Naomba majibu rasmi ya maandishi kutoka BOT juu ya wao kupokea pesa haramu zilizopitwa na wakati, BOT inafanya biashara na maharamia?

Kama kuna Ukweli kuhusu suala hili.

Hiyo inaonekana kama vile kuna dili fulani hivi. Madili ya namna hiyo yalishawahi kutokea nchini Nigeria na nchini Liberia.

Mathalani, nchini Liberia ilitokea kwamba baadhi ya Wanasiasa Watawala wa nchi hiyo ambao ni Wahalifu (Mafisadi) walishirikiana na Watendaji wa Benki Kuu ya nchi hiyo walitoa zabuni ya kuchapisha Noti Mpya za fedha za nchi hiyo kwa Kampuni Moja huko Ulaya. Baada ya noti hizo kuchapishwa kutoka kiwandani kwa Mzabuni, zilisafirishwa kwenye ma-container kupitia baharini hadi bandari ya Mji Mkuu wa nchi hiyo Monrovia. Hao Watawala wapiga madili walifanikiwa kuiba Jumla ya Makontena manne (4) yaliyobeba Noti Mpya, makontena hayo yenye fedha (Noti mpya) yaliibiwa hapo hapo bandarini na kisha kupotelea Mahali kusikojulikana na Kamwe hayakuwahi kupatikana tena hadi leo.
Watawala wa nchi za Afrika na madili ya kifisadi ni 'damu damu' kama samaki na maji
 
Daah, hii iliwahi tokea hata hapa Tz, maafisa wa BOT walijichapishia kimagendo kontena mbili za ziada ambazo haieleweki alichukua nani..,

Na kibaya zaidi, uchumi unafifishwa na vitendo vya kuchapisha noti bila utaratibu ili kulipa mishahara ya ndani.., pesa imepoteza sana thamani yake…

BOT mtaongeza inflation kwa hili zoezi la kuwapa maharamia pesa mpya
 
Hata Nigeria uliwahi kufanyika wizi na ufisadi kama huu, Rais Buhari alipoapishwa tu na kushika nadaraka ya uRais aliamuru wahusika wote wakamatwe na kufikishwa Mahakamani.
 
Kinachofuata hapa ni kupandisha tu kodi za nyumba, haiwezekani pesa ishuke thamani kiasi hiki halafu mtu alipe kodi hiyo hiyo kwa miaka 10
Ukiona kuna tatizo kubwa namna hii la kushuka kwa ghafla kwa thamani ya fedha katika nchi wakati nchi husika haipo vitani, tambua ya kwamba Utawala uliopo madarakani kuna namna mbaya inajihusisha nayo, aidha fedha chafu ya magendo imeingizwa kweye mzunguko wa fedha au kuna suala la uchapishaji wa fedha kwa njia zisizo halali. Mfano mzuri kwenye suala hili ni nchi ya Zimbabwe.
 
Kuna wajinga wanasema mitano Tena.
Mtavuna mabua 2030
Hii ni hatari, kuna uwezekano mkubwa serikali inachapisha pesa kiholela, haiwezekani pesa ishuke thamani kiasi hiki na hatupo vitani

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…