Nani kasema Nguruwe halali? Sio Ukristo au Uislamu kote wamemkana.

Hapo umevaa suruale ya mchina shati la muitaliano, kiatu cha mrusii....... Hizo dini mtajuana wenyewe kikubwa najua mie ni wa asili wa hili bara na huyo mdudu kwangu sio haramu baaas,,,,, dini tunadandia tuonekane bado tupo pia,,,,, waafrika tuna matatizo makubwa zaidi ya kuanza kubishania kitoweo
 
 
Marko 5:12-14

Neno: Bibilia Takatifu

12 Wale pepo wakamsihi Yesu, “Turuhusu tukawaingie wale nguruwe.” 13 Basi akawaruhusu. Wakamtoka yule mtu wakaenda wakawaingia wale nguruwe na kundi lote la nguruwe wapatao elfu mbili likatimka kasi kwenye mteremko ule, wakazama ziwani, wakafa.

14 Wale waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotokea. Watu wakatoka kwenda kujionea mambo hayo.


Neno la Bwana!
 
Hyo haihalalishi unajisi wake
 
Kwa hiyo wale nguruwe ndiyo hawa tulio nao wanaishi hadi leo? Au wale walikufa palepale?
 
Kasome historia hapa tunazungumzia dini na sio mila
Halali ni nini au unadhani Dini na Imani zilianza na Ukristo na Uislamu ? Unadhani ni Middle East na Wayahudi pekee ndio walioamini; Huko Asia na Afrika walikuwa hawana Imani ?

Unapotumia sehemu ya Imani ya wachache ku-generalize wote nadhani anayehitaji kusoma Historia ni wewe
( By the way Dini sio Historia ni Imani na unaweza ukaamini chochote unachotaka)
 
Akili zako mbovu na ulivyokaririshwa ndiyo zinakuelekeza ni najisi.Ninyi endeleeni kupiga umalaya kwa kujidai waimba kwaya.
Huyu atakuwa ni Msabato. Wana tabia ya kunyofoa nyofoa visheria vichache vya Musa na kuacha zingine maelfu kwa maelfu. Hawali nyamafu. Hawali wanyama wasiocheua. Hawali wanyama wasio na kwato. Hawali samaki wasio na mapezi. Hawaruhusu wanawake kusuka, kujipamba wala kuvaa hereni...na utopolo mwingine mwingi. Sijui kwa nini wamechagua hizi chache na kuacha zingine maelfu. Pengine ni maelekezo ya nabii wao Ellen G. White!

Biblia iko wazi kwamba Yesu Alikuja ili tuondokane na masheria haya ya Musa ambayo mengi yamepitwa na wakati isipokuwa tu zile amri 10 ambazo ndiyo Moral law kwa jamii nyingi.

➡️➡️➡️ Hakuna mtu atakayekwenda motoni kisa kitimoto, alikula bata au kambale......
 
Halafu hawa wanaokuwa wanafunguliwa na kujichunga wenyewe nyama yake huwa ni tamu sana.
Naomba unipatie location ya ulipo wapata mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…