Cvez
JF-Expert Member
- May 19, 2018
- 4,405
- 13,411
Sasa Waislamu tunahusika vipi katika hili ndugu? Mbona ghafla sanaWasabato, wakatoliki na waislam wanaabudu wasichokijua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa Waislamu tunahusika vipi katika hili ndugu? Mbona ghafla sanaWasabato, wakatoliki na waislam wanaabudu wasichokijua
Hicho ulichoandika ni mgawanyiko.wa kanisa katoliki kuwa mawili na baadaye vikaja vipande vingineHISTORIA YA KANISA B.
Kati ya mwaka 700 - 1054 kulitokea mgogoro mkubwa wa Kanisa ambao hatimaye ulikuja kuligawa rasmi Kanisa hapa duniani katika mapande makubwa mawili mwaka 1054. Upande wa Magharibi uliitwa Western Roman Catholic Church na ulikuwa unamtambua Askofu Mkuu wa Rumi (Papa) kama ndio kiongozi wao. Upande wa Mashariki uliitwa Eastern Othordox (Catholic) Church na ulikuwa ukimtambua Askofu Mkuu wa Constantinople (Patriarch) kama kiongozi wao.
Sababu zilizopelekea mgogoro na mpasuko ule zilikuwa nyingi zikiwemo: 1. Matumizi ya taswila na sanamu (images) katika ibada (the iconoclastic controversy). Kutokana na changamoto ya Uislamu eneo la Mashariki, mwaka 726, Mtawala wa Dola ya Byzantine alipiga marufuku matumizi ya taswira na sanamu (images) katika ibada. Askofu Mkuu wa Constantinople aliunga mkono. Kitendo kile kililaaniwa vikali sana na Askofu Mkuu wa Rumi (Papa) kwa sababu kuu mbili; mosi, Magharibi hakukuwa na Uislamu hivyo hawakuwahi kushutumiwa na Waislamu kuwa walikuwa wanaabudu sanamu kama walivyokuwa wamatuhumiwa watu wa Mashariki ambako tayari Waislamu walianza kuiteka. Pili, Papa alisisitiza kuwa watawala wa kisiasa hawakupaswa kuingilia maswala ya Kanisa. Suala hili lilikuja kupungua nguvu mwaka 843 baada ya Mkutano (Mtaguso) Mkuu wa Kanisa la Mashariki kupitisha matumizi ya picha tu lakini sio sanamu katika ibada. Hata hivyo, tayari umoja wa Kanisa ulikuwa umeathiriwa sana.
2. Mgogoro kuhusu asili ya Roho Mtakatifu (the Filioque Controversy). Mkutano Mkuu wa Nikea ulishatoa msimamo wa kiimani kuwa "Roho Mtakatifu atoka kwa Baba ...". Baadaye, katika Mkutano Mkuu ambao haukuwahusisha Kanisa la Mashariki, Kanisa la Magharibi lilifanya marekebisho katika tamko la imani (amendment) na kuandika kuwa "Roho Mtakatifu atoka kwa Baba na kwa Mwana ...". Kitendo hiki kilipelekea Kanisa la Mashariki kulituhumu Kanisa la Magharibi kwa uasi! Kwao maamuzi kama yale yalihitaji Mkutano wa Kanisa zima ambao ungehusisha Maaskofu wote. Hadi leo, Kanisa la Mashariki linaikiri Imani ya Nikea kama ilivyokuwa mwanzo pasipo mabadiliko wakati Kanisa la Magharibi (pamoja na matawi yake) limeendelea kuikiri Imani ya Nikea iliyobadilishwa kipengere hicho. Baadhi ya Makanisa siku hizi hutambua kiri zote mbili.
3. Ugomvi wa Madaraka. Askofu Mkuu wa Rumi (Papa) alitaka atambuliwe kuwa ndiye Mkuu kuliko wote wakati Askofu Mkuu wa Constantinople (Patriarch) aligoma kumtambua naye akisisitiza kuwa walikuwa na mamlaka sawa.
4. Hakukuwa na mpaka rasmi kati ya mamlaka ya Rumi na mamlaka ya Constantinople hivyo kuzua mizozo ya kiutawala.
5. Mashariki, Kanisa lilikuwa linatii mamlaka ya Watawala wa Dola (serikali) wakati Kanisa la Magharibi lilisisitiza kutokuingiliwa na Dola na lilisisitiza viongozi wa Kanisa kuwasimamia viongozi wa serikali kuhusu maadili, nk.
6. Tofauti za kitamaduni: Magharibi walikuwa wakizungumza Kilatini wakati Mashariki walikuwa wakizungumza Kiyunani (Kigiriki). Pia kulikuwa na umbali wa maili 1000 kati ya Rumi na Constantinople.
