Naomba Mkopo wa TSh 20,000 – Nimekwama kwa Sasa

Status
Not open for further replies.
Kwa uzoefu wangu watu wanaokopa elfu 10, 20,30,40 hadi 50 wengi wao huwa ni watata sana kwenye kuleta rejesho.

Kwa mtu anayetaka kulinda amani ya moyo wake ni vema akampatia mtu kiasi hicho bila kutegemea malipo.
 
Ukiona mtu analia lia kusaidiwa vipesa vidogo kuanzia 1,000-20,000/= jua huyo ni Changamoto katika jamii yake.

How comes ulie kukoswa 20K, wakati mikopo ya online imejaa!?

Mimi Mgodi wananikopesha sh 200K, Songesha kiwango cha mkopo wangu ni Sh 600K, hii ni laini ya Voda tu.

Kama kweli wewe ungekuwa mwaminifu ,20K isingekupiga nchenga

Kuna mawili,wewe ni Teja au mkamalia ukisindikizwa na Aviator
 
Naelewa utakuwa unapitia hali ngumu kwa sasa. Natamani ujue kipindi cha hali ngumu sio kipindi cha kujiona mnyonge na kufanya/kutamka vitu vitakavyokupa majibu ya kukuumiza. Pamoja na hali ngumu yako angalia ni wapi unatafuta msaada sio popote tu hata kwa sehemu unayojua itakuumiza. any way nisiseme mengi ila nakuombea ujasiri wa kusimama na kujua jinsi ya kupambana bila kutengeneza maumivu. Wewe sio wa kwanza kupata mapito... na Mungu akutangulie.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…