Uchaguzi 2020 Nani mkweli kati ya hawa watu? Spika, NEC au CHADEMA?

Jambo ambalo naamini mimi ni CDM wamepeka majina maana Kama cdm wangekuwa hajapeleka majina na tunavyowaaminia makamanda (Halima & wenzie) wasingekubal kwenda bungeni LAKINI yanaweza kuwa hayajapelekwa na Mnyika
Kwa hiyo wakapeleka jina la ayeko mahabusu kwamba mamlaka ni ya Cdm sio au umejiondoa ufahamu?
 
Ukweli utaupata kwa nani wakati vyombo vyote vilivyotakiwa kuutoa huo ukweli vipo mfukoni mwa Serikali, na hiyo Serikali ndiyo chanzo cha huu uchafu wote?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ndio upuuzi nisio utaka. Kama kweli barua ilikuwa forged,mahakama ipewe taarifa,amru ya uchunguzi ifanyike. Mahakama ikipindisha tutajua.
 
Huu mjadala ni wa kitoto sana.

Wakati uchaguzi unaanza tulishuhudia wanachama wa CHADEMA wakilalamika kwa wakurugenzi wa uchaguzi kunyimwa fomu kwa kile kinachodaiwa kuwa wameshachukua fomu ya ubunge kwenye majimbo X. Hivyo wakurugenzi wa uchaguzi hawatoi fomu hiyo tena kwa wagombea wa CHADEMA.

Waliochukua fomu walidaiwa kuwa walifika kwenye ofisi za wakurugenzi wa uchaguzi wakiwa na barua za CHADEMA zilizogongwa mhuri wa katibu wao wa jimbo/mkoa.

Hili sakata liliwakumba wagombea kadhaa wa udiwani kupitia CHADEMA, siwakumbuki kwa majina nafikiri baadhi ya majimbo ni Ubungo na Kibamba.

Je kesi hizi ziliishaje? Wale wagombea feki walichukuliwa hatua gani ? Barua zenye mihuri ya CHADEMA walipewa na nani?

Mwishoni wagombea halali walipewa fomu kwa amri kutoka juu nafikiri. Ni NEC waliona mapungufu hayo nchi nzima au nani alitoa suluhisho sikumbuki.

Kilikuwa ni kituko kwa wakurugenzi kuwanyima fomu wagombea kwa kisingizio cha kuwa tayari mwanachama wao ameshachukua fomu tena kwa barua halali ya uteuzi kutoka kwenye chama chao wenyewe.

Sasa turudi kwenye hili. NEC wamepokea barua halali kutoka kwa Mnyika. Mnyika anasemaje? Kama anakataa, je alazimishwe kuwa aliandika? Kama barua ilikuwa feki kwa nini NEC isikubali yaishe na wakisikilize chama cha CHADEMA ili haki itendeke. Barua halali ya majina halali ipelekwe NEC. Kama CHADEMA hawataki kupeleka majina, je walazimishwe?

Kama wasipopeleka majina, Je sheria au Katiba inasemaje kuhusu hilo.

Imefikia kipindi kila chombo kifanye jukumu lake na kiache ubabaishaji. Nchi hii ina wasomi na ni aibu kuonekana kituko kwa mambo yanavyofanyika bila weledi.

Kuwa mzalendo ni pamoja na kusema ukweli sio kutetea ubabaishaji hata kama ni kwa manufaa yako.

Asalaam
 
Hapo hakuna hata mmoja aliye mkweli wote vyura wanapiga kelele vichwa nje kiwiliwili majini, wakisikia mchakacho wanazama majini
 
Pumba gani hizi unaweka hapa? Hapa substance ni barua kutoka Chadema kwenda ni original? Ndio inayompa kiburi Ndugai,we unaleta porojo za uchaguzi. Zinatusaidia nini kwa sasa?
 

Ni hivi, CHADEMA inataka wale Wabunge waendelee kuwepo bungeni, ndiyo maana wanaenda mahakani badala ya kumwandikia spika kwamba wameshawatema.

CHADEMA wanajaribu kuhadaa watu ili wasishukiwe kwamba wamebadili gia on air.

Kifuatacho mahakama itabariki kwamba Wabunge wale ni halali, na hapo mjadala utafungwa rasmi ili mihimili isipigane.
 
Ngoma inapelekwa mahakamani mbivu na mbichi zitajulikana.
 
Hivi hiyo ruzuku itakayo tokana na wabunge 19 itaenda wapi? Kina Mdee niajilini mie niwe nawapokelea nitawatunzia vizuri
 
Pumba gani hizi unaweka hapa? Hapa substance ni barua kutoka Chadema kwenda ni original? Ndio inayompa kiburi Ndugai,we unaleta porojo za uchaguzi. Zinatusaidia nini kwa sasa?
Soma uelewe sio unakurupuka tu.

Barua hiyo unajua nani aliiandika na nani kasaini? Kama ni Mnyika basi ni halali kama sio yeye basi sio halali. Kuhusu CC ya CHADEMA itamwajibisha kama kweli barua ni halali maana aliandika bila baraka kutoka CC.

Ila kama Mnyika hausiki basi NEC inaleta ubabaishaji. Kuhusu Ndungai yeye anasubiri tu taarifa kutoka NEC.

Wenye kutueleza ukweli ni Mnyika kwanza, akikana basi NEC watueleze ukweli.

Nimefanya reference ya uchaguzi kuonesha CHADEMA walivyochezewa rafu sasa pumba ipo wapi?
 
Maswali mengine ni kam kujaribu kuwasafishA hawA wendawazimu wazalendo uchwara. Spika na Nec hao wote ni mawakalA wa yule muovu shetani na ndiye anayewAtuma kufanya wayafanyayo.
 
Wachache wenye muda wa kutafakari kwa kina.NEC ,N DUGAI na DPP lao moja.Lengo "kutakatisha" fedha za mabeberu. Hoja kama hizo hazipatiwi majibu stahiki. Ni kukanusha kwa povu la kabudi bila uthibitisho. Inasikitisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…