Naomba msaada mume wangu amekamatwa na polisi nyumbani saa nane usiku kwa tuhuma za kununua simu ya wizi. Vituo vyote wanadai hayupo na tusimtafute

its either ana link ya ujambazi au ugaidi. Ni kweli wasihangaike kumtafuta..

Hii iwe somo tuache kununua simu za mikononi kwa watu ambao hatuwafahamu..
Sheria hazipo hivyo mkuu hata kama ana kosa kila kosa lina adhabu yake na utaratibu wake na si utashi wa polisi , apelekwe mahakamani tutajua mbivu na mbichi ukiruhusu polisi kujiamulia utakuwa umeruhusu watu kuhukumiana mtaani maana polisi nao ni binaadamu kama sisi wana wivu na hulka nyingine za kibinaadamu, unaonaje siku polisi akakukutaa na demu anayemoenda beach akaamua kukumaliza kwa kusema alikuwa jambazi sugu tumemalizana nae
 
Hahahahaha..

Sawa subiri waende polisi
 
Huwa wanawawahisha wapi????
Inavyoonekana wewe ni miongoni mwa Askari Polisi wadhalimu waliopo hapa nchini ambao kamwe hawakubaliki mahali popote pale, siyo duniani wala siyo mbinguni kotekote hawakubaliki.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tz, Uhaini ndio kosa kubwa zaidi kuliko yote hapa nchini, lakini Katiba ya Nchi na Sheria nyinginezo hazisemi kwamba Polisi wanapomkamata mtu yoyote yule anayetuhumiwa kwa kosa la Uhaini basi wanatakiwa kumuua on the spot bila kufunguliwa Mashitaka Mahakamani. Polisi hawana mamlaka hayo kisheria.
 
Na hapo ukute kashapiga watu nondo na kucharanga wenzie viwembe!
 
Niliibiwaga vitu vyote na simu 3 asee 2017,Daah haya mambo magumu ila omba yasikukute,haki itendeke
Wanakudunga na visu au bisibisi! Hawa watu tunaongea tu ila hawafai... inawezekana alivyokamatwa huko ameunganishwa kwenye kesi nyingi hivyo chain inatafutwa. Wawe wavumilivu tu....
 
Maumivu yanapozidi na tunakosa msaada...tukubaliane tu...tuanzishe genge la kimafia....litatusaidia kupunguza maumivu...Sema aameen.. 👍
 
Ni dhambi kumzania mtu bure. Unajifanya ww ni Mungu unajua kila kitu?
 
Anapatkana vipi huyu Kama anaweza kuwasaidia basi tuwape mawasiliano yake awasaidie màana hata hawajui mama na mtoto WA mwaka mmoja asubuhi watakula nini

Inauma sana mkuu
bashite ni wakuvizia kwenye mikutano yake ccm wanamficha si wanamjua anaweza akamtumbua hata waziri yule akiachwa azulule mitaani, aende ofisi za ccm kama wanaweza mpa ratiba zake za mikutano si mwenezi yule, hata pata msaada kokote amtafute bashite kijukuu cha jiwe jpm bashite atamtafutia mtu wake akiwa hai au ametolewa kafara
 
Kununua simu ya wizi mtu afuatwe saa 8 usiku pamoja na mjumbe?
Hapana.
Kuna jambo jingine.
Kama huyo mwanamke hataki kufunguka hawezi kusaidiwa hapa.
Ile michongo ya polisi wahuni wanaouza simu kisha baadaye wanakuja kwa sura nyingine kukukamata na kukutisha kuwa simu iliibwa pamoja na vitu vya milioni 5. Mara mwenye simu kafa kwa kisu wakati unampora.
Hamna hamna milioni 4, 5 inakutoka wanakuachia kiaina kesi haina hata jalada mahali popote duniani.
Wanafanya dhambi kubwa sana. Kesho wanaiuza mtandaoni keshokutwa anashikwa mwingine.
Na kesi za simu unashikwa kwa kuoigiwa simu, wanampigia mtu wako wa karibu kisha huyo mtu wanamwambia akupigie mbele yao ili wakukamate.
Hii ya usiku wa maneno pamoja na wajumbe ni ya Ujambazi au ugaidi.
 
Hata angekuwa jambazi sawa ila je hawana haki ya kumuona au kumuekea dhamana? Sheria ikoje

Mwezi mzima mtu hayupo
 
hIZI SIMU ZINASHIDA SANAA
WENGINE UNAKUTA WAMEUAAA

OLE WAKUKUTE NASIMU YA MAREHEMU

CHUNGUZAA KAMA ALIEIBIWA YUKO HAI

KAMA NDIO PONA YAKE KAMA KAFAA NDUGU NAPITATU
Majbazi wengine wakifanya tukio huwa wanapora simu ya waliowapora au kuua halafu hizo simu hutupa barabarani wakijua kuna mtu ataokota ataitumia na polisi ndie watamdaka kama jambazi na muuaji

Simu nunua dukani usinunue ya mkononi wala ya kuokota
 
Ukamataji kwa police unafanyika saa yoyote ile,kutegemeana na kosa la mtuhumiwa! Kwa hiyo kazi inabaki kwa mpimaji kosa mwenyewe!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…