Pre GE2025 Nani kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara baada ya Mzee Kinana kujiuzulu?

Pre GE2025 Nani kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara baada ya Mzee Kinana kujiuzulu?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM TUKO IMARA .,. GOODMORNING , CHAWA WAKUU NDIO TUNAAMKA 😂 TUACHIENI CHAMA CHETU TUKIWEKE SAWA. MKIJA KUSTUKA MSHAPIGWA GOLI NANE , KIPA HAELEWEKI ANALINDA NINI. VIVA CCM , VIVA MAKADA WOTE. CCM HAITOKOSA USHINDI TANZANIA HII MIAKA YOTE .
 
Pinda anamfaa sana na atafaa kukivusha chama cha CCM
 
Siasa za bongo kuzielewa inabidi uwe bilionea kwanzq ndio utazielewa vinginevyo itakuwa kama kujaribu kumuelewa mwanamke
Kweli kabisa.
Askofu Gwajima anawaambia wananchi "mbunge sio kiongozi wa serikali " ila anachaguliwa kama muwakilishi wa wananchi tu.
Nkajiuliza swali kwenye somo la uraia tulifundishwa mihimili 3 ya dola 1)raisi 2)mahakama 3)Bunge
Wabunge ndo hutunga sheria
 
A
MWENYEKITI asijisahau kuwa wengi wanaotaka kumuangusha sababu zao kuu ni mbili tu,JINSIA yake na UZANZIBARI wake.
Hata ukimuuliza CHEMBA Leo Kwa nini hamumtaki Mama atakwambia hivyohivyo tu.
Hawana sababu nyingine.
Kwa nafasi hii muhimu,Achaguliwe MWANAMKE tena feminist hasa.
Muhimu aweze kukosoa bila hofu.Asiwe na makundi,anayeheshimika na watu wote ndani na nje ya CCM.Mwenye haiba na mzungumzaji mzuri.
Anayeweza kujibu Hoja na msomi.
Dawa ya moto ni moto.
Mimi naenda na ANNA TIBAIJUKA.
Asha Rose Migiro
 
MTANDAO ULIOKUWA UNAITAFUNA SERIKALI NA KUANDAA MAPINDUZI NDANI YA CCM NA SERIKALI KUELEKEA UCHAGUZI WA 2025 NA 2030

WAKATI TANZANIA imepata ahueni kubwa sana kwa tukio la hivi karibuni la kufukuzwa kazi kwa mawaziri wawili Nape Nnauye na January Makamba kwa tuhuma nyingi sana zilizokuwa zinawakabili na kubwa ni mipango yao ya kuhujumu urais wa Rais Samia na kutaka kuendesha mapinduzi ndani ya CCM kimya kimya kabla ya 2030 ni wakati sawa washirika wao kuwekwa hadharani wajulikane bayana.

Kikosi hiki kilikuwa na mtandao mkubwa sana ndani ya Ikulu na ndani ya vyombo vay usalama vya nchi na ndani ya CCM ambako kote huko limepita fagio la chuma na kuwakumba watu kadhaa wakubwa kwa wadogo lakini kwa kifupi ni kuwa nyumba imesafishwa vibaya sana.

January Makamba aliunda ,aliufadhili na kuuendesha mtandao hatari sana ndani ya serikali wa kuhujumu serikali na kumhujumu Rais Samia ndiyo maana alikuwa na uwezo wa kukutana na kufanya vikao na watu wake hawa nje ya Tanzania kwa gharama kubwa sana ya fedha za wizi alizonazo.

Moja ya mipango michafu na ya kuogopesha sana iliyokuwa inapangwa na kuratibiwa na watu hawa ni kuwa kwa vyovyote vile January Makamba lazima awe Mgombea Mwenza wa Rais Samia kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 na baadaye awe Makamu wa Rais kwa kuwa hilo linamsogeza karibu sana kuwa Rais mwaka 2030 au kuwa Rais kikatiba kama lolote litatokea. Yote hii ilikuwa inapangwa na mtandao huu kwa kuwa January Makamba hana nafasi hata bila kufukuzwa kuwa Mgombea wa Urais wa CCM mwaka 2030.

Suala la kuwa Makamu wa Rais na mawazo ya kuwa lolote linaweza kutokea kabla ya Rais Samia kumaliza muda wake mwaka 2030 ili January Makamba awe Rais wa Tanzania ndilo loliloshangaza na kustua watu wengi baada ya mipango ya mtandao huu hatari kuvuja.

Hofu ilitanda zaidi baada ya kujua mtu wa hovyo kama January Makamba amewezaje kusuka mtandao hatari kiasi hiki kwa zaidi ya miaka miwili bila kujulikana mpaka madhara ya mtandano huu yakaanza kuonekana dhahiri ndani ya serikali na CCM.

Hatuwezi kuacha watu hawa waliokuwa kundi na wanamtandano wa January Makamba bila kuwataja hadharani na kujulikana mbinu zao chafu na hujuma walizokuwa wanafanya dhidi ya serikali na Rais Samia.

Japo kiongozi wa waasi hawa January Makamba ameuwawa kabla vita haijaanza hatuwezi kuacha kuwataja wanajeshi wake ili waingie kwenye kumbukumbu kwa kuwa bado wako ndani ya CCM na serikali na wana madhara na lazima fagio la chuma liwapitie:

Wana mtandano hao ni hawa wafuatao;

1. Mzee Dullah Kinana
2. Mariam Ditopile
3. Balozi Togolani Mavura
4. Adama Malima
5. Nehemia Mchechu
6. Balozi Ombeni Sefue
7. Catherine Magige
8. William Lukuvi

Watu hawa ni waasi na wapinzani ndani ya serikali na wanamtandao waliokuwa wanachakata mipango ya kuhujumu nafasi ya urais ili January Makamba akne kwenye kiti hicho haya kama ni kwa mbinu za hila,nani kwetu sisi tunadhani ni dhambi kuacha na kutowataja na kuwasema hadharani ili wajulikane.

Wakati wahusika wakuu wamefukuzwa akiwemo mkubwa wao na ''master planner'' ni vyema tukajua kuwa hawa tumebaki nao kwenye mifumo ya serikali na ni hatari na sumu mbaya sana.

#KigogoMediaUpdates
 
Polepole arudi.
Atakuwa ameshapata mafunzo tosha toka Cuba.
Ikumbukwe nchi yetu ni ya kijamaa.
Japo hapo katikati ni kana kwamba walitaka kuifanya ya Kibepali chini ya mabepali wachache.
Polepole atafaa sana kwenye hii nafasi.
 
kama atampa pinda nafasi hiyo, katibu abadilishwe maana naona katibu wa ccm wa sasa nafasi hiyo haimtoshi.
kinana tangu alivyokua katibu alikua na busara,ukali, na maamuzi magumu aliyaweza. maana nakumbuka jadi mwenyekiti wake jk aliweza kumsema kama kuna makosa.
sasa katibu hasikiiki mwenyekiti ndio huyo halafu makamu nae akiwekwa mwenye busara tu bila ya kua mkali hapo wataruhusu wale vijana watukutu(wahuni) wapate nafasi ya kusumbua.
kama atampa pinda nafasi hiyo katibu atumbuliwe.nafasi hiyo haimtoshi.kalala sana.
 
Back
Top Bottom