Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Ndoa ni stara kwa mwanamke! Hivyo mwanamke anahitaji ndoa kuliko mwanaume
Wanawake wamekuwa wengi ama ni wengi kuliko wanaume... Hivyo ndoa imekuwa kitu adimu hasa ukizingatia kuwa.. Pamoja na uchache huo wa wanaume bado karibia nusu yao si waoaji
Sasa kutokana na hamaniko hilo la kuhitaji ndoa wengi wamejikuta wakiangukia kwenye mikono ya wanaume wasio sahihi
Kuna kauli moja mabinti wenye kutaka ndoa wanaitumia bila kujua madhara yake! Hii kauli ya kusema "hata nikimpata anayepumua tu inatosha!"
Wadogo zangu wa kike hakuna kauli ya kiwaki kama hii... Unaingia kwenye ndoa na sio kwenye mapenzi.. Kauli huumba na Mungu humpa kitu alichokiomba!
Hivi mnajua kwa hakika mwanaume anayepumua tu yukoje!? Si mlemavu wa viungo ama akili.. Bali ni mlemavu wa ufahamu na kujitambua yeye ni nani na anapaswa kufanya nini kwa wakati gani
Unaingia kwenye ndoa ambayo ni mahusiano ya kudumu mpaka talaka itakapowatenganisha! Kifo ni mustakabali
Unapaswa kuwa na mtu anayejitambua, anayejali, anayeweza kubeba majukumu ya baba.. Na anayeweza kuzikabili changamoto kwa weledi kwa hekima na kwa utulivu
Mwanaume anayepumua tu ni yule ambaye utamuacha kitandani uende kazini ukiwa umeshamuandalia mpaka chai, Ataamka kwa kuchelewa, hawezi kutandika hata kitanda. Atakunywa chai na kuacha kila kitu hapo.. Hatafanya chochote mpaka urudi ufanye vyote na bado usiku umpe!
Wengine anaweza kuwa na kazi lakini huoni tofauti yoyote na asiye na kazi majukumu yote unayabeba wewe. Mwanzoni mwa ndoa utaona kama utaweza.. Lakini taratibu mkishazoeana utaanza kuliona tatizo! Na tatizo litazidi kujipambanua kadiri familia itakavyoongezeka. Watoto, Wafanyakazi, Biashara, Ufugaji nk
Utajikuta usipofanya wewe yeye hagusi kitu.. Matumizi ya nyumbani
Mahitaji ya watoto shuleni na nyumbani. Mishahara ya wafanyakazi. Manunuzi ya vitu kama mna biashara. Kuhudumia mifugo kama mnafuga nk
Ikitokea umepata safari ya siku chache tu ndio utaliona tatizo kubwa katika uhalisia wake..utakuta kila kitu kimeparaganyika Hesabu kwenye biashara, Manunuzi hakuna, Loss kama zote. Kama ni mifugo si ajabu kukuta mingine imekufa kwa kukosa huduma na mingine kupotea kwa kukosa ufuatiliaji.
Anaweza kufanya kikubwa ni matumizi ya pesa zako.. Ana we za Ku control mpaka account zako. Anachoweza kingine ni kukuzalisha kila mwaka bila kujali future ya hao watoto. Mwisho wa siku unajikuta unajutia majuto yasiyo na faida.. Unajikuta binti mdogo unazeeka kabla ya umri na kuandamwa na magonjwa yatokanayo na msongo wa mawazo
Nina mengi ya kuandika.. Lakini ya msingi ni haya! Kama ukiisoma hii mada na kuielewa naamini utabadili mtazamo wako kuhusu mwanaume wa kukuoa
Chelewa kuolewa lakini olewa na mtu sahihi.. Si wali nazi wala si mwanaume suruali wala si yule anayepumua tuu