Nani Karuhusu Waturuki kufanya umachinga wa kukopesha vyombo vya umeme mitaani? TBS na FCC mnayajua haya?

Nani Karuhusu Waturuki kufanya umachinga wa kukopesha vyombo vya umeme mitaani? TBS na FCC mnayajua haya?

HII NCHI ni shamba la bibi kama Teuzi wanapewa Wageni itakuwa kufanya biashara kiholele wacha Waturuki wajitafutie Riziki
Na wanakimbilia Tanzania kwa sababu wanajua ndio nchi ambayo Serikali yake inahamaisha Uchuuzi.

Hawawezi enda Rwanda wala Kenya,kwa kifupu ni wanakimbilia pale ambapo wanajua Mamlaka zina sapoti uchuuzi.
 
Hawa wanao jiita wawekezaji, serikali haiwaanhalii. Wanawaacha mpaka kwenye biashara ndogo ndigo kama hizo. Kungekuwa na limit unakuja kuwekeza atleast awe na duka kubwa
Serikali wapi? kwanza nchi tu Raia wake wana mentality za kichuuzi, achilia mbalia Serikali. Sasa njoo kwa Serikali inayo sapoti uchuuzi.

Hawa hawawezi enda Rwanda kwa kagame wala hapo Kenya. Kwa kifupi Africa nzima ni Tanzania ndio ina Serikali inayo sapoti uchuuzi. Nchi nyingine zina piga sana vita uchuuzi make hauna impact kwa uchumi wa ncni.
 
Watanzania si wabunifu halafu ni wavivu wa kufanya kazi, wacha Waturuki wapige kazi. Kama tatizo ni la ukaguzi basi lawama ni mamlaka zetu ambazo zimeoza maana zinaongozwa na wezi wa mitihani ya kidato cha nne 1998.
Ni watanzania wachache sana ambao ni wabunifu na wanaotaka kuumiza akili, the rest ni wavivu na kufunika uvivu huo wanakuja na terms mbali mbali, mapenzi ya Mungu, nimeridhika, kulaum serikali all the time
 
Serikali wapi? kwanza nchi tu Raia wake wana mentality za kichuuzi, achilia mbalia Serikali. Sasa njoo kwa Serikali inayo sapoti uchuuzi.

Hawa hawawezi enda Rwanda kwa kagame wala hapo Kenya. Kwa kifupi Africa nzima ni Tanzania ndio ina Serikali inayo sapoti uchuuzi. Nchi nyingine zina piga sana vita uchuuzi make hauna impact kwa uchumi wa ncni.
Serikal ikipiga marufuku uchuuzi labda kwa raia wa kigeni. Ila wabongo wenyew ewengi watalala njaa
 
Kama hawamdai!
Bhasi aone kama nao wameona Fursa ya uwekezaji kwenye kufanya kitu cha Tofauti, Si vizuri kuona Wivu "Envy" kwenye Kitu mwenzako anachofanya kwa kuingiza kipato wivu uwe wa kufanya zaidi yake na sio kumuharibia
Wanaingiza viapato kwao au kwa Serikali? Hapo wana toa pia somo, watoto wakimaliza shule wanatamani kuwa wachuuzi pia. Nchi hii ni ya ajanu mno, hawa hawawezi enda Kenya mkuu make kule mamlaka hazisapoti uchuuzi.
 
Serikal ikipiga marufuku uchuuzi labda kwa raia wa kigeni. Ila wabongo wenyew ewengi watalala njaa
Wanalalaje njaaa? Tunatengeneza Taifa legelege ambali kutumia akili ni hakuna, Uchuuzi unaoigwa cira kokote kule, moja ya sababu ni kuwafanya raia wawe crative.
Ndio maana kwenye uzalishaji hakuna kitu kila mtu ndoto zake ni kumilik Frame
 
Wanaingiza viapato kwao au kwa Serikali? Hapo wana toa pia somo, watoto wakimaliza shule wanatamani kuwa wachuuzi pia. Nchi hii ni ya ajanu mno, hawa hawawezi enda Kenya mkuu make kule mamlaka hazisapoti uchuuzi.
Mkuu ulitaka waingize kipato kwa serkali badala yao?
Unafikiri wanaweza kuwepo hapa bila Serkali kujua?
Kumbuka wana Visa, Wana Permit, na Balozi zao zinajua wamekuja kufanya nini!

Kwahyo tuilaumu serkali yetu tu kwa hilo
 
Niliona wanasambaza blenda mitaani ila vitu vyao ni very expensive na overpriced.

Wanakopesa blenda "heavy duty" sh 300,000. Wakati ni counterfeit..zinauzwa hapo kariakoo hadi sh 55000.

Hotpots zao hao waturuki wanakwambia laki 4-6.
Sasa nani huyo mjinga anunue blenda laki tatu, hata kama unakopeshwa.
 
Huu ni uhuni mwingine wa serikali. Hawa waturuki na machinga wengine kutoka mataifa mengine hawana hata vibali vya kuishi nchini achilia mbali kufanya biashara

Hapa swali la msingi ni serikali imeanza kutoa vibali kwa wageni kufanya umachinga wa vyombo? Sheria za nchi zinaruhusu?

