Darubini ndio nyimbo iliyompa ufalme Afande Sele, darubini ilitoka kabla ya shindano na sio baadaDarubini ilitoka baada ya kupewa tayari ufalme was rhymes lakini kwenye mashindano aliingia na wimbo mtazamo ambao aliwashirikisha wasanii Wawili.Afande sele alibebwa sana katika ushindi ule kwa kuchukuwa wimbo ambao tyr alibebwa pia
Acha ubishi darubini ilitoka kabla ya shindano na ndio nyimbo iliyombeba afande hadi akatwaa tunzo... Dito alipanda jukwani kuperform darubini akiwa bado yupo primary...Wewe hauna kumbukumbu nzuri labda.Afande sele baada ya kushinda akaachia ngoma yake ya Darubini kali ambayo ilifanya vizuri sana kwenye chat za bongo nadhani hapa ndo unajichanganya na kuzania ilitoka kabla ya mfalme wa rhymes.
Mtazamo ilikuwa kabla ya mashindano na ndo nyimbo aliyoingia na Sele.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Mkuu mbona hujamjibu?
Niliandika mada kama yako miaka michache nyuma...hii hapa..
NANI HASA ALISTAHILI UFALME WA RHYMES MWAKA 2004?
Shindano la kumsaka mfalme wa Rhymes katika bongo flava ni moja ya shindano lililopata msisimko mkubwa kwa kipindi hicho, hii inawezekana ilitokana na kukutanishwa manguli wa muziki kwa kipindi hicho hali iliyopelekea uamuzi wa nani ashinde kuwa mgumu wa walio wengi!
Shindano liliwakutanisha
1. Jay moe(kama unataka demu)
2. Afande Sele(Darubini kali)
3. Prof J(Msinitenge)
4. Inspector Haroun (Bye Bye)
5. Solo Thang(Simu yangu)
6. Madee(Kazi yake Mola)
7. MwanaFA(Alikufa kwa ngoma)
8. Mandojo na Domokaya(Nikupe nini)
9. Soggy Dogy(Kulwa na Doto)
10. Dully Sykes
Ila Dully alijitoa siku chache kabla ya shindano!!
Shindano liliandaliwa na Global Publisher chini ya E. Shigongo na zawadi kwa mshindi wa kwanza lilikuwa gari, japo sikumbuki ni gari ya aina gani!!
Shindano lilifanyika usiku wa tarehe 27 June(siku ya ijumaa), na hatimaye Afande Sele kutawazwa kama mshindi na kuwa mfalme wa rhymes, huku ushindi wa pili ukienda kwa Inspector Haroun na ushindi wa 3 wakichukua akina Mandojo na Domokaya!
Ushindi huu ulipingwa na watu wengi kuanzia watu wa kawaida mpaka wasanii wenyewe!!
Haikupita muda Solo Thang aliandika wimbo akipinga kile kinachoitwa kupanga mshindi, namnukuu "wengine wananirubuni eti nashindania gari, kumbe washapanga wampe nani toka awali, sitarudia kosa hata zawadi waweke meli, wanipe ghorofa mbili wanikabidhi na sheli"
Solo Thang akuishia hapo, katika wimbo wa Traveller anasikika tena akisema "Mi siyo mfalme njozi mi siyo mgambo sele"
Fid Q naye katika Mwanza Mwanza aliendelea kuthibitisha kutokukubalika kwa ufalme wa Afande, namnukuu "Mfalme wa Rhymes ambaye Soggy Doggy hamtaki, anamwita Kobe hawezi mzidi mbio farasi"
Madee naye alienda mbali na kudai hajawai ona mfalme ana nywele chafu!!
Sasa ni takribani miaka 12 imepita toka Afande Sele atangazwe kuwa mfalme wa rhymes na hajapata mrithi wake, mwaka 2005 shindano alikufanyika baada ya washiriki kudai maslahi zaidi huku wengine wakipinga kunakoitwa kupangwa mshindi ambaye ilisemekana alitakiwa kuwa Fid q, ambaye alishajinadi kuwa ni mfalme atakayefuatia baada ya Selemani Msindi!!
Je Afande Sele alistahili ufalme wa Rhymes? Kama hakustahili nani alipaswa kupewa hilo taji?
Yaan walimuweka Inspector badala ya Ulamaa!???
Kweli walizingua.
mbona mgumu kuelewa hivyo, wimbo alioingia nao kwenye shindano ni darubini kali na sio mtazamo
We kweli ulikuwa bado kinda kipindi hicho!!!.
Solo hakuwa na ngoma kali!?.
Unaijua albamu yake ya HOMA YA DUNIA?.
Solo ndio alistahili ufalme wa ryhmes.
Ndio mtaalam wa vina kuwahi kutokea bongo.
"Bila shaka Solo thang nakubalika
Kama unabisha muuliza John kalamashaka
Hakuna utani hii fani mi nainyaka
Acha masihara
Mi kinara
Bongo kenya n'tang'ara
Sina papara
Ndio maana bora
Wenye vilemba vya ukoka wamedorora
Hili kombora
Msururu mrefu watanibeba na vingora....
Jay hakustahili hilo liko wazi kabisa, Solo Thang ni mkali sana ila kwa afande wa kipindi iko alikua kiboko.
Afande alistahili kuwa mkali wa rhymes.
Hivi bila mademu aliimba nani?
Bila mademu nani angepiga pamba,bila mademu nani angejiona bomba .... wale mliosomba shule za bweni haya mambo mliyaonaSio bila mademu.Ngoma iliitwa Ingekuwa vipi By mwana fa na Jaymo
Ninayo hiyo ngoma.. Ngoja nitakuchekia aliyeimba!!Bila mademu nani angepiga pamba,bila mademu nani angejiona bomba .... wale mliosomba shule za bweni haya mambo mliyaona
Poa mkuuNinayo hiyo ngoma.. Ngoja nitakuchekia aliyeimba!!
Kwani si wewe mwenyewe ndiye uliyesema kipindi hicho mashindano yanafanyika ulikuwa bado mtoto!?.Sasa dharau imetoka wapi?.Acha zarau ndugu.Sio kama nabeza uwezo wa Solotheng hapana,ila nasema kipindi cha mashindano hayo hakuwa na ngoma kali at that moment
Nasikiliza ngoma yake hapa HOMA YA DUNIA.Kwa upande wangu kura yangu ya turufu ilikuwa kwa Solo Thang Ulamar Mwanazuoni Aliyekomaa
Nashukuru umewasaidia vijana, walitaka tupigizane kelele tuJibu hilo hapo.View attachment 1111967
Mzee mwenzangu ww ndio huna kumbukumbu nzuri unataka kusema darubini kali imetoka baada ya shindano, hapo umekosea kabla ya shindano darubini kali ilikuwepo.Wewe hauna kumbukumbu nzuri labda.Afande sele baada ya kushinda akaachia ngoma yake ya Darubini kali ambayo ilifanya vizuri sana kwenye chat za bongo nadhani hapa ndo unajichanganya na kuzania ilitoka kabla ya mfalme wa rhymes.
Mtazamo ilikuwa kabla ya mashindano na ndo nyimbo aliyoingia na Sele.