Hivyo navyo ni vipengele muhimu sana kwenye ustawi wa ndoa.. Lakini pia ni muhimu kwenye first appearance ikupe walau nusu ya picha ya mtu mwenyewe kimaishaZodiac and Numerology ni muhimu kwa mwanadamu hasa kwenye kupengele cha kusudio la muunganiko wa kipindi kirefu. Nakurudishia pasi mzee wa kilinge kwako Mshana JR
Nakazia hapaπ¨mku wakimaliza kuchangia hii mada naomba uje na mada nyingine kuhusu sisi wadogo zako wa kiume wenye kutafuta mke wa kuoa
Mitoto ya siku hizi ya kike Yana roho ya Nyegere, kiburi, sio wasikivu, wanakula nyoka Hadi nyoka zinawaogopaNdoa ni stara kwa mwanamke! Hivyo mwanamke anahitaji ndoa kuliko mwanaume
Wanawake wamekuwa wengi ama ni wengi kuliko wanaume... Hivyo ndoa imekuwa kitu adimu hasa ukizingatia kuwa.. Pamoja na uchache huo wa wanaume bado karibia nusu yao si waoaji
Sasa kutokana na hamaniko hilo la kuhitaji ndoa wengi wamejikuta wakiangukia kwenye mikono ya wanaume wasio sahihi
Kuna kauli moja mabinti wenye kutaka ndoa wanaitumia bila kujua madhara yake! Hii kauli ya kusema "hata nikimpata anayepumua tu inatosha!"
Wadogo zangu wa kike hakuna kauli ya kiwaki kama hii... Unaingia kwenye ndoa na sio kwenye mapenzi.. Kauli huumba na Mungu humpa kitu alichokiomba!
Hivi mnajua kwa hakika mwanaume anayepumua tu yukoje!? Si mlemavu wa viungo ama akili.. Bali ni mlemavu wa ufahamu na kujitambua yeye ni nani na anapaswa kufanya nini kwa wakati gani
Unaingia kwenye ndoa ambayo ni mahusiano ya kudumu mpaka talaka itakapowatenganisha! Kifo ni mustakabali
Unapaswa kuwa na mtu anayejitambua, anayejali, anayeweza kubeba majukumu ya baba.. Na anayeweza kuzikabili changamoto kwa weledi kwa hekima na kwa utulivu
Mwanaume anayepumua tu ni yule ambaye utamuacha kitandani uende kazini ukiwa umeshamuandalia mpaka chai
Ataamka kwa kuchelewa
Hawezi kutandika hata kitanda
Atakunywa chai na kuacha kila kitu hapo..
Hatafanya chochote mpaka urudi ufanye vyote na bado usiku umpe!
Wengine anaweza kuwa na kazi lakini huoni tofauti yoyote na asiye na kazi majukumu yote unayabeba wewe
Mwanzoni mwa ndoa utaona kama utaweza.. Lakini taratibu mkishazoeana utaanza kuliona tatizo!
Na tatizo litazidi kujipambanua kadiri familia itakavyoongezeka
Watoto
Wafanyakazi
Biashara
Ufugaji nk
Utajikuta usipofanya wewe yeye hagusi kitu..
Matumizi ya nyumbani
Mahitaji ya watoto shuleni na nyumbani
Mishahara ya wafanyakazi
Manunuzi ya vitu kama mna biashara
Kuhudumia mifugo kama mnafuga nk
Ikitokea umepata safari ya siku chache tu ndio utaliona tatizo kubwa katika uhalisia wake..utakuta kila kitu kimeparaganyika
Hesabu kwenye biashara
Manunuzi hakuna
Loss kama zote
Kama ni mifugo si ajabu kukuta mingine imekufa kwa kukosa huduma na mingine kupotea kwa kukosa ufuatiliaji
Anaweza kufanya kikubwa ni matumizi ya pesa zako.. Ana we za Ku control mpaka account zako
Anachoweza kingine ni kukuzalisha kila mwaka bila kujali future ya hao watoto
Mwisho wa siku unajikuta unajutia majuto yasiyo na faida.. Unajikuta binti mdogo unazeeka kabla ya umri na kuandamwa na magonjwa yatokanayo na msongo wa mawazo
Nina mengi ya kuandika.. Lakini ya msingi ni haya! Kama ukiisoma hii mada na kuielewa naamini utabadili mtazamo wako kuhusu mwanaume wa kukuoa
Chelewa kuolewa lakini olewa na mtu sahihi.. Si wali nazi wala si mwanaume suruali wala si yule anayepumua tuu
Nimesoma uzi na comments zake zote so far, midume haijaja kupokea ushauri bali imeunga mkono na kuongezea nyama kwenye bandiko la kaka yao, kwahiyo ni kazi kwa washauriwa kuchukua au kupuuza ushauri.Mada imewaita wadogo zake Mshana wa kike ajabu naona midume na ndevu zao ndio wamejaa hapa, hii kiuhalisia tuite vipi?
ππππMada imewaita wadogo zake Mshana wa kike ajabu naona midume na ndevu zao ndio wamejaa hapa, hii kiuhalisia tuite vipi?