Naomba kuelezwa ni nani Mwingine zaidi ya Dkt Tulia na David Kafulila amewahi kurejesha Chenji Serikalini?

Naomba kuelezwa ni nani Mwingine zaidi ya Dkt Tulia na David Kafulila amewahi kurejesha Chenji Serikalini?

Siasa bwana. Yaani huyu kafulila mbona anapata sifa kiasi hiki sasa hivi. Kafulila si wajana wala juzi, lakini why sasa hivi ukiingia JF vichwa vya habari ni Kafulila tu??
Au ni yeue mwenyewe anamiliki account zaid ya kumi akijisifu ionekane ni watu wengine wanamsifu?
Sijakataa kumsifu mtu, lakini akisifiwa muda mfupi kabla ya uchaguzi tunapata na wasiwasi
Ulitaka ni wakati gani tuseme sifa zake na uzalendo wake kwa Taifa letu.
 
Bunge la mama mkimbiaji halina mzuka, linaboa, bunge la kudai waTanzania sorry watanganyika kudaiwa passports za kwenda Tanzania , sorry kwenda nchi ya Zanzibar, as a leader, how can you allow your subordinate kupayuka utumbo like that? Utawala wa wamama huwa unaboa sana!! Natamani uishe hata leo. Kazi bora ya wamama ni kulea watoto basi.

Hizi story za uzalendo sijui kurudisha chenji for me ni fiksi tu. Warudishe kwa nani? Sidhani yupo mtu kwenye lile genge anaweza hilo.

Kuna vitu haviingii akilini, bongo mzalendo mmoja tu Magu peke yake hakuna mwingine, nilivyokuelewa imebaki chenji B3 , wizi B mbili, inarudisha B moja na kuita waandishi wa habari kujisifu uzalendo my foot!!
Naona unapaniki sana bila saba zaidi ya wivu na chuki binafsi .
 
Huoni kuna watu watakopa ili awe Rais na akiwa Rais auze nchi?
.Mtu ataeweza kopesheka 1 tilion hawez kuwa na shda ndogo ndogo za pesa za mirad ya milioni 100
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna watu ni WAZALENDO kwelikweli,ni wasafi sana, ni waaminifu waliopitiliza,ni wacha Mungu na wenye Hofu ya Mungu sana na wana uchungu mkubwa Sana na Maisha ya watanzania. Miongoni mwa watu hao basi ni hawa watu wawili ambao wamewahi ishitua Tanzania na kugusa mioyo ya mamilioni ya watanzania.

Ngoja niwape story bila kuwachosha kuelekea wikendi. Ilikuwa hivi Mheshimiwa Chuma Mwenyewe David Kafulila akiwa katibu Tawala Mkoa wa Songwe alipewa Billion Sita kujenga mpaka kumaliza ujenzi wa Makao makuu ya mkoa wa Songwe yanayopatikana katika kata ya Mlowo Eneo la Nselewa. Lakini Chuma kwa kutumia mfumo wa Force Akaunti katika ujenzi wa Makao makuu hiyo hakumaliza pesa hiyo.

Ambapo mpaka jengo linamalizika na kukamilika Chuma Kafulila akabakisha Chenji ya Karibu Billion Mbili.Siku hiyo anasoma taarifa hiyo mbele ya waziri mkuu mwaka 2020 Ofisi za makao makuu ya mkoa ,watu wote walibaki Midomo wazo na kustaajabu Uzalendo alio uonyesha CHuma Kafulila. Nakumbuka siku hiyo alisoma taarifa hiyo kwa umakini na utulivu wa hali ya juu sana. Na kwa bahati nzuri mimi mwenyewe nilikuwepo siku hiyo na nilikuwa karibu sana eneo la Tukio na nilikuwa nimesimama jirani na Mheshimiwa David Silinde ambaye siku hiyo alipewa nafasi ya kuzungumza pia. Nilikuwa jirani maana nilikuwa ni kiongozi wakati huo kwenye jumuiya ya vijana yaani UVCCM.

Siku hiyo nakumbuka wakati tunarejea majumbani Chuma Kafulila alikuwa ni gumzo sana tena sana midomoni mwa watu ,kwa namna alivyo onyesha uzalendo wa kipekee na uaminifu wa kiwango cha juu sana.

