Naomba kujulishwa taratibu za kubadili uraia kutoka kuwa mtanzania bara na kuwa mzanzibari

Naomba kujulishwa taratibu za kubadili uraia kutoka kuwa mtanzania bara na kuwa mzanzibari

Hapana, uraia ndio kitu kikubwa kuliko ukaazi, naendelea kusisitiza, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT, kwa maoni yangu, kuiita nchi yako kuwa ni nchi ya kusadikika ni upungufu wa uzalendo.
P
Pia wana Rais wa Zanzibar anayechaguliwa kikatiba na pia wana Spika wa Bunge lao na Jaji mkuu wa Zanzibar.
 
Wakuu naomba kwa yeyote anayejua anisaidie namna ya kuhama kutoka kuwa mtanzania wa Tanzania bara na kuwa mtanzania wa Zanzibar yaani kuwa mzanzibari

Nataka kuwa mzanzibari wa kuhamia ili niwe na haki ya kumiliki ardhi kule na Tanzania bara pia, kugombea uongozi kule na nafasi za Muungano kama utais lakini pia niweze kugombea ubunge kule ili niweze kuteuliwa kuwa waziri katika wizara za muungano na zisizo za muungano kama ilivyo kwa Makame Mbarawa anayeongoza wizara isiyo ya muungano ambayo ni ya Tanzania bara lakini kwa mtu kutoka Tanzania bara hawezi kuteuliwa kuongoza wizara Zanzibar.
Nikiwa mzanzibari naweza kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya Zanzibar au Tanzania bara kama ilivyo kwa Shaka ambaye ni DC huku Tanzania bara lakini hakuna mtanzania bara anayeweza kuwa Sheha, DC au RC kule Zanzibar.

Nataka kuwa mzanzibari kwakuwa wazanzibari wanajitambua sana linapokuja suala la nchi yao na uraia wao tofauti na watanganyika waoga hawataki kuwepo kwa Tanganyika yao utadhani ikiwepo watakufa wote. Ni watu waoga sana na hawaipendi asili na nchi yao kama wazanzibari. Naombeni meongozo wa kuachana na Tanganyika nimechoka kuionea aibu nchi yangu bora nihame kabisa. Kumbukeni KILA MZANZIBARI NI MTANZANIA LAKINI SI KILA MTANZANIA NI MZANZIBARI. Naombeni wazanzibari mnipoker nije kushirikiana nanyi kuipigania Zanzibar
Mkuu umetisha hahaha.. 😂😂😂
Naona umetoa ya uvunguni mwa moyo...😂
 
, Zanzibar sio nchi
Mnachanganya sana watu, sijui kwa faida ya nani?

Kuna mahali popote ndani ya sheria za JMT inayosema "Zanzibar siyo nchi"?
Lakini maandishi yapo chungu nzima tokea huko ndani ya "nchi ya Zanzibar" yanayo itambulisha kuwa ni nchi, na sheria zinazo ainisha mipaka ya nchi hiyo; na wakazi wa nchi hiyo wanaotambuliwa kuwa "WaZanzibari"; akiwemo na rais wa JMT!

Imebaki tu siku moja kumpata shujaa, mZanzibar shujaa ajitokeze mbele na kukana huo uTanzania unaolazimishwa watu wa nchi hiyo wawe nao.
Shujaa huyo atamke wazi hadharani kwamba yeye hautambui uTanzania, anaolazimishwa awe nao bila ya ridhaa yake.
 
Hapana, uraia ndio kitu kikubwa kuliko ukaazi, naendelea kusisitiza, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT, kwa maoni yangu, kuiita nchi yako kuwa ni nchi ya kusadikika ni upungufu wa uzalendo.
P
Mkuu 'Paskali' usifikiri hueleweki kwa hivyo vikaratasi vya uTanzania; kama vilivyo vile vya Katiba yenyewe.

We exist in ambiguity, and as long as maslahi hayaguswi, hayo mengine potezea tu. Hakuna mjinga atakayehoji chochote.
 
Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye uraia mmoja tuu, Zanzibar sio nchi, bali ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani na utambulisho wake wa ndani uitwao ukaazi, sio uraia, ni utambulisho tuu!.
P
Kaka Pascal utahojiwa tena... This time Zanzibar ni nchi au siyo nchi
 
Mnachanganya sana watu, sijui kwa faida ya nani?

Kuna mahali popote ndani ya sheria za JMT inayosema "Zanzibar siyo nchi"?
Tanzania ni nchi moja tuu ya JMT, yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani. Hivyo ndivyo isemavyo katiba ya JMT.

Katiba ya Zanzibar inayoitambulisha Zanzibar kama nchi, haitambuliki na katiba ya JMT, hivyo haituhusu, wala haiihusu JMT!.

Kwa vile Zanzibar iko huru kwenye mambo yake ya ndani, rukhsa kujiita vyovyote, as long as mwisho Chumbe, tusiwaingilie.
Hili jambo tumelizungumza sana humu, mimi hadi nimeliandikia makala Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
Wanabodi!

Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.

Conclusion
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, hili pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa mmefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye serikali moja?

Wasalaam,
Paskali.
P
 
Wakuu naomba kwa yeyote anayejua anisaidie namna ya kuhama kutoka kuwa mtanzania wa Tanzania bara na kuwa mtanzania wa Zanzibar yaani kuwa mzanzibari

Nataka kuwa mzanzibari wa kuhamia ili niwe na haki ya kumiliki ardhi kule na Tanzania bara pia, kugombea uongozi kule na nafasi za Muungano kama utais lakini pia niweze kugombea ubunge kule ili niweze kuteuliwa kuwa waziri katika wizara za muungano na zisizo za muungano kama ilivyo kwa Makame Mbarawa anayeongoza wizara isiyo ya muungano ambayo ni ya Tanzania bara lakini kwa mtu kutoka Tanzania bara hawezi kuteuliwa kuongoza wizara Zanzibar.
Nikiwa mzanzibari naweza kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya Zanzibar au Tanzania bara kama ilivyo kwa Shaka ambaye ni DC huku Tanzania bara lakini hakuna mtanzania bara anayeweza kuwa Sheha, DC au RC kule Zanzibar.

Nataka kuwa mzanzibari kwakuwa wazanzibari wanajitambua sana linapokuja suala la nchi yao na uraia wao tofauti na watanganyika waoga hawataki kuwepo kwa Tanganyika yao utadhani ikiwepo watakufa wote. Ni watu waoga sana na hawaipendi asili na nchi yao kama wazanzibari. Naombeni meongozo wa kuachana na Tanganyika nimechoka kuionea aibu nchi yangu bora nihame kabisa. Kumbukeni KILA MZANZIBARI NI MTANZANIA LAKINI SI KILA MTANZANIA NI MZANZIBARI. Naombeni wazanzibari mnipoker nije kushirikiana nanyi kuipigania Zanzibar
Nenda Zanzibar, onana na uhamiaji wa huko watakupa utaratibu.
 
Nilivutiwa sana na kichwa cha mada yako: " Naomba kujulishwa taratibu za kubadili uraia kutoka kuwa mtanzania bara na kuwa mzanzibari"
Hili pekee lingejitosheleza sana kwa mjadala wa mada hii bila ya kuweka hayo maelezo mengine, ambayo nadhani yamepanuwa sana mada na kuififisha.

Mimi nilivutiwa na hiki kichwa cha mada, kwa sababu sijui taratibu zikoje, mtu ukitaka kuwa mZanzibari ukiwa unatokea Tanganyika.

Wenye kujuwa utaratibu huo tafadhali uelezeni kwenye mada hii.
Lazima kuna vigezo vyao, Mbona Mzee Mwinyi na Mzee Jumbe wote ni Watanganyika na wakapata mpaka Urais wa Zanzibar.

Ni kufata taratibu zao tu na vigezo vipo tayari, nahisi licha ya watu hao wawili maarufu, kuna wengi wengine wasio maarufu wana uraia wa huko.
 
Itakuwa ngumu kuliko kuomba uraia wa Israeli.
Nani alikwambia uraia wa israel mgumu kuupata? Wanahaha kutafuta watu huko.

Nani anataka rusha roho za Hams, Hebolla na sasa Wayemeni.

Wale Watanzania wa Bashe walirudi au wameselelea hukohuko?
 
Nani alikwambia uraia wa israel mgumu kuupata? Wanahaha kutafuta watu huko.

Wale Watanzania wa Bashe walirudi au wameselelea hukohuko?
Uwe unalala au ma wewe mme ameenda shirikishi?

Makosa ya kiufundi achana nayo
 
Muungano wetu ni complicated kidogo! Lakin kichaa pekee narudia kichaa pekee ndo atadhubutu kuvunja muungano.Hakuna namna mtu mwenye akili timamu atakubal kupoteza sehem ya nchi yake!Russia na ukubwa wake inanyang'anya maeneo ya ukraine ikidai ni yake nakadhalika. Halaf mwendawazim mmoja anataka kutengane ili tuanze kushare vitu tulivyokuwa tunapata bure na kwa ukubwa kama bahari na airspace.
 
Lazima kuna vigezo vyao, Mbona Mzee Mwinyi na Mzee Jumbe wote ni Watanganyika na wakapata mpaka Urais wa Zanzibar.

Ni kufata taratibu zao tu na vigezo vipo tayari, nahisi licha ya watu hao wawili maarufu, kuna wengi wengine wasio maarufu wana uraia wa huko.
Kwani raia wa huko ni nani hasa. Waarabu?

Jumbe na Mwinyi walikuwa huko kabla ya Tanzania kuwepo, kwa hiyo wao hili haliwahusu. Lakini akina Karume na wao walikuwa huko, Wazanzibari kamili.
 
Back
Top Bottom