Ndugai anajua nguvu ya rais kikatiba, ànajua rais ana uwezo wa kumpoteza. Akaamua kuondoka kwa amani kawaachia wana harakati ila kaonesha njia.
Nguvu ya rais ya kikatiba ipi ingeweza kumpoteza Ndugai?
Unaweza kutaja kifungu ili tukichambue?
Ndugai kaonesha njia ipi? Ya kuufyata mkia?
Ndugai ni mtu mmoja mjinga ambaye kaupata Uspika kwa bahati, na kwa sababu walimuona mjinga watam control. Ndiyo maana kashindwa hata kuwa strategic kujua nini aseme wapi, lini, kwa mkakati gani. Akaishia kujiuzulu kijinga.
Matatizo yenu Watanzania wengi hamjui kufikiri bila kulinganisha watu. Hamjui kufanya abstract thinking.Hapa mshajipanga team Ndugai vs team Samia.
This is a false dichotomy.
Mshasahau Ndugai na Samia na Magufuli wote wamefanya ushenzi nchi hii.
Hamjui kusimamia principle.
Kwa taarifa yako, rais hana uwezo wa kumuondoa Spika kikatiba.
Hivyo, Ndugai kama kweli aliona nchi inauzwa alikuwa nanuwezo wa kukomaa kwenye hilo.
Tatizo Ndugai issue yake haikuwa nchi kuuzwa, issue yake ilikuwa tofauti akaropoka issue ya nchi kuuzwa. Akajiuzulu.
Haya ni mambo ya power struggles za Sukuma Gang na Samia, Watanzania mnadanganywa nchi inauzwa.
Kwani Magufuli alivyoua upinzani wazi na kumwambia Ndugaye awadhibiti wapunzani bungeni, yeye Magufuli atawadhibiti nje, Ndugai alikuwa msafi sana?
Ndugai hakushiriki kupitisha sheria kandamizi za Magufuli bungeni?
Why all of a sudden kisentensi kimoja cha Ndugai ndiyo kimfanye awe shujaa, tena kwa kujiuzulu.
Kujiuzulu kwa Ndugai na watu wanavyomshabikia ni kielelezo cha kwa nini Watanzania ni masikini.