Naomba kufundishwa mbinu za kuepuka watu wa Jumuiya na Parokia

Hizi jumuiya zitakuja kufa kadri maisha yanavyosonga. Hata Ulaya a marekani zilikuwepo enzi hizo lakini sasa hivi hakuna anayezitaka maana wameona hazina maana na pia watu sanataka privacy sio kila mtu apajue nyumbani kwako kiundani.
 
Yule kijana aliyejinyonga kule Tanga akiwa ansomea upadre hakuzikwa na kanisa eti wala hakukuwa na ibada. Majirani na ndugu waliingiza mwili kaburini akazikwa. Yaani ni mambo ya ajabu sana, eti sheria zao haziruhusu.
 
Mtoa mada ameonesha ujasiri walau wa kuleta jf ila sio kuwaambia mubashara. Suala la michango makanisani imekuwa kero sana kwa watu wengi. Kama unasali na hujajipata usahau kufanikiwa kama kila mchango unatoa kama wanavyohamasisha. Kwenye hii Dunia unatakiwa utende wema, usiharibie mwenzako, kufanya kazi kwa bidii na kujilinda mwenyewe ukiomba Mungu akusaidie kwa hilo
 
Wachina hawamjui Yesu wala Mtume so MUNGU atawachoma wote au?
 
Kwa niaba ya wana jumuiya tumeshakujuwa, kumbe ndiyo maana Ulitaka kutugonga na Gari lako siku za nyuma tulipompitia mke wako. Fedha na Mali unazoringia na kututangaza huku jf siyo tabia nzuri kuna siku utatutafuta alafu tutakuwa bize na waumini wengine.
 
Maisha yetu yamejaa utoaji,utafanya kwa hiari au lazima ,usijidikie vibaya kutoa
Tutoe kwenye mrejesho wa kuonekana sio tunatishana Mungu Yesu alafu tunashibisha familia zao ila sisi tukikwama hatuna pa kukimbilia
 
Okoka uachane na mafarisayo na masadukayo.
 
Ulivyotaja tu magari 3 nimeacha kusoma.
 
Haujui ukichokiamini. Hapo umekwepa ukristo. Yesu alitufia msalabani ili tumtumikie. Ukishindwa kutumika kama huyo mtka mada maana yake umeukataa ukristo. Hapo siyo inshu ya SDA. Inshunninkuktumikia Mungu wapi na kwa namna gani hapo ndiyo kisanga ila si kusema hawana mambo mengi. Mungu ana mambo mengi ambayo anataka mtu ayafanye. Kalaghabaho.
 

Acha ujinga wewe. Hata Yesu mwenyewe hakuwa mkristo

Ukitaka kumtawala mtu mpe hofu kwanza. Nyinyi ndio wapuuzi mmejazwa hofu. Ili mtawaliwe na wajanja wenye makanisa yao.

Yesu sio Mungu hata wayahudi wenzake wanamkataa na kumuona tapeli tu.

Kwanza Kanisani tunaenda ku socialize tu sababu ni utamaduni tulioukuta kwa wazazi wetu. Ila tumeshajitambua tunajua dini ni utapeli tu
 
Soma tena paragraph zako mbili za mwisho. Wewe siyo Mkristo. Mkristo ni yule anayemfata Kristo. Wewe unafata wazazi. Ukristo siyo dini ni Imani na huna hiyo Imani. Tuachie tunaojua tunachokiamini. Pia, tangu leo fahamu msabato siyo mkristo.
 
Kizazi kinapotea, pita hapa na upige kura yako

 
Una hoja, japo wapuuzi watakushambulia.
 
ukiwa huna akili unaweza kutupa dhahabu na kuokota jiwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…