Kukaa kimya ni ishara ya utulivu, busara na Hekima na ni hekima kubwa sana.
Kuna hekima kubwa mbili huwa naziomba na ninawaombea viongozi Kwa Mungu wetu:
Ya kwanza, ninaomba na kuwaonbea kukaa kimya hata pale wanaweza kujibu. Jibu la kukaa kimya ni bora kuliko la kunena. Hata kwenye Biblia ,Yesu alipopelekwa mbele ya Pilato alikaa kimya bila kuzungumza wala kujibu lolote na mpaka Pilato akaona hana hatia yoyote.
Kukaa kimya kwa Rais Samia ni hekima ya kiuongozi na kiongozi bora anatakiwa kujua ni lini na wapi akae kimya. Pale unaposhtakiwa, unapotuhumiwa, unqposingiziwa na unajua dhamira yako ni njema na safi ni hekima ya juu KUKAA KIMYA MTETEZI WAKO NI MUNGU.
Ya pili, naomba na kuwaombea kutofanya hata pale unapoweza kufanya. Mamlaka zote zimetoka Kwa Bwana hivyo kiongozi anatakiwa kuwa na Hekima na Kiungu kuongoza na sio muda wote ni wa kufanya.
Kama una mamlaka haimaanishi kutokufanya ni udhaifu. Kwenye Biblia tunaona Yesu alifatwa na askari wenye marungu na silaha kumkamata lakini katika kumkamata ikataka kutokea kama mapambano na Yeye akauliza ,je mnadhani nashindwa kumwambia Baba yangu aniletee majeshi 12 ya malaika?
Uwezo wa kushusha majeshi ya malaika anao na mamlaka anayo lakini haimaanishi kutowashusha ni udhaifu ila ni hekima ya kutokufanya hata pale unapoweza kufanya kaitumia.
Hivyo basi haimaanishi kukaa kimya Kwa Rais Samia ni udhaifu au ana hatia hapana ni hekima aliyonayo kama kiongozi. Sio Kila suala ni la kujibu Kwa sababu washtaki wako hawataridhika au hawatarishishwa na majibu yako