Nani kasema Nguruwe halali? Sio Ukristo au Uislamu kote wamemkana.

Motoni utaenda kwa mchanganyiko wa dhambi nyingi nguruwe ikiwa moja wapo
 
Upo sahihi
Mie nawaonaga watu wanahangaika kuwa dini yao ionekane Safi wakati hata upendo tu wa kusaiidia wenye uhitaji anashindwa akikutana na mke wa mtu anapata hisia anatongoza anapiga anajificha baadaye anakuja kukomaa hapa kuwa kitimoto ama dini yetu Ni Safi na ndio Mungu amesema tusali anapaimbia.
Analeta swala la yanga vs Simba or cdm vs ccm.

Dini Ni your lifestyle na Tabia zako na mwenendo wako kiujumla kwenye maisha yako ya kila siku.

Usidhani dini Ni kuwa mbudha,mhindu,mkristo ,mwislamu.
Na dini zote za dunia hii zinafundisha UPENDO NA AMANI . Zingine Ni mbwembwe tu za kujisifia kuwa mie wa kwangu Ni Bora kuliko wa kwako
 
Katika Agano JIPYA Nguruwe ni ruksa kuliwa! Baada ya Kristo kuja vyakula vyote vilivyohesabika ni najisi katika Torati(Agano la KALE)-Walawi 11:4-43),alivitakasa kwa Neno la Mungu,(Marko7:16-19)-Yesu akasema,Kimuingiacho mtu hakimtii mtu unajisi,bali kimtokacho.Kwa kusema hivyo alivitakasa vyakula VYOTE.Na tena Neno la Mungu linasema,vilivyotakaswa na Mungu wewe usiviite Najisi,(Matendo9:11-16)
Vimtokavyo mtu ambavyo vyaweza kumtia mtu unajisi ni vile vitokavyo moyoni,yaani maovu au dhambi,(Marko7:21-23)
Kwa hiyo kama mtu hali nguruwe lakini anafanya maovu mf.uzinzi,ulawiti,ufiraji,uuaji,wizi,kinyongo,matusi,Uongo,nk mbele za Mungu huyo ni Najisi.Na walio najisi wote mahali pao ni katika lile ziwa la moto liwakalo kiberiti,(Ufunuo21:8)
Soma,(Warumi14:14).Kwa hiyo ni ruksa kula Kitimoto bila wasiwasi! Na usisikilize roho za majini zisemazo usile hiyo kitu,unachotakiwa ni kushukuru tu then unaendelea kula,(1Timotheo4:1-5)
 
Mnasomaga maandiko gani hayo? Sisi hatufuati maagizo ya Walawi, sisi tunafuata maagizo ya Yesu Kristo. Wanangu pigeni kitimoto kama kawa ni nyama halali kabisa! Nenda kasome Marko 7:14 -23 Uone jinsi Yesu alivyoturuhusu kula kila kitu maana vituingiavyo kutoka nje havitutii unajisi!
 
Kama una imani basi utaelewa tu chochote Mungu Alichokataza basi kina madhara.

Kama una imani lkn....au nasema uongo swahiib?
 
Motoni utaenda kwa mchanganyiko wa dhambi nyingi nguruwe ikiwa moja wapo
Naacha rasmi kujibizana nawe.

Huna hoja isipokuwa mihemko tu kwa vile umeanzisha uzi.

Kama wewe ni Mkristo unakufuru sana unapoidharaulisha damu ya Yesu iliyomwagika msalabani kwa ajili ya wokovu wetu kwa kuilinganisha na nguruwe...

I am out 🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️
 
Wewe endelea kula tende ulizoagizwa na Mungu wako, tuache na kitimoto yetu, sisi siyo Walawi wala waarabu, kumbuka hata wamasai wangefanikiwa kueneza Imani yao Hadi mtwara na kwingine kungekuwa na katazo la kuto kula samaki Toka kwa Mungu
 
Asante mkuu tumewaza pamoja! Tumemjibu vya kufanana! Asante sana!
 
Kama una imani basi utaelewa tu chochote Mungu Alichokataza basi kina madhara.

Kama una imani lkn....au nasema uongo swahiib?

Kwenye Ukristo mambo ni tofauti siyo kama huko kwenu ambako sijui wokovu unapatikanaje.

Huku kwetu wokovu unategemea Neema ya Mungu kupitia kwa damu ya Mwana wake Yesu Kristo na siyo haya maelfu ya sheria za Musa.

Siwezi kwenda motoni kisa nilikula bata, kambale au kitimoto!
 

Hizi dini hizi acha tu..

Walipokataza nguruwe asiliewe kwakua hecheui, ndio hapohapo wamekataza ngamia na sungura na wanyama wengine wasio na kwato wasiliwe.

Wewe unakula ngamia hamna shida, na wala nguruwe hawakupigii kelele, kwann wewe unawapigia wao kelele?
 

 
Una hoja usikilizwe
 
Hatumjadili ngamia hapa upo nje ya mada
 
Kwahyo unatenda dhambi kwa kutegemea uokovu wa yesu si tuliambiwa kila mtu atabeba msalaba wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…