Ukitaka kujua hawana vibali, chelewesha malipo halafu mshauri aende kufungua madai mahakamani. Hana huo ujanja badala yake kuna baadhi ya viongozi hasa askari polisi wanakuwa wameshaunda nao urafiki. Hawa watu hawana hata jeuri ya kwenda kituo cha polisi

Kingine cha ajabu, wanatembea na siraha kwenye hizi Noah au bajaji wanazotembea nazo na ukitaka kujua ni wakorofi chelewesha malipo yao

Hili binafsi nimelishudia kwa jamaa mmoja aliyechukua vitu vyao kwa makusudi (hakua na lengo la kuvinunua) akivitunza kama vilivyo kwa zaidi ya miezi minne huku akiendelea kusumbuana nao kwenye malipo. Baadae akawaambia hana hela ya kulipa na vifaa vimeshahalibika hivyo waende kushitaki popote ataenda kujieleza

Wee...timbwili lake lilikuwa si la kitoto. Polisi hawataki kwenda badala yake wanawapigia mapolisi "wao" na kwa bahati mbaya simu hazikupokelewa. Uzuri jamaa alishaweka mitego yake ya kujilinda. Vurugu ilipozidi, walitokea watu waliokuwa wamekwisha andaliwa na jamaa wakawakamata wote ili wawapeleke central. Walioanza kuomba yaishe ni wale waturuki na hawakuwa tayari kufika kituoni

Hawana vibali vya kuishi nchini, hawana vibali vya kufanya kazi nchini wapo kihuni huni tu
Huyo rafiki yako kichwani siyo mzima.
 
Wanalalaje njaaa? Tunatengeneza Taifa legelege ambali kutumia akili ni hakuna, Uchuuzi unaoigwa cira kokote kule, moja ya sababu ni kuwafanya raia wawe crative.
Ndio maana kwenye uzalishaji hakuna kitu kila mtu ndoto zake ni kumilik Frame
Wewe ni mgeni na hii nchi. Wamachinga tu wenyewe wameshindwa kuwa manage, kama kuwa legelege wameshakuwa legelege, uki block wamachinga now idadi ya wasio kuwa na ishu za kufanya mtaani itaongezeka. Thats the reality

Labda kama una namna ieea nyingine how to regulate hii kitu iwe na faida kwa jamii. Eitherway kwa jamii ya kitanzania bado sana
 
Waafrika tuache kulalamika kwa kuwa tumeamua kubweteka na kuishi kama full time consumers...

Tukitaka vitu bora, tujifunze kuunda vitu vya kwetu wenyewe...
Hakika
 
Hivyo vitu fake vipi kwao Waturuki tu mkuu au una lingine mkuu? Au ni hisia kwamba wanachukua ajira za Watanzania yaani mpaka umachinga wanafanya wao?

Kama issue ya bidhaa fake, je ukienda kwenye maduka mengine mbali na Waturuki hakuna bidhaa fake?

Kama ni issue ya umachinga wao, je kabla ya kuja wao kuanza na huu ubunifu wa kuuza vyombo Kwa mkopo, je Kuna Mtanzania yoyote alikuwa anaifanya hii kazi ya kukopesha vyombo kiasi kwamba anaingilia maslahi ya Watanzania?. Ukiangalia Kwa makini utagundua huo ni ubunifu wao na unarahisisha upatikanaji wa vyombo vya kielektroniki Kwa urahisi japo gharama inakuwa juu Kwa kuwa ni mkopo.

Suruhisho si kuwalaumu bali na wewe ingia road Kwa style/ubunifu mwingine ambao utauza Kwa wananchi maana Watz wengi hawakuwa wanafanya biashara ya mtindo huu wa mkopo ambapo mtu anachukua vyombo ANATUMIA huku ANALIPA KIDOGO KIDOGO bali ilikuwa mtu ANABANDIKA yaani UNALIPA KIDOGO KIDOGO ukimaliza ndo unachukua bidhaa.

Mie nachukulia kama UBUNIFU hivyo na nyie muige
 
Wana JF.

Si kwa nia mbaya maana waturuki wametoa ajira lakini kuna haya.

Waturuki wamekuwa wakizunguka mitaani na bajaji wakikopesha vyombo mbali mbali. Msala wangu kwao ni kwamba, nani ametoa kibali cha ukaguzi wa vyombo vyao vya umeme?

Kama kuna mtu wa TBS na FCC inabidi kwa pamoja kuchunguza vifaa vinavyosambazwa na waturuki wanaofanya kazi zao kama wamachinga. Waturuki wana bajaji nyingi zinazunguka mjini nyumba kwa nyumba wakikopesha vifaa mbali mbali vya umeme.

Hasa Rice Cooker na Multicooker. Vifaa vingi vinavyotumia moto, hasa wakati wa kupika vimekuwa nyaya za machine zinapata moto kiasi cha kuyeyuka na kusababisha hatari ya kuunguza nyumba. Ni kweli Tanzania ni dampo kuu la vifaa vilivyoigiziwa na kufanywa original , lakini vingi vinaingizwa kwa njia ya panya.

Hipo haja ya kupita nyumba kwa nyumba na kukagua vifaa vya umeme vya majumbani. Hapa tutaepusha nyumba kuwa zinaungua hovyo na kusababisha uharibifu mkubwa wa vitu. Kama FCC na TBS wasipochunguza vifaa vya umeme vinavyoingizwa nchini. Basi tutegemee nyumba nyingi kuungua.
Ze kantri nao iz like a headless chicken...

Tunakwenda bila kuenda
 
Wewe nunua katumie

Watumiaji/wanunuzi wenyewe hatuna viwango vya TBS....
Juzi multicooker ilitaka kuunguza nyumba na sijamaliza deni lao. Nawasubiri nikawatupie dude lao. Wakisumbua nitawaambia wakanishitaki.
 
Back
Top Bottom