Naomba leo mniache niseme na Wasabato, nimeamua kuamka nao leo

Hicho ulichoandika ni mgawanyiko.wa kanisa katoliki kuwa mawili na baadaye vikaja vipande vingine

Lakini kuna makanisa ambayo hayakuwa connected labisa na kanisa la Rumi wala hayakuwa sehemu yake yaliendelea na imani zao kwenye mataifa mbalimbali

Sema tatizo wana theolojia wengi hujikita tu kwenye historia ya ukatoliki wanasahau kuwa ukristo haukuanzia kwenye uromani katoliki

Wanasahau kufuatilia hizo branch zingine ambazo hazikuwa connected na kanisa katoliki
 
Ukristo asili yake ni Israel, kwa wayahudi! Na vitabu vyote ndani ya biblia vimeandikwa na wayahudi (ukiondoa LUKA ambaye hata hivyo bado kuna utata kama alikuwa myahudi au myunani mgiriki).

Maana LUKA hakuwa kati ya mitume wa yesu wale thenashara (12) lakini inadaiwa alikuwa ni mmoja wa wafuasi wa yesu nguli, wengine wanasema alikuwa daktari (tabibu) hapo bado wanazuoni wa biblia wanatofautiana!

Lakini vitabu vingine vyote ndani ya biblia vimeandikwa na wayahudi wenyewe, na Ukristo ulianzia uyahudi JERUSALEM siku ya pentekoste (ukiacha siku alizohubiri Yesu mwenyewe).

Japo baadae kwa mateso ya wayahudi wenye kushika dini ya kiyahudi ilibidi mitume wengi na wakristo wengi wa kiyahudi kukimbiloa nji jirani ya Siria, Damascus, wengine wakaenda Antiokia ambapo huko ndipo jina WAKRISTO lilipoanza kuitwa rasmini.

Sasa jamaa zangu wanakuja hapa na kupotosha watu kwamba eti BIBLIA IMEANDIKWA sijui na wakatoliki bla bla blaaaa!

Tuache huu upotofu na uzushi hausaidii kitu! Mungu ni mmoja, Bwana wetu Yesu Kristo ni mmoja na imani moja!

Inatosha! hayo ya uzushi na udhehebu hayana tija Sana!
 
Kwamba ulikuta kafungua duka?
 
Sasa si ungeingia ndani akupe Maji yake aliyoweka akiba...
Yaani asikupe ya kuuza..
Simple tu
 
Ivi mfano unatakiwa kumeza dawa na huna maji , au unahitaji maji kusafisha jeraha, hayo yote cyo dharura , au unataka kupika na huna maji , au mmi ndo cjui dharura
Nenda hospital au kaombe kwingine
 
Shida ni kutoyaelewa maandiko,kiasi kwamba mtu/watu tunakuwa watumwa.Yesu alishasema "Sabato iliwekwa kwaajili ya watu na si watu kwaajili ya sabato".
Halafu hakuna kifungu chochote kinachotamka kwenye Biblia kuwa Sabato ni siku ya Jumamosi

Mungu alisema fanya kazi siku sita ya saba pumzika.Sabato iwe siku gani kwa wiki ni makubaliano ya jamii eneo husika cha msingi wafanye kazi siku sita ya saba wapumzike yaweza kuwa siku yeyote ya juma yaweza kuwa alhamisi,ijumaa,Jumamosi au jumapili au yeyote
 
Yaani yuko tayari mtu afe kwa kiu kisa sabato,huu mzigo.
 
Tafuta pesa acha makasiriko shida zako zisikulazimishe kuwapangia Watu namna ya kuishi kwanza wewe popo kweli yaani unakosaje maji ndani ya nyumba afu unaenda kwa msabato kumtengulia sabato yake kwa akili yako finyu.
 
Ungetumia energy hii kutukana serikali kuwaletea miundo mbinu ya maji tungefika mbali,ila mtu maji yake,imani yake,why umtusi?tafuta hela kijana,ukiwa lofa kila mtu utamuona KAVU
 
Well said mkuu,,

Hawa jamaa wanataka kupotosha watu kwa kulikuza dhehebu lao!

Sijui wanadhani watu wote ni wajinga kama wao?!

Wasome biblia waachane na mapokeo yasiyo na matunda!

Wokovu unatoka kwa wayahudi , sio Vatican!
Tatizo wana theolojia wengi hujikita zaidi kwenye historia ya kanisa katoliki sio historia ya Ukristo kwenye Biblia

Kwa hiyo wana theolojia wengi huelezea historia ya Ukristo kama historia ya kanisa la Roman Catholic

Wanaanza na u roman Catholic ulivyoanza na baadaye kugawanyika na kuongelea madhehebu yaliyoibuka kutokea Ukatoliki na kujifanya wasomi wa Historia ya kanisa

Historia ya kanisa haianzii kwenye mwanzo wa kanisa katoliki.Hilo lilianzishwa miaka kibao toka Yesu afe ,kusulubiwa na kufufuka ni dini ilikuja baadaye sana tena mno

Ndio maana hupotoka wakiongelea historia ya Ukristo

Wanajikita kuongelea historia ya kanisa la Roman Catholic badala ya historia ya Ukristo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…