Wanabodi!
Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.
Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa
Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.
Conclusion
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, hili pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa mmefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye serikali moja?
Wasalaam,
Paskali.