Leo hii tarehe 29 July 2024 Mzee kinana amejiuzuru nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.
Abdulrahman Kinana ni miongoni mwa viongozi mahiri waliowahi kutokea katika historia ya CCM na alifanya kazi kubwa sana ya kukiimarisha wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 hivyo pamoja na kijiuzuru kwake bado CCM itaendelea kumuhitaji.
Kama mwana CCM nimeona ni vyema nitoe ushauri,maoni na mapendekezo yenye tija kwa ustawi wa Chama hasa wakati huu tunakoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji 2024 pamoja na uchaguzi mkuu 2025
Nitaangazia options mbalimbali zinazoweza kuchukuliwa na CCM ili kuhakikisha anapatikana Mwana CCM mahiri ili kujaza nafasi hiyo.
1.Dr Bashiru
Ally
Binafsi ningependa Dr Bashiru Ally Kakurwa ambaye amewahi kuwa katibu mkuu wa CCM anajaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.
Ni ukweli ulio wazi kuwa kama CCM inamhitaji mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo nyeti ya uongozi basi Dr Bashiru aweze kuangaliwa kwa jicho la tatu.
Dr Bashiru hana uhusiano wowote na makundi ndani ya CCM,amewahi kuwa katibu mkuu wa CCM hivyo anakijua chama vizuri,ni msomi mbobezi, Mwadilifu,bado ni kijana, hajapitwa na wakati na bado anazungumza lugha ya wapiga kura tulionao.
Dr Bashiru ni vocal,ni kiongozi asiyeyumbishwa, ni muumini wa siasa ya ujamaa na kujitegemea.
Tunao wazee wastaafu kama vile Stephen Wasira na Mizengo Pinda lakini ni vyema hawa waendelee Kula pension zao.
2.William Lukuvi
Huyu naye anaweza kufikiriwa hasa kutokana na seniority aliyonayo na kwa kuangalia historia yake ya muda mrefu kwenye Chama na serikalini.
3.Tunao wazee wastaafu kama vile Stephen Wasira na Mizengo Pinda lakini ni vyema hawa waendelee Kula pension zao.
4.Rajab Abdulrahman Abdallah- Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga na Mjumbe wa CC
Huyu ameanza kufanya kazi nzuri tokea alipochaguliwa hivi karibuni kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga.
Pamoja na hayo nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni kubwa kwake na sina hakika kama anaweza kumudu majukumu mazito ya kitaifa.
5.Dr Emmanuel Nchimbi.
Huyu ni katibu mkuu wa sasa wa CCM na anafanya Kazi vizuri sana.
Naamini ataendelea kushika nafasi ya ukatibu mkuu angalau mpaka baada ya uchaguzi mkuu ujao 2025.
Hatahivyo Chama kinaweza kumpandisha kuwa Makamu mwenyekiti na nafasi ya katibu mkuu ikajazwa na kada mwingine na kama hili litatokea basi wafuatao wanaweza kurithi mikoba ya ukatibu mkuu.
A.Hussein Mohamed Bashe
kwa maoni yangu huyu ndiye waziri Bora katika Baraza la mawaziri kutokana na kazi kubwa anayofanya kama waziri wa kilimo .
Bashe japo ni mwanasiasa lakini ni administrator mzuri na shughuli za utendaji amefanya kwa muda nrefu.
Tatizo ni kuwa endapo Bashe atateuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM itakuwa ni kazi ngumu kumpata mtu nwingine anayeweza kujaza nafasi ya waziri wa kilimo kutokana na sababu kuu mbili,kwanza ni kwasababu wizara ya kilimo chini ya Bashe ndiyo wizara active kwasasa na isitoshe huko kilimo kuna agenda nzito za kitaifa kama vile Building Better Tomorrow ambayo yeye ndiyo mwasisi.
Huyu ameonyesha uwezo mkubwa sana na haitakuwa Jambo la ajabu kama atapata nafasi kubwa zaidi ya uongozi ndani ya Chama au serikalini Katika siku za usoni
Outsiders
B.Antony Mtaka,Amos Makala,John Mongela , Martin Shigela,Dr Galila Wabanhu na Dr Suleiman Jaffo
Hawa pia wanaweza kufikiriwa
Naomba kuwasilisha