Nani wa kumfungia kiongozi wetu Speed Governor? Nchi itapigwa mnada hii

Sawa mkuu china inaidai shingap USA, IMF na hiyo WB leta figure
 
Katiba pendekezwa ipunguze madaraka ya Rais
 
Kuna msemo wanasemaga, "wawekezaji watatengeneza ajira kwa vijana wetu"
 
Mkuu Rabbon usijidanganye. Nchi hii serikali haina pesa. Sababu moja kubwa ni hiyo uliyoandika kwenye sentensi yako ya pili. Hakuna makusanyo ya maana wala matumizi yenye weledi.

Halafu hilo pendekezo la kukopa na kununua meli kubwa za uvuvi ni kwa watu wenye mikakati ya dhati ya maendeleo kwa kutumia rasilimali kubwa walizojaliwa. Watu wenye akili kubwa na upeo mkubwa wa kufikiri.

Sio watu wanaochota hazina ya taifa kwenda kununua ndege eti kufufua shirika mfu bila business plan, vigezo muhimu wala kuzingatia taratibu makini za manunuzi. Wanaachia advantage yote kwa wauzaji na madalali wao! Halafu muda mwingi zina park, au kuwa matengenezoni, detention au wanazurura nazo nchini na duniani wenyewe. Na hakuna anayehoji wala kusumbuka na hilo.

Fahamu tu hii ni nchi ya kitu kidogo; nchi ya watu wadogo (courtesy of Eric Wainaina). Hakuna linalowezekana. Acha Wakorea waje na mimeli yao wavue kwenye deep sea yetu bila mikwaruzo. Hata bila mikataba wanaweza tu kama Wachina na Wathailand wanavyotuibia siku zote bila hata kujua.
 
Nimeona taarifa kuwa rate ya kulipa kwa mwaka imepanda
Na deni limeongezek kwa 15% tangu magu aende
Na gharama za maisha zinapandaga tu
Mara umeme
Pesa inashuka thamani kila siku
Dola adimu
Ajira hakuna

Seriously this is paining me
Tuache unafki na ushabiki wa kijinga penye ukweli tuuseme kiuzalendo zaidi
Na tufanye maamuzi kama watu wazima tunaomuogopa Mungu
Ccm 2025 inabidi itoke tu,, au ituletee kiongozi mwingine ambaye ni wa uhakika
 
Mara tunaletewa madawa ya kufunga uzazi, mara nchi imeuzwa ooh Wanyama wanabebwa

Hivi yote haya hayafanywi na wazawa ama
Tunajitoa ufahamu tu
 
Mkuu kama unafanya kwa ajili ya uchawa ni sawa lakini. Kama unafanya kutokana na ujinga then wewe sina cha kukusaidia.
Hayo maden USA anayalipa kwa dola au?
 
TISS! They need to do ''ze needful''
 
Mkuu kama unafanya kwa ajili ya uchawa ni sawa lakini. Kama unafanya kutokana na ujinga then wewe sina cha kukusaidia.
Hayo maden USA anayalipa kwa dola au?
Anayalipa Kwa makamasi Yako.Your ignorance is no more bearable ,naona unauliza maswali ya kijinga.
 
Kwa HOJA ulizotoa hapo juu,

Unakubaliana nami kuwa pesa zipo za kutosha, tatizo ni RUSHWA, zinaishia mifumo ya waizi.

Na Kwa kuwa hakuna Uzalendo kuhusu Nchi, watu hawajishughulishi kufikiri Kwa kina Kwa maslah ya nchi.
 
Kwa HOJA ulizotoa hapo juu,

Unakubaliana nami kuwa pesa zipo za kutosha, tatizo ni RUSHWA, zinaishia mifumo ya waizi.

Na Kwa kuwa hakuna Uzalendo kuhusu Nchi, watu hawajishughulishi kufikiri Kwa kina Kwa maslah ya nchi.
Tanzania hakuna Rushwa Kuna udokozi,kungekuwa na Rushwa Kwa extent mnayotaka kuaminisha watu , Nchi isingeweza kusukuma maelfu Kwa maelfu ya miradi.
 
Wewe acha janja janja........Hata kama kaeleza gazeti nzima speed ya ukopaji imepita maelezo.

Na kumbuka Prof Mkumbo in anyway ataandika uongo tu.
Kukopa walianza kukopa USA na Russia na wanaendelea kila uchao, huwezi kupiga hatua zozote kwa kujifungia ndani.

Hayati JPM alikejeliwa kwa kujifungia kwake humu humu Afrika, leo SSH anakejeliwa kwa kujichanganya kwake na dunia halisi!.

Matatizo yapo vichwani mwetu tu na sio kwingine kokote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…