Nani kakwambia alitishiwa maisha?Angefanyaje sasa kama pengine alitishiwa maisha
Kwa kilichotokea,ungekuwa wewe ungeweza kuendelea?Nani kakwambia alitishiwa maisha?
Mbona unaleta speculations?
Na kama una woga kwenye nchi tata kama Tanzania kwa nini unagombea Uspika in the first place?
Nini kilitokea kwa mujibu wako?Kwa kilichotokea,ungekuwa wewe ungeweza kuendelea?
Katiba Haina tatizo, hajuteuliwa kuwa VP na katiba. Hata chadema walimteua Salum Mwalimu kuwa mgombea mwenza!Hilo ni katiba ndo imeliweka
Ndugai anajua nguvu ya rais kikatiba, ànajua rais ana uwezo wa kumpoteza. Akaamua kuondoka kwa amani kawaachia wana harakati ila kaonesha njia.Nini kilitokea kwa mujibu wako?
Kilichotokea for sure ni Ndugai kuji contradict.
Kasema nchi inauzwa, nchi aliyoapa kuilinda, halafu kajiuzulu. Bila kuilinda. Kamuachia kiti cha Uspika Tulia, kuwadi wa kuuza nchi.
Sasa hapo huoni kwamba Ndugai ni sehemu ya tatizo, si sehemu ya kuondoa tatizo?
Ningemuona Ndugai wa maana sana kama angeitetea point yake mpaka afukuzwe, sio ajiuzulu mwenyewe kama mbwa koko. Tuone kabisa kapigana mpaka mwisho, kashindwa kwa kufukuzwa. Nani kamfukuza, kwa kanuni gani, tumbane huyo aliyemfukuza. Kwa nini unamfukuza Spika anayetetea nchi, anayetaka nchi isiuzwe?
Mimi nikiamua kusimamia kitu ninachoona ni sawa siwezi kujiuzulu. Kama kuna ukweli kwenye hoja ya nchi kuuzwa, ningeisimamia mpaka nifukuzwe kwenye chama au nipigiwe kura ya kuondolewa Uspika. Au niwaondoe hao wanaouza nchi.
Ndugai angeondolewa hivyo, hapo labda mngekuwa na point ya kumsherehekea kama mtu wa maana.
Sasa nyinyi mnamsherehekea mtu aliyeshindwa kutetea nchi isiuzwe licha ya kupewa manyota ya Uspika?
Watu wanagombea nafasi kubwa kwa kupenda vyeo tu, ikiwa wanatakiwa wafanye kazi ya kikubwa wanajiuzulu?
Hivi hamuoni kuwa Ndugai alikuwa anacheza mchezo wa siasa tu, na kama issue kweli ni kuuza nchi, yeye mwenyewe na Magufuli walishaanza kuharibu misingi ya kuifanya nchi isiuzwe siku nyingi tu?
Ndugai ni mtu wa kusifiwa kweli? Kwa kauli ya nchi inauzwa tu? Na kujiuzulu?
Are you serious?
Ni sawa na kubambwa live ukimtafuna beki tatu. Lazima uwe mpole tu.Hoja nzito kama zile anaanzaje kuthubutu kufungua kinywa?
Nguvu ya rais ya kikatiba ipi ingeweza kumpoteza Ndugai?Ndugai anajua nguvu ya rais kikatiba, ànajua rais ana uwezo wa kumpoteza. Akaamua kuondoka kwa amani kawaachia wana harakati ila kaonesha njia.
Ana agenda yake ambayo sio nzuri...angekuwa clean angeshakemea mara moja...lkn kwakuwa kachafuka hana namna zaidi ya kukaa kimya kusubiria upepo utaenda vpHalafu eti wapumbavu wanamsifia kwa ukimya.
Nyumba inaungua moto halafu unamsifia mwenye nyumba kwa ukinya?
Acha UjingaKukaa kimya ni ishara ya utulivu, busara na Hekima na ni hekima kubwa sana.
Kuna hekima kubwa mbili huwa naziomba na ninawaombea viongozi Kwa Mungu wetu:
Ya kwanza, ninaomba na kuwaonbea kukaa kimya hata pale wanaweza kujibu. Jibu la kukaa kimya ni bora kuliko la kunena. Hata kwenye Biblia ,Yesu alipopelekwa mbele ya Pilato alikaa kimya bila kuzungumza wala kujibu lolote na mpaka Pilato akaona hana hatia yoyote.
Kukaa kimya kwa Rais Samia ni hekima ya kiuongozi na kiongozi bora anatakiwa kujua ni lini na wapi akae kimya. Pale unaposhtakiwa, unapotuhumiwa, unqposingiziwa na unajua dhamira yako ni njema na safi ni hekima ya juu KUKAA KIMYA MTETEZI WAKO NI MUNGU.
Ya pili, naomba na kuwaombea kutofanya hata pale unapoweza kufanya. Mamlaka zote zimetoka Kwa Bwana hivyo kiongozi anatakiwa kuwa na Hekima na Kiungu kuongoza na sio muda wote ni wa kufanya.
Kama una mamlaka haimaanishi kutokufanya ni udhaifu. Kwenye Biblia tunaona Yesu alifatwa na askari wenye marungu na silaha kumkamata lakini katika kumkamata ikataka kutokea kama mapambano na Yeye akauliza ,je mnadhani nashindwa kumwambia Baba yangu aniletee majeshi 12 ya malaika?
Uwezo wa kushusha majeshi ya malaika anao na mamlaka anayo lakini haimaanishi kutowashusha ni udhaifu ila ni hekima ya kutokufanya hata pale unapoweza kufanya kaitumia.
Hivyo basi haimaanishi kukaa kimya Kwa Rais Samia ni udhaifu au ana hatia hapana ni hekima aliyonayo kama kiongozi. Sio Kila suala ni la kujibu Kwa sababu washtaki wako hawataridhika au hawatarishishwa na majibu yako
Ningekuwa me ndo Mkuu wa majeshi I swear to God Ningekuwa nimeshampindua Bimkubwa.Kiongozi makini huwezi kukaa kimya ilhali unashuhudia nchi yako ikiporomoshwa na kugawanyika kwenye jambo ambalo umelianzisha wewe!
Maana ya uongozi ni kuliongoza taifa katika hali zote.
Na nyakati kama hizi ndio haswa unapotakiwa kuonyesha upeo wako.
Ina maana hata tukiingia vitani kwa kuvamiwa kijeshi.
Rais ataendelea kukaa kimya?
Sasa hapo anafanya Busara kwa manufaa ya nani?
Nchi inaelekea kugawanyishwa huku yeye akiendelea kuhudhuria makongamano na warsha kila uchao!
Kwenye hilo nakupinga live...
Uraisi ni taasisi na siyo suala la mtu binafsi.
Tukome kuweka makopo madarakani
Mzee mbona umetoa kauli Kali Dana[emoji2]Watoto wako wameshafanyiwa utaratibu wa chakula mkuu?!! Maana jioni hii, punde tu itakuwa usiku.