Nani kasema Nguruwe halali? Sio Ukristo au Uislamu kote wamemkana.

Nani kasema Nguruwe halali? Sio Ukristo au Uislamu kote wamemkana.

We! huyu mdudu mtamu asikwambie mtu, ukikutana na yule OG kwa sababu saa hivi kuna mabroiler ya nguruwe, hayo ndo yamefanya niache kula.
Ila hiki kiumbe sio poa, napendaga rosti ichanganywe na ndizi
 
Kuna mambo ambayo yana madhara ya moja kwa moja kwa Jamii na kwa mtazamo wangu hayo ndio yangewekwa mbele mbele sana kwenye mahubiri kuliko kuzungumzia Nguruwe sijui siku ya kusali ni ipi kwa mtazamo wangu ni mambo mepesi mno kulinganisha na
Ufisadi
Ujambazi
Mauaji
Uasherati
Mapenzi ya jinsia moja
Uonevu
Kusaidia wasiojiweza
 
Wakuu hii threads haihusiani na masuala ya imani za kidini, ni katika kujiuliza tu; ni kwanini Wanyama hususani jamii ya nyani ambao ndio tunashabihiana nao sana, hawatumiwi sana katika tafiti za tiba kwa ajili ya kupata viungo vya kupandikizwa watu wenye mahitaji ya viungo kama; figo, moyo, ini, mapafu, macho nk ??, nikiwa katika hamu ya kujua jambo hilo nikabahatika kuingia kwenye mtandao na kuona; Indian journal of Urology, ambamo nakakuta "thesis" yenye kichwa cha habari hii; "The potential advantages of transplanting organs from pig to man".

Humo nikapata jibu la swali langu; kwanini jamii ya nyani haitumiki katika tafiti kupata viungo kwa ajili ya watu??--- jibu lilikuwa hili; (1) Risk of Virus and (2) most primates are classed as endangered species.--- hizo ndizo sababu kuu mbili jamii ya nyani hawatumiwi katika huo utafiti.

Badala yake nikaona maneno haya; "Pigs Organs are ANATOMICALLY similar to human organs".

Hapo nimejifunza kitu kwamba; viungo vya nguruwe bali hata nyama yake inashabihiana (similar in anatomy) na viungo na nyama ya mtu, hoja ni hii; je tukisema kula.nyama ya nguruwe na viungo vyake ni karibu (similar) na kula nyama ya mtu hapo itakuwa ni kosa??!.

NB: Tafiti bado zinaendelea ili kufanya viungo vya nguruwe visiwe rejected na recepient immune system kwasababu hicho hadi sasa ndio kikwazo kikubwa watafiti wamekuwa wakipambana nacho, waila katika jambo hilo kama watafiti watafanikiwa basi kitimoto atapanda thamani kubwa sana duniani kuliko hivi sasa anavyokuwa "cannibalised" na watu.

Nawasilisha.
 
Kuna mambo ambayo yana madhara ya moja kwa moja kwa Jamii na kwa mtazamo wangu hayo ndio yangewekwa mbele mbele sana kwenye mahubiri kuliko kuzungumzia Nguruwe sijui siku ya kusali ni ipi kwa mtazamo wangu ni mambo mepesi mno kulinganisha na
Ufisadi
Ujambazi
Mauaji
Uasherati
Mapenzi ya jinsia moja
Uonevu
Kusaidia wasiojiweza
Hiyo na sio hoja ukitaka siasa nenda jukwaa lake
 
Inakusaidia nini wewe hiyo hoja? Hapa nimeagiza nusu ROSTI wewe subiria hoja..!! Nashushia na gambe basi mwaaah..!!

By the way, hivi mbona bia mnakunywa hadharani na huku ni haramu kwenu? ACHENI UNAFIKI WA KUDHANI KITIMOTO NDO DHAMBI PEKEE KWENU ...!!
Tetea kwa hoja acha makasiriko
 
Katika dini ya Ukristo, maandiko matakatifu ya Biblia yanapinga ulaji wa nguruwe kwa sababu inachukuliwa kuwa ni mnyama najisi.

Hii inapatikana katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11:7-8 ambapo inasema " Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi. .Hamtakula nyama yao, wala hamgusi mizoga yao. Hao ni najisi kwenu."

Pia, kuna vifungu vingine vinavyopinga ulaji wa nguruwe kama vile Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 14:8 ambacho kinapinga ulaji wa nguruwe, na Matendo ya Mitume 15:28-29 ambayo yanahimiza waumini kuepuka kula nyama iliyotolewa kwa sanamu na damu.

Kwa upande wa Uislamu, Quran inapinga ulaji wa nguruwe na inachukuliwa kuwa ni haramu kwa Waislamu. Kifungu cha Quran Surat al-Baqarah 2:173 kinakataza ulaji wa nguruwe pamoja na nyama ya wanyama waliochinjwa kwa njia ya kuchinjwa bila kumtaja Mungu, damu, nyama ya wanyama wanaouliwa kwa sababu ya miungu, na wanyama waliofariki kwa kifo cha asili. Kwa hivyo, Waislamu wanachukulia ulaji wa nguruwe kama jambo la kinyume na mafundisho ya dini yao.


NB: TUJADILI KWA AYA NA VIFUNGO MBALIMBALI ZA VITABU MBALIMBALI VYA DINI NGOJERA HAZITAKIWI.

View attachment 2613342
mfungo wa Ramadan huwa kitimoto kinadoda sokoni
 
Back
Top Bottom