Nani anayemlazimisha Asharose Migiro kuvaa Mahijabu na Mabaibui? Ni kumkosea sana

 

Anaonekana kama kibibi flani ombaomba au kigagula/kichawi au muuza mihogo ya kuchemsha kwenye sinia mitaa ya Ikwiriri.
 
Huhitaji sheria kutambua mavazi ya kidini.
Nchi haiendeshwi kwa hisia bali inaendeshwa kwa sheria na katika sheria za nchi yetu hakuna sehemu inapo tambua kuwa mavazi fulani ni utambulisho wa dini fulani.
Hivyo unaruhusiwa kuvaa nguo yeyote lamsingi iwe imekaa kiheshima tu

Na katika uislamu hakuna sehemu ambayo inasema ni razima kuvaa hijabu au nikabu bali uislamu umeamlisha mwanamke ajistiri na mtu anaweza kujistiri kwa nguo yeyote tu sio lazima hijabu.
Suala la hijabu ni ubunifu wa binadamu katika kurahisisha mambo kwenye uvaaji tu.
Alafu ww ni mribelari gani usiye amini katika uhuru wa mtu kuvaa atakavyo?
 
Mnataftiza tu maneno. Lkn sidhani kama itasaidia kumtoa Samia before 2030
Hili la 2030 usiwe na shaka nalo; Samia ni mhalifu, na kama walivyo wahalifu wote ni lazima awajibishwe kabla ya hiyo 2030 unayozungumzia wewe.
 
Mwaka 1989 au 1990 nilikutana na Asharose Harare kwenye conferences tofauti sote tungali vijana. Mimi nilikuwa kwenye conference ya CDRC University of Zimbabwe, na yeye alikuwa kwenye conference tofauti kabisa ambayo nadhani ilikuwa inafanyika Holiday Inn Harare. Asharose alikuwa liberal kweli, kwani alikuwa anavaa jeans ambazo Tanzania zilikuwa hazijafika wakati huo
 
Kumbe wa kitambo kidogo
 
Katiba yetu inasema sisi ni taifa la kijamaa, sasa je ni kweli sisi ni taifa la kijamaa?? Narudia tena, huhitaji sheria kutambua vazi au utambulisho wa kidini pia sina shida watu kuvaa hijabu zao mkuu ila lazima tutambue ukweli na uhalisia wa nchi yetu ilivyo kwamba kwa upande wa Tanganyika kutakuwa na kelele tu kwa baadhi ya watu ikitokea wameingia Ofisi ya umma wakakuta watumishi saba kati ya kumi wamevaa hijabu, na kuna scenario nyingi tu za ajabu ajabu zinaweza kuzuka, mfano chumba cha Waislamu kuswali peke yao Airport Arusha kilizua utata na malumbano sana, sasa busara ni kuepusha mambo kama haya kwa ku discourage utambulisho wa kidini katika masuala ya umma.

Pia uvaaji hijabu kwa Waislamu ni jambo la sheria na religious conditioning zaidi, viashiria vya uhuru ni kwa mbali sana.
Utasema watoto wa shule za msingi wanavaa hijabu kwa hiyari yao wenyewe na kupenda?
 
Ndio maana CCM inatuona wananchi ni binadamu wa hovyo maana kazi yetu ni kuropoka tu.

Yaani wewe kuona jina la Asharose ushahitimisha tayari na dini yake.

Kukusaidia tu jina lake la ubini ni Asharose Mtengeti na dini yake ni muislamu wa kuzaliwa.

Hivi inakuwaje huna info za mtu unaetaka kumuongelea. Halafu tafuta picha zake akiwa balozi utaona hiyo ‘turban’ amekuwa akifunga kichwani muda wote akiwa balozi U.K.

Ni shida sana ndio maana asilimia kubwa ya wachangiaji wa JF wanaodai maendeleo hawakumuelewa Magufuli ignorance is still high in Tanzania.
 
Mkuu hii ni mada nzuri sana, anzishia uzi wake ili wanadiplomasia waijadili
 
Inawezekana vipi mwanadiplomasia wa level ya Dr Asharose Migiro na umri wake huo alazimishwe kuvaa aina furani ya mavazi kwa sababu ya cheo/madaraka?
Haiwezekani
 

Nimesha kwambia kuwa waislam wameamliwa kujistiri na mtu anaweza kujistiri kwa nguo yeyote tu na sio razima iwe hijabu ,kwenye uislamu nguo yeyote ni ya kidini ili mradi inakustiri tu.
Na ndio maana sheria haijasema kuwa ili uingie msikitini ni lazima uvae ijabu au nguo fulani bali unatakiwa kuingia msikitini ukiwa umejistiri.

Kwa hiyo hao watoto wasio vaa hijabu hizo sale zao huwa wamezivaa kwa uamuzi wao au kwa kupenda?
Basi kuanzia sasa hivi waanze kwenda shule wakiwa uchi ili wakisha kuwa watu wazima wavae kwa kupenda.
Au ndo nyinyi ambao kwenu mwanamke kuvaa hijabu ni utumwa na ushamba ila nyinyi wake zenu kuvaa kilo tano za manyele ya marehemu kichwani (wigi) ndo ujanja na usomi?

Kuhusu watu kukalalamika huo ndo upumbavu wa waafrika kujaji na kuchukulia uzito mambo ya kipumbavu na yasiyo kuwa na athari kwenye maisha yake.
Yaani usiumizwe na ubadhirifu wa fedha na huduma mbovu ila uumizwe na hijabu uliyo kuta ameivaa muhudumu wa ofisi utakuwa na akili au utakuwa na funza kichwani?
 
Kama vipi aachane na Huo ukatibu Mkuu wa CCM ili aweHuru.
Huyo alishakuwa Naibu Katibu Mkuu UN hawezi kuwa na njaa, sijui kwanini kakubali huo utopolo wa Mbogamboga. Na hasikiki akibwabwaja ujinga ujinga kama Madelu, nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…