Mwingine ni Dada wa Taifa na Rais wa IPU na msomi Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini.huyu sina sababu ya kueleza mengi maana mnakumbuka Billion kadhaa alizorejesha serikalini baada ya kubana matumizi kule Bungeni.

Nimeamua niandike haya kueleza kuwa kuna watu ni waaminifu na wazalendo sana,ambao miongoni mwao ni hawa niliowataja hapa.

Jiulizeni ndugu zangu watanzania ni mara ngapi mmesikia kuwa mradi fulani Umepelekewa mamillioni kwa mamillioni ya pesa, lakini pesa zimekwisha na mradi haujafika hata nusu na hela haieleweki iliko kwenda? Mara ngapi mmesikia miradi kama vile ujenzi wa shule au kituo cha afya au barabara au usambazaji wa maji unakatu umekwama kukamilika kwa kuwa tu mapesa yaliyotolewa yameliwa na kuisha kabla hata mradi haujafika hata Nusu yake? Hamjaona haya wanapofanya ziara mawaziri wetu huko mikoani wakisikitika mpaka wanatamani kulia baada ya kukuta pesa zimeliwa? Hamjaona waziri mkuu wetu akiongea kwa uchungu na kwa huzuni na kuagiza ukaguzi na uchunguzi ufanyike kubaini waliotafuna pesa?

Lakini vyuma hivi Mheshimiwa Dkt Tulia pamoja na David Kafulila vilirejesha Chenji ya mamilioni kwa mamilioni,pesa ambazo wangeamua kuzichepusha kutunisha akaunti zao benki. Lakini kwa uzalendo wao wakasema hapana acha turejeshe pesa hizi ili zikajenge vituo vya afya ,shule, usambazaji wa maji safi na salama,umeme, barabara n.k.

Mwisho niseme tu kuwa mimi ni mzalendo na nimekuwa na tabia ya kutetea na kuwasemea wazalendo wote. Mimi sioni haya wala aibu kumtetea na kumsemea mzalendo bure kabisa pasipo malipo ya aina yoyote ile wala kupewa hata mia tano tu ya Vocha. Nataka Taifa liwe na utamaduni wa kuwaunga mkono wazalendo na wachapakazi wa Taifa letu ,tusiache wakachafuliwa na kushambuliwa na wabaya .ndio maana kuna watu awali wakasema mara nalipwa kwa uchawa ,wengine wakasema nalipwa na Mheshimiwa Dkt Tulia,wengine wakasema Nalipwa na Mwamba Mwenyewe Paul Makonda na sasa wengine wanasema nalipwa na Chuma Kafulila.ila hawasemi nalipwa shilingi ngapi na kwanini nilipwe na kila mtu na na kwa watu wote hao? Na hawasemi kwamba wao wanalipwa na nani kuchafua watu humu jukwaani na mitandaoni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Sio kurudisha chenji Tu

Wengine walikuwa hawachukui ela kabisa

Leo nakutajia wawili Tu

Zito kabwe na January makamba
 
Sio kurudisha chenji Tu

Wengine walikuwa hawachukui ela kabisa

Leo nakutajia wawili Tu

Zito kabwe na January makamba
Sio rushwa kurudisha Fedha za miradi,
Zitto hajawahi kuwa Kiongozi wa Serikali hata hivyo
 
Nimeamua niandike haya kueleza kuwa kuna watu ni waaminifu na wazalendo sana,ambao miongoni mwao ni hawa niliowataja hapa.
Kurejesha fedha ni aidha mradi umejengwa chini ya kiwango au ameshindwa kutumia akili za kawaida kbs kuomba kubadilisha matumizi ya fedha hizo ili kutatua kero zingine lukuki ambazo ziko kwenye maeneo yao ya kazi!!!
 
Kurejesha fedha ni aidha mradi umejengwa chini ya kiwango au ameshindwa kutumia akili za kawaida kbs kuomba kubadilisha matumizi ya fedha hizo ili kutatua kero zingine lukuki ambazo ziko kwenye maeneo yao ya kazi!!!
Mradi ulijengwa katika viwango vinavyotakiwa na kukubalika. Huwezi pia ukajipangia matumizi yako kabla ya kufuatwa kwa utaratibu.maana lazima ufahamu kila kitu ni lazima kipitie utaratibu maalumu.
 
Back
Top Bottom