Naomba kufundishwa mbinu za kuepuka watu wa Jumuiya na Parokia

Maisha yetu yamejaa utoaji,utafanya kwa hiari au lazima ,usijidikie vibaya kutoa
 
Kabisa kwan kuzikwa ni nn kwamba mtu akisema mungu baba mrehemu ndio umeenda peponi au
Ndio uendelee na upagani wako kwa uhuru, na uwaachie wanaoamini vingine waendelee kuabudu kwa uhuru pia. Inashangaza mtu ni mpagani halafu anataka na wengine wawe kama yeye!
 
😂 katibu unakataa ukatibu wakati kuna watu wanajisifu hata kusoma neno pale mbele na wamewekeana zamu!, ila haka ka dunia katamu sana mi nimekapenda na nilichokipendea ni kitu kimoja waumini sio wachoyo!..😂
Nakumbuka ndoa yangu iliishia hapa ni miaka mitano (5 ) sasa.....
 
Miaka 50,60,70.. hata 100 mbona sio mbali 😀 siku ukifa mbona utapata majibu yote huko roho yako itakapoenda.
 
Bado narudi pale pale. Unatumia nguvu nyingi, hadi matusi, kulazimisha watu waamini ambacho wewe unaamini. Kwani tukitofautiana na kila mmoja akabaki na anachoamini, tatizo liko wapi?
Sawa baki na hivyoo sasa wacha sisi wapagani tuenjoy life
 
SDA mimi naona wanachosha kwenye yale mambo ya makambi na sunday school.. masharti ya kula kunywa si magumu sana
 
Kabla ya yote aliye na ID ya pengo amu-Quote hata kama nae anatumia I'd fake tumu quote aje hapa ajibu

Kwanini Wana watisha waumini eti usipotoa zaka mara sadaka na michango huzikwi ukipatwa na matatizo husaidiwi?

Kuna askofu alisusa kabisa kutoa kipaimara kisa tu watu wametoka michango kidogo wahusika walilia sana walikuwa wamejiandaa asee walilia mno lkn hakujari kama utani akaondoka!

Hili dhehebu Kwa Sasa lipo kibiashara live.

Kuna mwezi nilipiga hesabu ikaja
157,600/=

Sijui zawadi ya mototo yesu 10,000
Mshumaa wa xmaa5000
Mchango wa kununua msalaba mkubwa wa parokia then na wakigango35,000/=

Michango ya jumuiya,ujenzi pamoja na kumtegemeza katekista yote hapa iligota laki na uchafu

Hapa sadaka haipo Wala zaka!

Halafu katekista Unakuta kalewa vibaya
 
Ulinogewa na viporo? Maana SDA huwa hawapiki j.mosi. Au nyimbo zao zisizo na ala?
 
SDA mimi naona wanachosha kwenye yale mambo ya makambi na sunday school.. masharti ya kula kunywa si magumu sana

Kwanza SDA hawana sunday schools. Wao wanasali jumamosi

Pili Makambi sio lazima ile ni mikutano ya kidini tu wiki nzima. Hata wale SDA damu damu huwa hawaendi kila siku. Wanakuwa kazini siku zingine.

Pia Kula na kunywa sio sheria kusema unasimamiwa. Wanafundisha tu kuacha kula vyakula vyenye madhara kiafya. Maana kwao health lifestyle ni part ya mafundisho ya imani yao.
 
Ulinogewa na viporo? Maana SDA huwa hawapiki j.mosi. Au nyimbo zao zisizo na ala?

Wabongo wape kichwa cha habari. Stori watatengeneza wenyewe.

Binafsi nilisikia mengi sana kuhusu wasabato. Ila siku niliyoenda kusali kwao. Nikajua kwamba niliyoyasikia nje mengi sio ya kweli. Ni chumvi tu za watu.

Mfano wewe mtu mzima kabisa akili yako inaamini SDA huwa hawapiki jumamosi wala kuosha vyombo ?
 
Rafiki yangu hayati Shirima(RIP) wa Tandale alikuwa na duka kubwa kiasi hakuwa anashiriki jumui ndogo mtaani ila alituma michango yote,siku alipofariki hakuna kiongozi yoyote wa RC aliyekuja kwenye mazishi yake hadi walokole fulani walikuja kuokoa jahazi.
Bora usitoe mchango wowote jiunge na kanisa la Masanja Mkandamizaji au la Lovely Irene Uwoya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…