Naomba kufahamishwa kuhusu Afisa Doria Mtandaoni kwenye kesi ya Lissu

Naomba kufahamishwa kuhusu Afisa Doria Mtandaoni kwenye kesi ya Lissu

Leo nilipokuwa nafuatilia shauri la Bw Lissu kulikuwa na shahidi wa Upande wa Serikali alitoa ushahidi kuhusi shtaka la lissu la makosa ya mtandao.

Ningependa kujulishwa yule shahidi ni mtumishi wa Jeshi la Polisi, Mtumishi wa TCRA au ni mtu binafsi.

Halafu kozi yake ya miezi 2 kutoka kwenye hicho chuo cha unit upanga ilikuwa on job training au ndio kozi iliyomsaidia kupata hiyo kazi.
Natanguliza shukrani kwa atayenipa majibu sahihi.

Kusema kweli yule jamaa ushahidi wake sijauelewa kabisa nimebaki na maswali mengi kichwani
Hakuna shahidi pale, hii kesi ni ya kutengeneza na ndiyo maana haina mashiko ila serikali wamekomaa na habari za kizushi ili tu kumshikisha adabu Lissu. CCM ni wapuuzi sana.
 
uvivu na uoga wako ndio umakini wako gentleman 🐒
Kweli kabisa. Siku uoga wangu wa kuandamana ukitoka ndipo nitakapopata viongozi wasioamini kuwa Mimi ni mvivu.

Fursa zipo za kilaghai ila CCM mnaona watu ni wavivu!
 
Kweli kabisa. Siku uoga wangu wa kuandamana ukitoka ndipo nitakapopata viongozi wasioamini kuwa Mimi ni mvivu.

Fursa zipo za kilaghai ila CCM mnaona watu ni wavivu!
ardhi ya kilimo yenye rutuba iko bwerere nchi nzima hakuna haja ya kusingizia wengine gentleman 🐒
 
ardhi ya kilimo yenye rutuba iko bwerere nchi nzima hakuna haja ya kusingizia wengine gentleman 🐒
Mawazo ya kizamani ya CCM kudhani Kilimo ni kulima. Kila mtu anaweza kulima lakini siyo kila mtu anaweza kufanya Kilimo.

Tanzania tuna chuo Cha kilimo hatuna chuo cha kulima. CCM inadhani kulima ndiyo kilimo.

Halafu Kilimo siyo adhabu au dampo la kutupia watanzania wanaoshindwa kwingine. CCM mnadhani kila Ardhi iko kwa ajili ya Kilimo.
 
Back
Top Bottom