7. Tofauti za ki-Liturgia: Hizi zilihusu mambo madogo madogo kama kutumia au kutokutumia mikate iliyochachushwa au isiyochachushwa katika sakramenti au ekaristi, kula mkate au kutokula mkate pamoja na divai wakati wa meza ya Bwana; Makasisi/Mapadre kunyoa au kutokunyoa ndevu na kuoa au kutokuoa, nk.
Mgogoro huo uliendelea hadi mwaka 1054 wakati Askofu Mkuu wa Rumi alipoandika waraka wa kumtenga Askofu Mkuu wa Constantinople kwa kutotii, naye Askofu Mkuu wa Constantinople akaandika waraka wa kumtenga Askofu Mkuu (Papa) wa Rumi. Hivyo Maaskofu Wakuu wa Makanisa Makuu ya Rumi na Constantinople wakawa wametengana na ndio Kanisa likawa limegawanyika rasmi. Kanisa la Magharibi liliendelea kugawanyika na kuzaa matawi kwa mfuatano ufuatao kuanzia lipi lilianza; Waldensian, Moravian, Lutheran, Mennonite, Presbyterian, Baptist, Anglican, Methodist, Assemblies of God, nk. Kanisa la Mashariki halijwahi kukumbwa na migogoro au migawanyiko ingawa lina matawi mengi kama vile Ethiopian Church, Coptic Church (Kanisa la Misri), Greek Orthodox, Russian Orthodox, Eastern Orthodox, Syrian Church, nk.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT).
Mtoto ni dharuraNajiuliza tu hivi mtoto akidumbukia shimoni hawato mtoa kwasababu ya siku ya sabato?
Kwamba ulikuta kafungua duka?Yamekukuta kama yangu inaniumga mpaka leo japo imepita miaka
nilitoka home pana umbali kidogo na huyo mama kwenda kununua sabuni nafik ananiambia aah leo sabato nikondoka kwa uchungu sana.
Wanasahau hata Yesu liwaulizaga watoto zenu sijui wanapunda wakizama mtoni hamtawatoa kisa sabato?
Ivi mfano unatakiwa kumeza dawa na huna maji , au unahitaji maji kusafisha jeraha, hayo yote cyo dharura , au unataka kupika na huna maji , au mmi ndo cjui dharuraMtoto ni dharura
Maji siyo dharura
Nenda hospital au kaombe kwingineIvi mfano unatakiwa kumeza dawa na huna maji , au unahitaji maji kusafisha jeraha, hayo yote cyo dharura , au unataka kupika na huna maji , au mmi ndo cjui dharura
Halafu hakuna kifungu chochote kinachotamka kwenye Biblia kuwa Sabato ni siku ya JumamosiShida ni kutoyaelewa maandiko,kiasi kwamba mtu/watu tunakuwa watumwa.Yesu alishasema "Sabato iliwekwa kwaajili ya watu na si watu kwaajili ya sabato".
Huna hoja .....au ...uelewa wako bado ni mdogoNenda hospital au kaombe kwingine
MKUU SIO KWA UBAYA ILA nilikuwaga Nakuheshimu sikudhania kama na Wewe Unaamini huo Ujinga.Mwamposa usimguse hapo, huyo ni Mtumishi wa Mungu.
Watu wamekesha leo kwenye mkesha wa chako ni chako.
Yaani yuko tayari mtu afe kwa kiu kisa sabato,huu mzigo.
Hakusema ana kiu elewa mada kasema anataka hauziwe kumbe akili ya yako haina akili? Umesoma shule au umesoma vitabu?🤣Yaani yuko tayari mtu afe kwa kiu kisa sabato,huu mzigo.
Nimesoma matako yakoHakusema ana kiu elewa mada kasema anataka hauziwe kumbe akili ya yako haina akili? Umesoma shule au umesoma vitabu?🤣
Kivipi?yenyewe haikuletwa Afrika?Dini ya haki na yenye utaratibu wa jinsi ya kuishi ni ISLAM pekee nyingine zote ni utapel
Tatizo wana theolojia wengi hujikita zaidi kwenye historia ya kanisa katoliki sio historia ya Ukristo kwenye BibliaWell said mkuu,,
Hawa jamaa wanataka kupotosha watu kwa kulikuza dhehebu lao!
Sijui wanadhani watu wote ni wajinga kama wao?!
Wasome biblia waachane na mapokeo yasiyo na matunda!
Wokovu unatoka kwa wayahudi , sio Vatican!
sadaka hailazimishwi ndugu kilaza.Sasa kama hauzi kwa sababu ya kiimani basi ngekupa tu kama sadaka