Naomba kufundishwa mbinu za kuepuka watu wa Jumuiya na Parokia

Kama wanakuja kwako fuga midogi tu

Ova
 
Si wataniona najidai
Aisee umenishangaza kweli kweli. Eneo nililozawali mimi wakazi wake karibu wote ni wakatoliki. Kuna wazee wengi tu hawaendi kanisani na wala hawajishughulishi na mambo ya jumuia. Na kila mtu alishawajua. Hawakanyagi kanisani ng'o, hawatoi mchango wowote na wala hawashiriki kwenye lolote. Kwa kifupi wanaitwa wapagani. Sasa wewe kinakushinda nini? Dunia hii ukiogopa kufanya jambo eti binadamu wengine watafikiria vile... unaweza kujikuta unakwama kwenye mambo mengi.
 
Mnalazamisha na ndio maana asipoenda jumuiya hata kama anahudhuria Ibada kanisani mnaanza kumpa vitisho mara ooh ukifa padiri Haji kwenye maziko Yako, mara ooh kanisa linakutenga, basi kama vipi bomoeni makanisa ili tubaki na jumuiya tu.
Hivi serikali hawaoni haja ya kuweka sheria ya kuchoma moto miili. Maana kuna watu dini unatishiwa hautazikwa as if huo mwili una umuhimu tena duniani.Kwanini pasiwepo na kuchoma miili moto ili tusave muda na nafasi?
 
Jana wametangaza upanuzi wa kanisa unahitaji bajeti ya 700M ambayo naona ni nyingi. Parokia yetu ni changa haijatabarukiwa (kuwekwa wakfu), ila nikipiga hesabu naona tangu parokia inaanzishwa nikiwa A level huwa watu wanachangishwa tu. Mapato ya kanisa kwa mwaka ni around 100M, naona dalili ya kukamuliwa hela inakuja ingawa siishi tena uko.

Nakumbuka tulianza vijana wengi ila sasa tumepungua, naamini na watu wazima wamepungua.
Huwa ni changamoto kujenga kanisa au kulifanyia maboresho watu wenye roho nyepesi hukimbia.

Vitu sipendi ni kupotezewa muda mara vijana jogging, misa na askofu, matembezi ya nini sijui, beach mass.

Kanisa nilitaka nilitupe ila nikajiuliza nikitaka kuoa mke anayesali na asiyesali naoa nani, anayesali. Watoto wangu watakuwa wanasali au atheists, bora wasali. Nikabaki
 
Hata Ushoga ulianza na hoja kama hizi hizi, mwishowe unaanza kuenea kwa Kasi. Hili nalo ni eneo lingine la wanaompinga Mungu linavyoanza.

Hamia Freemason, wanamuabudu Shetani na pesa za kula Bata wanapata.
Usiwe na akili finyu kiasi hiki, jibu hoja kwa hoja. Mtu kauliza swali ww unaanza kuleta mambo ya ushoga yanahusiana nn hapa?
 
Hujanielewa wife ndiye ananirudisha nyuma kwa sababu anawaomba msaada kuwa mimi nimeingiliwa na shetani so wanakuwa na matumaini na mimi
 
Sasa hapo unaanza kufunguka! Believe me or not I don't care! Hizi dini zoote kwa majina yake nyuma yake hiko roho inayokamata fahamu na kuamini unamtumikia Mungu lakini kiundani unatumikia taasisi za kinyonyaji za kibepari na kibwenyenye zilizojenga mtandao na kufungamana na nguvu za giza! Kama wewe ni wa hiyo dini kama ulivyosema na hiyo dini ndo iliyokufungisha ndoa umefungamana na madhabahu ya hiyo dini na hiyo roho ukitaka kuihasi lazima uhadhibiwe na mwisho watasema "unaona? Mungu kaanza kumpiga"! Broh! Kuna njia moja tu ya kukimbia dini nayo kuokoka! Just you and your faith in Jesus Christ! You don't even need to go to divinity churches! Unaweza kuvuta nguvu za Mungu ukiomba na kusikiliza mafundisho sahihi na kusimama kivyako na ukatoboa bila kutishwa na kupigwa na maroho ya mashetani yaliyomo kwenye dini! Maroho ya dini yana nguvu kuliko wachawi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…