Nani wanaoharibu nchi kati ya utawala wa CCM na vijana wanaodai haki na uwajibikaji?

Nani wanaoharibu nchi kati ya utawala wa CCM na vijana wanaodai haki na uwajibikaji?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Ni kujitoa ufahamu na kukosa akili viongozi wa CCM, watawala, BAKWATA na machawa wao wengine wengi kupayukapayuka kwamba vijana wanaharibu wanaharibu nchi na kufuata mkumbo tu kwa kurubuniwa katika harakati zao za kudai haki, kupinga dhuluma na kutaka uwajibikaji.

Wanaoharibu nchi hii ni CCM na utawala wake waliofunga njia na fursa zote za kushiriki siasa za maana katika nchi hii kwa wasio wana CCM, watoto wao, ndugu zao na machawa wao kwa kuharibu mifumo ya chaguzi zote kuanzia za wenyeviti wa kijiji, mitaa, udiwani, ubunge mpaka urais.

Wanaoharibu nchi hii ni waliopoka uhuru wa mahakama za nchi na kuzifanya ziendeshwe kwa maagizo ya watawala wa CCM na matamanio yao binafsi.

Wanaoharibu nchi ni wanaofanya ufisadi wa kila aina wa rasilimali za nchi ambazo zilipaswa kuwanafaisha raia wote.

Wanaoharibu nchi hii ni watekaji, wapotezaji na wauaji wa raia wenye mawazo tofauti yasiyopendwa na utawala wa CCM.

Wanaoharibu nchi ni wanaoutumia kete ya udini kutugawa pale ambapo raia wanapinga udhalimu, ukandamizaji na uonevu wa kila aina.

Wanaopinga haya maovu, ukandamizaji na udhalimu uliokithiri kamawe hawewaezi kuwa wanaharibu nchi, wamedanganywa au kurubuniwa. CCM iache kutudharau kwa kutuona bado ni wajinga wasio na maarifa au taarifa na mambo haya yatapingwa iwe kwa njia ndefu au fupi. Hakuna mtu mwenye akili atakayekaa kwa utulivu bila wasiwasi ikiwa hajui mustakabali wa kesho yake kutoka dola iliyojisimika bila ridhaa ya raia huku ikiwawinda raia wake wenyewe wenye mawazo mbadala mithili ya wananyamapori waharibifu.

Na utawala haramu hauwezi kuwafundisha raia njia sahihi za kudai haki zao.

Screenshot_20251205_104046_X.jpg
 
Back
Top Bottom