Huu ni uhuni mwingine wa serikali. Hawa waturuki na machinga wengine kutoka mataifa mengine hawana hata vibali vya kuishi nchini achilia mbali kufanya biashara
Hapa swali la msingi ni serikali imeanza kutoa vibali kwa wageni kufanya umachinga wa vyombo? Sheria za nchi zinaruhusu?
Ukitaka kujua hawana vibali, chelewesha malipo halafu mshauri aende kufungua madai mahakamani. Hana huo ujanja badala yake kuna baadhi ya viongozi hasa askari polisi wanakuwa wameshaunda nao urafiki. Hawa watu hawana hata jeuri ya kwenda kituo cha polisi
Kingine cha ajabu, wanatembea na siraha kwenye hizi Noah au bajaji wanazotembea nazo na ukitaka kujua ni wakorofi chelewesha malipo yao
Hili binafsi nimelishudia kwa jamaa mmoja aliyechukua vitu vyao kwa makusudi (hakua na lengo la kuvinunua) akivitunza kama vilivyo kwa zaidi ya miezi minne huku akiendelea kusumbuana nao kwenye malipo. Baadae akawaambia hana hela ya kulipa na vifaa vimeshahalibika hivyo waende kushitaki popote ataenda kujieleza
Wee...timbwili lake lilikuwa si la kitoto. Polisi hawataki kwenda badala yake wanawapigia mapolisi "wao" na kwa bahati mbaya simu hazikupokelewa. Uzuri jamaa alishaweka mitego yake ya kujilinda. Vurugu ilipozidi, walitokea watu waliokuwa wamekwisha andaliwa na jamaa wakawakamata wote ili wawapeleke central. Walioanza kuomba yaishe ni wale waturuki na hawakuwa tayari kufika kituoni
Hawana vibali vya kuishi nchini, hawana vibali vya kufanya kazi nchini wapo kihuni huni tu