Naomba kujua kuhusu matibabu ya macho na gharama zake

Desierto

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
901
Reaction score
3,112
Mke wangu ana matatizo ya mcho ya kuona mbali aliwahi kuugua macho akapona kama miaka 8 imepita.

Sasa nimejaribu kufatilia kidogo nikasikia kitu kinaitwa mtoto wa jicho na matibabu yake ni kubadilishiwa lensi tu.

Basi shida yangu nataka kujua makadirio ya matibabu yanaweza kufikia kiasi gani. Ili nijipange hata kwa mwaka mzima.

Pia vipi kuhusu bima nikijiunga inaweza kunisaidia kupunguza gharama?

Asanteni nasubiria ushauri wenu.
 
Mtoto wa jicho (cataract) gharama zake hata laki mbili hazifiki kwa macho mawili. Ni operation ndogo sana hiyo mgonjwa na ni outpatient (mnarudi kulala nyumbank).

Swali; Kama alikuwa haoni mbali (myopia), mlitumia matibabu gani? Miwani au operesheni?
Maana mtu ambaye haoni mbali, huwa mara nyingi anapata cataract (mtoto wa jicho), kama asipovaa miwani ya kurekebisha lenzi.

Ushauri; hata akifanyiwa operesheni ya mtoto wa jicho asiache kuvaa miwani. Miwani ni dawa kwa myopia na ni kinga ya mtoto wa jicho pia.
 
Hajawahi kutumia miwani mkuu na hapendi anasema inamuumiza hajazoea
 
Aliponaje kutokuona mbali? Alifanyiwa operesheni?
Hakupewa lenzi sahahi; hakuna mtu anaumia na miwani kwa kupewa lenzi sahihi mkuu.
Mpeleke hospitali kama Aga Khan, CCBRT au Muhimbili akafanyiwe utaalamu zaidi mkuu.
Wahi chapu jamaa yangu.
 
Nenda Medwell hospital ipo mpakani kibaha kwa shilingi 10,000 au 15,000 utapata tiba.
 
Mtoto wa jicho (cataract) gharama zake hata laki mbili hazifiki kwa macho mawili. Ni operation ndogo sana hiyo mgonjwa na ni outpatient (mnarudi kulala nyumbank).

Swali; Kama alikuwa haoni mbali (myopia), mlitumia matibabu gani? Miwani au operesheni?
Maana mtu ambaye haoni mbali, huwa mara nyingi anapata cataract (mtoto wa jicho), kama asipovaa miwani ya kurekebisha lenzi.

Ushauri; hata akifanyiwa operesheni ya mtoto wa jicho asiache kuvaa miwani. Miwani ni dawa kwa myopia na ni kinga ya mtoto wa jicho pia.
Kwani kuna operation ya myopia? Mimi sioni mbali na natumia miwani. Lakini bado kuona mbali kama mwenye macho ya kawaida tatizo. Natumia lensi -5 wanasema nikaongeze lensi, ni kweli? Haitasababisha shida zaidi?
 
Operation ya myopia ipo, unawekewa artificial lens. The best option ni miwani au contact lens, sababu operations zina risk zake. Kama bado lens zako zinaweza tibika (corrected) kwa miwani, miwani ni bora zaidi.

Kuhusu ishu yako: Sio mbaya kuongeza miwani, ukitoa miwani bado unaonana blurred?
Maana inatakiwa uwe una boreka uoni kutokana na miwani husika.
 
So kuongeza lensi haina madhara?
 
So kuongeza lensi haina madhara?

Haina madhara yeyote mkuu. Lensi kazi yake ni kufanya mwanga ufike/ugonge nyuma ya duara la jicho/eyeball ili wewe uone vizuri. Kinachotokea hapo ni kwamba uoni wako haijaimarika, unahitaji lenzi ya juu. Ukiimalika utapunguziwa lenzi au ukitoa miwani ile blurry itapungua.
 
Kwanza ingekuwa mtoto wa jicho hata wewe ungeiona maana siyo kitu cha kujificha na ndio inahitaji surgery. Kutokuona mbali tiba ni miwani tu . Aende apime macho ,lens anachagua mwenyewe inayomfanya aone comfortable .Atajaribu lens tofauti tofauti hadi ile itayomfaa . CCBRT kupima pamoja na miwani si chini ya laki mbili. Achana na mambo ya surgery labda kama anasumbuliwa na suala zito kama pressure ya macho. Mtoto wa jicho ni doa jeupe kwenye mboni ya jicho
JICHO.jpg
 
Back
Top Bottom