Naomba kufundishwa mbinu za kuepuka watu wa Jumuiya na Parokia

SDA mimi naona wanachosha kwenye yale mambo ya makambi na sunday school.. masharti ya kula kunywa si magumu sana
Hivi SDA ni kanisa la kihistoria kama lutheran na Roman Catholic au ni kanisa la ki-pentekoste yaani la kilokole?
 
Ukiweza kuwafanya waamini wewe ni Freemason umemaliza kazi.
 
Njia rahisi ni kuwakwepa kwepa kijanja hivyo hivyo. Ikitokea event yoyote unatengeneza excuse usijumuike nao ingawa usiache kwenda katika ibada. Mwishoe watachoka na kukupotezea. Kwetu sisi introverts ni kazi rahisi mno hiyo.
Yaan ni rahisi saana hata hupigizani kelele na mtu unachoamua ndo hicho hicho!!!
 
Njia rahisi ni kuwakwepa kwepa kijanja hivyo hivyo. Ikitokea event yoyote unatengeneza excuse usijumuike nao ingawa usiache kwenda katika ibada. Mwishoe watachoka na kukupotezea. Kwetu sisi introverts ni kazi rahisi mno hiyo.
Sidhani kama njia sahihi, siku ya siku utatengenezewa zengwe utaitwa mbele ya madhabahu kuwa unachaguliwa kuwa Fulani na hutaweza kuchomoa. Unadhani hao viongozi wa parokia na jumuiya huwa hawawasiliani na viongozi wakuu wa kabisa kuwa kuna mtu potential mahala. Utanasa Tu
 
Uliisha waonjesha asali. Ukitaka wasikutafute, usitoe chochote. Hata ukienda kanisani usitoe, wakileta bahasha usitoe, wakiandika barua usijibu, wakikualika jumuiya usiende, wakikualika harambee usiende na usichangie,wakija kwako usiwepo.
Watakuacha.
 
Uliisha waonjesha asali. Ukitaka wasikutafute, usitoe chochote. Hata ukienda kanisani usitoe, wakileta bahasha usitoe, wakiandika barua usijibu, wakikualika jumuiya usiende, wakikualika harambee usiende na usichangie,wakija kwako usiwepo.
Watakuacha.

Hakuna kanisa katoliki linalobembeleza imani ya mtu hivi ati kisa ana hela mtaani halipo. Huyu jamaa anawapiga fix. Bilionea Mrema alitengwa na kanisa sababu hakuwa mshiriki leo huyu kisa magari matatu ati parokia imng'ang'anie? Aseme ishu ni mke wake hana control naye, kwani akimkanya mke wake asimletee watu wa kanisa kwake na hataki mambo hizo si atatatua tatizo feki ambalo halipo.

 
Haya always huandikwa na wasio Wakatoliki,lakini tunaoelewa huwa tunawapuuza.

Hakuna kitu kama hicho ndani ya Kanisa na hatishwi mtu kila mtu na utashi wake wa kuamua anachoona kinamfaa
Jizuie kujilazimisha kupindisha uhalisia wa ile kweli kwa maana ni hakika kuwa yapo matamko yasemayo " usipotimiza ya Jumuiya na ikitokea ukapata tatizo au tukio (mf. ndoa, ubatizo, kifo etc) linalohitaji Msaada wa parokia; hutasaidiwa",.

Hali hiyo inafanana na ya Miaka ya 1,500 na ndio sababu ya kuundwa Kwa uprotestant, hivyo hata Sasa hii post in m'protestant wa yaliyomo Jumuiya.
 
Kwanza unajichanganya mwenyewe kwenye maelezo yako. Unakaataje Mungu hayupo bila uwepo wake? Huwezi kukataa uwepo WA kitu bila kitu kenyewe Ku exist first. St Anselm, alisema wapumbavu husema hakuna Mungu, wakati mawazoni mwao the concept God is already there.


Tuje kwenye jumuiya na ukatoliki, hakuna kanisa katoliki bila jumuiya. Jumuiya ndogondogo ndio msingi WA kanisa lenyewe rejea kitabu cha matendo ya mitume kwenye agano jipya, wakiristu WA mwanzo mitume WA Yesu na wafuasi Wao waliishi maisha ya jumuiya. Waliweka vitu pamoja na kugawana kadiri ya mahitaji. Kwasasa ndani ya kanisa katoliki jumuiya zinatusaidia kujuana, kusali pamoja na kusaidiana.

Umesema umebatizwa, umepokea komunyo na kipaimara na ndoa ndani ya kanisa katoliki lakini hujaelewa Imani ya kanisa katoliki. Kanisa katoliki linafundisha juu ya Imani na halilazimishi wala kutafuta waumini wabakie ni hiyari yako kama unaona kanisa katoliki si mahali pako nakushauri uondoke huna sababu ya kukwepa jumuiya.
 
Sawa kwa muktadha wa niliye-quote hapo juu yeye ameshayakataa hayo Kanisa linamlazimisha vipi kuyakubali wakati yeye ameshaikataa imani?

Hayo kwenye bold yanamuhusu muumini mwenye imani Catholic akishakuwa siyo Mkatoliki huna namna utamlazimisha mtu aamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…