Naomba kujua mgogoro wa Ngorongoro maana mbuga ni muhimu haiwezi kuhamishwa Ila ndugu zetu nao muhimu pia

Kwa hiyo unashauri mbuga ya Ngongoro ifutwe ibaki kuwa Eneo la masai kuchungia sio ???
Kama Wanzanzibar wote wanaweza kuhamishwa na Zanzibari Kufutwa kwa nini isiwezekane kwa Ngorongoro na wamasai? Wote si ni binadamu!
 
Ardhi Tanzania ni mali ya umma na mamlaka ya kumirikisha matumizi yake yako kwa Rais wa nchi. Kwa msingi huo, bado haki ya kila mwananchi kumiliki
Ili tuweze kujadili kinachoendelea huko Ngorongoro, ni muhimu kujua umiliki wa ardhi kisheria Tanzania.

Ardhi ni sehemu yote iliyo juu na chini ya uso wa nchi, vitu
vyote vyenye kuota kiasili juu ya nchi, majengo na miundo
mingineyo iliyokaziwa kwa kudumu juu ya ardhi

Ifuatayo ni baadhi ya misingi halisi ya ardhi kama
ilivyoainishwa kwenye mwongozo wa ardhi wa kitaifa (sera) na kutafsiriwa na sheria mbalimbali za nchi:
i. Ardhi yote ni mali ya umma na imekabidhiwa kwa Raisi kama mdhamini (msimamizi) mkuu kwa niaba ya watanzania wote;
ii. Kulinda haki zote za miliki za ardhi zilizopo, yaani miliki ya ardhi ya kimila na ile ya kiserikali;
iii. Kugawa ardhi kwa haki na kwa raia wote wa Tanzania;
iv. Kudhibiti kiasi ambacho mtu mmoja au taasisi yaweza kumiliki na kutumia kwa mahitaji yake bila kuwaathiri
Watanzania au wanajamii wengine;
v. Kuwezesha utumiaji endelevu wa ardhi katika shughuli za kiuzalishaji kwa manufaa ya wote;
vi. Kuhakikisha kwamba maslahi yeyote katika ardhi yana thamani na yanalindwa katika muda wowote wakati wa mapatano yanayoweza kuathiri thamani ya mmiliki;
vii. Kulipa fidia kamili na kwa wakati kwa mtu yeyote ambaye haki miliki ya ardhi yake inafutwa, inabadilishwa au inaingiliwa kwa namna yeyote na serikali kwa manufaa ya umma na yeye kuathirika na zoezi hilo; nk

Swali, Je, misingi hiyo imezingatiwa?
 
Ahasante mkuu kwa kuchangia kisomi kabisa
 
kabisa, magufuli aliwahamisha wasukuma na waha katika pori tengefu la kazirankanda, tena akawachomea moto na manyumba, leo pori la kazirankanda lina zimba pori tena walionawiri na twiga nyati na uoto wa asili wenye kupendeza.

magufuli aliwahamisha wapimbwe na kuanzisha hifadhi ya katavi kuna pori tengefu la inyonga yupo mwekezaje mahiri africab, leo bohora kila mwaka lazima aje na wageni wake zaidi ya miasita kupumzika wote huo ni uchumi,

kule bunda eneo la nyatwali mazungumzo yako hatua za mwisho wanakijiji kuhamishwa kupisha njia ya tembo kwenda kunywa maji ziwani wakati wa kiangazi, kule mugumu wanakijiji wanapisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa kwa ajili ya matajiri kuteremkia, sasa shida iko wapi wamasai kupisha eneo dogo tu kwa shughuli za utalii, au wanaona faraja kikimbizana na fisi tembo na mbweha, au kwao sifa kuonesha mbupu zao kwa watalii,
 
Jibu hoja mkuu
Tuwaache wamasai waharibu mbuga au tuilinde mbuga ya ngongoro

..maelfu ya magari ya watalii yanaharibu mbuga kuliko Wamaasai na ng'ombe wao.

..ujenzi wa mahoteli, na makambi ya kulala watalii, ndani ya hifadhi, unaharibu mazingira ktk mbuga zetu.

..busara itumike kuweka mzani sahihi kati ya mazingira, Wamaasai, na shughuli za kitalii.
 
watalii wanalipa ushuru tunapata pesa ya kuendesha nchi 87% ya fedha za kigeni zinatokana na utalii, hao wamasai wanaindiza dola ngapi kwa mwaka kwenye uchumi wetu, kama wamasai wana umuhimu wa kukaa serengeti ngorongoro tufute hifadhi hizo wamasai wagawane mashamba halafu mtuambie hii 87% tutaipata wapi
 
[emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
nyerere aliwasikiliza wazee wa tanu akafuta mashamba ya Lobo Galanose Mackenzie Lonhro, leo tunaagiza ngano shairi maziwa ya nido khanga, mafuta ya kupikia sukari, sasa tunataka kuua hifadhi ya serengeti ngorongoro kisa siasa za kipuuzi
 

..kunatakiwa kuwe na BALANCE sahihi kati ya mazingira, utalii, na Wamaasai ambao eneo la Ngorongoro ni makazi yao ya asili.

..sio kweli kwa asilimia 100 kwamba shughuli za Wamaasai zinaharibu mazingira ya Ngorongoro.

..Wamaasai wamekuwepo Ngorongoro vizazi na vizazi ni mbuga hiyo bado ipo. Tusiwachukulie kama maadui, bali wadau na wahifadhi wa Ngorongoro.

..kila upande ujishushe. Tufanye maamuzi yatakayoridhisha pande zote. Tusitumie mabavu.
 
Wamaasai wamebaki baaada ya kusimama kidete, anzisha uzi mwingine wa kujiliza.
 
Hivi wale N'gombe na mbuzi wawamasai na midege inayotua na mishughuli mizito inayoendelea na nani anahatarisha wanyama na uoto wa asili wa mbuga ya ngorongoro au ndio walewale tuu nafikiri uelewi tembelea siku moja kabla ya kujadili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…