Nani kasema Nguruwe halali? Sio Ukristo au Uislamu kote wamemkana.

Katika dini ya Ukristo, maandiko matakatifu ya Biblia yanapinga ulaji wa nguruwe kwa sababu inachukuliwa kuwa ni mnyama najisi.

Hii inapatikana katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11:7-8 ambapo inasema " Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi. .Hamtakula nyama yao, wala hamgusi mizoga yao. Hao ni najisi kwenu."

Pia, kuna vifungu vingine vinavyopinga ulaji wa nguruwe kama vile Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 14:8 ambacho kinapinga ulaji wa nguruwe, na Matendo ya Mitume 15:28-29 ambayo yanahimiza waumini kuepuka kula nyama iliyotolewa kwa sanamu na damu.

Kwa upande wa Uislamu, Quran inapinga ulaji wa nguruwe na inachukuliwa kuwa ni haramu kwa Waislamu. Kifungu cha Quran Surat al-Baqarah 2:173 kinakataza ulaji wa nguruwe pamoja na nyama ya wanyama waliochinjwa kwa njia ya kuchinjwa bila kumtaja Mungu, damu, nyama ya wanyama wanaouliwa kwa sababu ya miungu, na wanyama waliofariki kwa kifo cha asili. Kwa hivyo, Waislamu wanachukulia ulaji wa nguruwe kama jambo la kinyume na mafundisho ya dini yao.

NB: TUJADILI KWA AYA NA VIFUNGO MBALIMBALI ZA VITABU MBALIMBALI VYA DINI NGOJERA HAZITAKIWI.

View attachment 2613342
Mbona umemsahau Ngamia ni haram lakini jamaa wanafakamia hadi maziwa yake
 
Screenshot_20230507-163139_Google.jpg
Screenshot_20230507-163158_Google.jpg
Screenshot_20230507-163216_Google.jpg
Screenshot_20230507-163243_Google.jpg
Screenshot_20230507-163310_Google.jpg
 
Hiyo ilimtokea petro tu, swali nawe kawatakasa kakwo leta andiko
Kwa hiyo kuna mafungu ya Biblia yanamhusu Petro pekee? 😳😳😳

Kama ni hivyo basi karibia nusu ya Biblia itabidi tuipuuze maana habari zake nyingi zinahusu maisha ya watu - ambao kwetu tunapaswa kuwaona kama mifano....Mitume na mashujaa wa imani!

Na hili ni Agano jipya ambalo lilikuja kutengua yale masheria maelfu na maelfu ya Musa (kubakiza moral law - Amri 10 za Mungu); na likasema wazi kwamba tutakwenda mbinguni si kwa kufuata masheria yale ya kutokula nyamafu, samaki wasio na mapezi, wanyama wasio na kwato, wanyama wasiocheua na utopolo mwingine!

Hitimisho:

➡️➡️➡️ Hakuna mtu atakayekwenda motoni kwa sababu eti alifakamia Mbuzi wa Vatican....
 
Mababu zetu enzi zile walisemaje ? Au wao hawakupata Memo kuhusu haya mambo mpaka yalipoletwa na Merikebu ?
 
Back
Top Bottom