Mkuu acha watu watafute maisha. Wamalawi wanachapa kazi ambazo waswahili wengi hawawezi. Wengi wapo very professional, wanathamini kazi. Watanzania wengi sisi ni wajanjawajanja. Unataka wafukuzwe hizo kazi utafanya wewe? possibly not. kwa nini uumie mtu kutumia nguvu na akili yake kujipatia riziki? hii mipaka iliwekwa na wajinga fulani huko Berlin kwa maslahi yao. Kuna ndugu zako wako SA, US, UK , Canada hawana vibali lakini wanapambana. Ndo hao wanasaidia ndugu zao hapa TZ na kwingineko.
Mpaka leo sioni sababu ya mwafrica kuwa mkimbizi Africa. wacheni vijana watafute maisha. Na wewe ukitaka nenda Congo au kwingineko. Ilmradi usiibe cha mtu.
Mwisho wa siku wakifanya makosa waadhibiwe kama wengine. Ila tusiwahukumu tuu kwa sababu wanaitwa wamalawi. It is just a name!
Africa maisha ni magumu sana. ukiona mtu ana hustle mheshimu baada ya kumfitini.