Naomba majibu rasmi ya maandishi kutoka BOT juu ya wao kupokea pesa haramu zilizopitwa na wakati, BOT inafanya biashara na maharamia?

Naomba majibu rasmi ya maandishi kutoka BOT juu ya wao kupokea pesa haramu zilizopitwa na wakati, BOT inafanya biashara na maharamia?

Benki kuu ya Tanzania (BOT) wanawajibu wa kutoa ufafanuzi juu ya kwanini wanapokea pesa haramu kutoka kwa maharamia? Nafafanua ni kwanini nasema hivi…

Pesa ya zamani ikitaka kufutwa na kuletwa pesa mpya kwenye mzunguko, BOT hutoa tangazo rasmi juu ya muda wa kuanza kupokea pesa za zamani pamoja na tarehe ya mwisho ya kuzibadilisha pesa hizo.

Pia katika tangazo hilo, huwa wanaweka wazi kabisa kwamba, tarehe ya mwisho ya kubadilisha pesa hizo ikifika, basi pesa hizo hazitakuwa halali tena, na hazitafaa kutumika kwa ajili ya malipo popote pale nchini au duniani!

View attachment 3137012
View attachment 3137014

Pesa ambayo waTz tunaambiwa tupeleke ili tupewe mpya moja wapo ni hiyo hapo kwenye picha. Sasa mtu unajiuliza, hii pesa tarehe yake ya kikomo ya kuibadili ilishapita, na hivyo automatically pesa hii ni haramu kutumika au kubadilishwa popote pale nchi au duniani! Leo imekuwaje BOT wanataka kufanya biashara haramu?!

Nini kinaweza kuwa kinatokea?

- Mara nyingi tulimsikia JPM akitishia kubadilisha pesa zote na kuleta mpya, hili alitishia watu walichombia malorry ya pesa na kuyafukia chini kwenye sandarusi ili kuzificha pesa hizo za biashara haramu, maana yake hawawezi kupeleka bank kutokana na kukosa maelezo juu ya chanzo cha pesa hizo. Mara nyingi pesa hizi huwa zinatakatishwankwa kutumia makanisa ya kikokole na biashara zingine za kusafishia pesa chafu. Mfano CRDB SADAKA ni genge la kutakatisha hizi pesa (Money Laundering)kwa kuzipitishia kwa akina Mwamposa na kuwapa commission tu.

Sasa linapokuja tangazo la ghafla la kubadili fedha, na unakuta muda ulioweka labda ni miezi miwili tu, ni ngumu kwa aliyefukia Trillion 10 chini ya ardhi kuzinadili au kuzitakatisja zote kwa muda mfupi kiasi hicho, hivyo utakuta kuna pesa haramu kama Trillion 5 hivi anaweza kubaki nazo chini ya ardhi baada ya tarehe halali ya kubadilisha pesa kupita, na ndio inakuwa imekula kwake.

Sasa imekuja awamu hii ya 6 na kutaka kutafuta pesa za uchaguzi kwa njia haramu hadi naona aibu, ni aibu. Pesa haramu ambayo ilishaharamishwa automatically baada ya tarehe ya kuzibadili kupita, ndio wanataka wamsaidia huyo mtu kuzibadilisha pesa haramu na kumchapishia noti mpya, ambayo bila shaka italeta inflation kushusha zaidi thamani ya shilingi, maana akipata tu noti mpya, atazibadili kuwa dollar chap na kukimbia nazo nje ya nchi!

BOT chagueni moja, mnipe majibu ya maandishi au muaibike dunia nzima kwa kutakatisha pesa haramu!
Kama kuna Ukweli kuhusu suala hili.

Hiyo inaonekana kama vile kuna dili fulani hivi. Madili ya namna hiyo yalishawahi kutokea nchini Nigeria na nchini Liberia.

Mathalani, nchini Liberia ilitokea kwamba baadhi ya Wanasiasa Watawala wa nchi hiyo ambao ni Wahalifu (Mafisadi) walishirikiana na Watendaji wa Benki Kuu ya nchi hiyo walitoa zabuni ya kuchapisha Noti Mpya za fedha za nchi hiyo kwa Kampuni Moja huko Ulaya. Baada ya noti hizo kuchapishwa kutoka kiwandani kwa Mzabuni, zilisafirishwa kwenye ma-container kupitia baharini hadi bandari ya Mji Mkuu wa nchi hiyo Monrovia. Hao Watawala wapiga madili walifanikiwa kuiba Jumla ya Makontena manne (4) yaliyobeba Noti Mpya, makontena hayo yenye fedha (Noti mpya) yaliibiwa hapo hapo bandarini na kisha kupotelea Mahali kusikojulikana na Kamwe hayakuwahi kupatikana tena hadi leo.
Watawala wa nchi za Afrika na madili ya kifisadi ni 'damu damu' kama samaki na maji
 
Daah, hii iliwahi tokea hata hapa Tz, maafisa wa BOT walijichapishia kimagendo kontena mbili za ziada ambazo haieleweki alichukua nani..,

Na kibaya zaidi, uchumi unafifishwa na vitendo vya kuchapisha noti bila utaratibu ili kulipa mishahara ya ndani.., pesa imepoteza sana thamani yake…

BOT mtaongeza inflation kwa hili zoezi la kuwapa maharamia pesa mpya
 
Sikusoma maelezo yote ila kwa kutumia akili naweza kubashiri ufisadi unao fanyika hapo ...ni kuwa 👉 PESA HIZO ZILIKUWA BENKI KUU NA KUCHUKULIWA NA WAHUNI ...YAANI WAKUU WA BANKI KUTOKA KWENYE MAGHARA YAO YA PESA ZA ZAMANI KISHA NDIYO WANAKUJA NA HIYO RUHUSA ILI WAZIRUDISHE NA KUPEWA PESA MPYA ...yaani wahuni wanachota mamilioni ya pesa za zamani kama hiyo elfu 10 kisha wanazirudisha na kupewa pesa mpya za halali kwa sasa ...wanajua pesa za zamani hazizingatiwi kwenye masanduku ya bank hivyo wakizichota hakuna wa kuuliza maana hazina kazi tena sasa ili ziweze kuwa na faida hizo pesa za zsmani walizo zichota hapo hapo bank kuu ni kualalisha ubadilishaji kwa sasa ...tatizo rais tuliye naye ni Zero brain hana akili ya kutambua huu mchezo mchafu
Hata Nigeria uliwahi kufanyika wizi na ufisadi kama huu, Rais Buhari alipoapishwa tu na kushika nadaraka ya uRais aliamuru wahusika wote wakamatwe na kufikishwa Mahakamani.
 
IMG_2213.jpeg
 
Kinachofuata hapa ni kupandisha tu kodi za nyumba, haiwezekani pesa ishuke thamani kiasi hiki halafu mtu alipe kodi hiyo hiyo kwa miaka 10
Ukiona kuna tatizo kubwa namna hii la kushuka kwa ghafla kwa thamani ya fedha katika nchi wakati nchi husika haipo vitani, tambua ya kwamba Utawala uliopo madarakani kuna namna mbaya inajihusisha nayo, aidha fedha chafu ya magendo imeingizwa kweye mzunguko wa fedha au kuna suala la uchapishaji wa fedha kwa njia zisizo halali. Mfano mzuri kwenye suala hili ni nchi ya Zimbabwe.
 
Kuna wajinga wanasema mitano Tena.
Mtavuna mabua 2030
Hii ni hatari, kuna uwezekano mkubwa serikali inachapisha pesa kiholela, haiwezekani pesa ishuke thamani kiasi hiki na hatupo vitani

Back
Top Bottom