakini sio ya kutambaa na magoti, ni umakorokocho. Ni kama unakuta mke anamuambia mumewe shikamoo. Nilishangaa sana sehemu. Yaani watu usiku mnageuzanageuzana na kutoa milio ya maajabu halafu asubuhi tena mashikamoo.
 
Ila tambua PENZI ni ulevi fulani hivi.
Unavyomfikiria mwanao kwa sasa , mbele ya penzi anaweza akabadilika ukashangaa.
Wengine wanafikia hata kuwakana wazazi kabisa...achana kabisa na huu uraibu unaoitwa penzi.
Wewe nafasi yako kama mzazi ni kumwombea Mungu apate mwenza mwema.
Hakuna mapenzi ya hivyo nakwambia ni unafiki tu. Naamini hatafanya maana hajafundishwa hivyo.
Na ninavyomuona ni feminist kabisaa hatakubali huo upuuzi
 
NALIA NGWENA nimeshindwa kabisa hata machozi ya uongo na kweli hakuna Tena suala la kupiga magoti ndio suala gumu mno kwangu.

Nina mpango wa kumvisha Pete shemeji yenu lakini nikifikiria kuhusu Jambo la kupiga goti na kutoa machozi ya furaha nashindwa kabisa.

Njooni mnishauri huwa mnawezaje wezaje kufanya hivyo.
 
Hya ni mambo ya wa Kristo tu, kwa Waisilamu mwanaume ni aljari siku zote
 
Hya ni mambo ya wa Kristo tu, kwa Waisilamu mwanaume ni aljari siku zote
Sijyi kwanini nyie maamuma chochote kikiwa kibaya na cha hovyo mnakihusisha na ukristo. Acha ujinga wako wewe. Juzi tu Juma Kitinku kapiga goti na kulia mbele za mwanamke hapa Sinza. Usipende kugeneralize na kusingizia dini za wenzio mambo ya hovyo.

Hiyo suala halihusiani na dini ila linahusiama na ujana na utandawazi. Vijana wengi wa sasa hawajitambui na wanaigiza maisha ya mapenzi wanayoyaona kwenye TV na ndio maana mwisho wa siku wanalalamika kuhusu ndoa zao kutokudumu. Hakuna sehemu kwenye Ukristo imeandikwa hivyo au inayowataka wanaume kupiga magoti wakati wa kuvalishana pete. Ni tujamaa twa sasa tu na kuigiza maisha.
 
We mtoto wa kiume muache mkeo mtarajiwa ndo apige goti then kimahaba unaweza muinua ndo umveshe

Siezi ruhusu mwanaume wangu apige goti wooiiii bora tusimame wote kama minguzo ya umeme
Ubarikiwe
 
We mtoto wa kiume muache mkeo mtarajiwa ndo apige goti then kimahaba unaweza muinua ndo umveshe

Siezi ruhusu mwanaume wangu apige goti wooiiii bora tusimame wote kama minguzo ya umeme
Mwanaume anatakiwa kupiga goti kwasababu yeye ndio kaenda kuomba uchumba

Logically anayeomba ndiye anayetakiwa kupiga goti...ndio maana wanasemaga 'she said yes'
 
Mwanaume anatakiwa kupiga goti kwasababu yeye ndio kaenda kuomba uchumba

Logically anayeomba ndiye anayetakiwa kupiga goti...ndio maana wanasemaga 'she said yes'
Baba yako wakati anaenda mposa Mama yako mpaka mkazaliwa nyie alipiga goti? Wacheni kuonea na kuyumbisha vijana wa watu. Waoneeni huruma.
 
Baba yako wakati anaenda mposa Mama yako mpaka mkazaliwa nyie alipiga goti? Wacheni kuonea na kuyumbisha vijana wa watu. Waoneeni huruma.

Sidhani kama umesoma nilichoandika....kwasababu jibu la swali lako lipo kwenye nilichoandika
 
Back
Top Bottom