Naomba msaada mume wangu amekamatwa na polisi nyumbani saa nane usiku kwa tuhuma za kununua simu ya wizi. Vituo vyote wanadai hayupo na tusimtafute

Naomba msaada mume wangu amekamatwa na polisi nyumbani saa nane usiku kwa tuhuma za kununua simu ya wizi. Vituo vyote wanadai hayupo na tusimtafute

Huwa siamin kabisa katika hii paragraph yako ya Tatu mkuu,..Serikali haitumi wauaji,yaani serikali haswa iwakusanye wewe na wewe na wewe kamanda ova kafanyeni mauaji kwa hawa raia kwa sababu hii na hii ..Mimi huwa nasikia sikia ila hili jambo halipo bhana.

Isipokuwa naamini kuna vikundi vya wahuni wenye mamlaka ama waliopewa dhamana na serikali wanafanya uhuni huo kwa faida Yao wenyewe bila serikali kujua na serikali ukitaka kuingilia kwa kuwa wao ndio njia ya kupitia wanayafumbafumba ndio màana mpaka Leo hatupati ukweli.

Ila serikali Kama serikali kutuma wauaji hapana..au mm sijui màana yaa serikal kwani serikali ni nini mkuu..serikali?kuna jamaa hapa pemben ananijibu et serikali ni sirikali pumbaf zake.

Utawala lazima uw pande mbili za shilingi. Ubaya na Wema.
Usiombe ukakutwa na utawala katika upande wa ubaya utamjua shetani live.

Hakuna utawala wenye Nuru pekee. Huo sio utawaka
 
Inawezekana huyo kijana yupo kwenye ule mtandao wa vijana wanaokwenda somalia kupata mafunzo kwahiyo nendeni kwa code
 
Inawezekana huyo kijana yupo kwenye ule mtandao wa vijana wanaokwenda somalia kupata mafunzo kwahiyo nendeni kwa code
Hapana ni kijana WA kawaida tu WA mtaani amejiajiri ni fundi simu na vifaa vya umeme na kuuza vifaa vya simu ni msakatonge tu WA kawaida na wengi wanamfahamu hana Tabia za ovyo
 
Dah! Poleni sana ndugu zangu kwa hiyo changamoto kubwa iliyowakuta. Waambie wajaribu kumtafuta huyu +255620898989.

Hana shida anaweza kuwapa mwongozo wa changamoto yao na kuwatoa wasiwasi.

Ova
Wamempgia amewaelekeza waende kituo cha polisi mburahati,wamefika wamesikilizwa na wameambiwa kwa kuwa hii ni kanda nyingine na chanika alikopelekwa ni kanda nyingine waende wakaonane na RPC
 
KUNA MTU NINGEKUPA ILA NAITAJI KUMJUA HUYO ALIYEKAMATWA YUPOJE NA KAZI YAKE NO KUFICHA
Jamaa ni mjasiriamali tu ni fundi simu na vifaa vya umeme,kuuza makava ya simu,kuweka protects,na vikorokoro vingine vya simu,ni msakatonge tu WA kawaida na hata huyo mjumbe wake anakiri ni kijana mzuri asiye na shida na yoyote hapo mtaani.
 
Kuna watu wanaandika. Makala ndefu wakati wa Magufuli watu walikuwa wanatekwa, tatizo jeshi la polisi imeoza linatakiwa lifumuluwe.
 
Kaka naomba unisaidie kunielezea matatizo yangu kwenye ule mtandao wenu wa jamii forums ulionisaodia kipindi kile, wakati huu nahitaji msaada sana

Haya ni maneno ya binti ambaye anaitwa Rahma Shaabani Kiwangala, mwenye mtoto mdogo wa takriban mwaka mmoja mkazi wa Manzese mburahati, mtaa wa kwa jongo Kata ya makurumla ambaye saa nane usiku akiwa na mume wake nyumbani walifuatwa na mjumbe wa mtaa anayeitwa Zuhura Ngwenje namba zake ni 0715328582 (yupo tayari kutoa ushirikiano) akiwa ameambatana na maaskari wawili WA kituo kikubwa cha polisi CHANIKA MWISHO ambao majina Yao ni Mussa Ally na Bonifas Gablier ambao walimkamata mume WA binti huyu anayeitwa OMAR MWELEA HUSSEIN kwa kosa la kununua simu ya wizi.

Polisi hao wawili walimchukua mpaka kituo kikuu cha polisi CHANIKA MWISHO, asubuhi ndugu wa mtuhumiwa walikuja kumuangalia ndugu Yao na kufuatilia kesi yake wakaambiwa kesi IPO kwenye upelelezi na hawakupewa ruhusa ya kumuona ndugu yao, kuanzia siku hiyo kila wakija kufuatilia wakawa wanazungushwa bila kuruhusiwa kumuona ndugu Yao,na wakati mwingine wakawa wanakuja na mjumbe wao aliyefanikisha kukamatwa kwake lakini jibu la mwisho wakajibiwa kwamba HAKUNA KESI KAMA HIYO KITUONI HAPO NA WASIENDE TENA KUFUATILIA HAPO.

Binafsi nimempgia mjumbe na amekiri kutokea kwa tukio hilo na amesikitika sana kwa sheria kupindishwa na ndugu hao kutopata haki ya kusikilizwa,kujua wapi alipo ndugu Yao na amesema ameenda kwa mkuu kulifikisha swala hilo na amewakuta maaskari hao wapo kituoni hapo na akawatambua kuwa ndio walewale walikuja kumkamata Bwana Omary lakini bado hakupewa ushirikiano wowote.

Tukio hili limetokea usiku WA tarehe 18 mwez WA pili jumamosi kuamkia jumapili saa nane usiku.mpaka Leo umetimia mwezi mmoja bila ndugu kujua lolote na wameambiwa Hakuna kesi Kama hiyo WASIENDE kufuatilia kituoni HAPO.

Tunaomba serikali ya Jamhuri ya Tanzania iwasaidie ndugu hawa kujua ukweli unaofichwa ni upi katika hili, ili iwasaidie familia hii kujua alipo ndugu Yao?

Mke wake na ndugu kwa ujumla wanasema wanahitaj tu kujua hata Kama polisi hawa wamemuuwa ndugu Yao basi waonyeshwe mwili wakazike ama wajue tu kuwa ameuwawa wazike nguo zake.

Inauma sana kwa kweli imagine ni ndugu yako ndio amefanyiwa hivyo,ndugu zangu tumsaidie huyu Bwana asiyejulikaana alipopelekwa,familia yake na mke wake kwa ujumla angalau wafaham alipopelekwa na polisi hawa

Tukumbuke Tanzania ni ya kwetu sote na sote tuna haki sawa.

Mama wasaidie wanao, kwani waliopewa mamlaka ya kusaidia ndio wamepata maguvu ya kukandamiza wenzao
Poleni sana.. Imefika JF... Taarifa zitapatikana
 
Hayo maelezo. Kuna vitu binti anaficha.

Polisi sio wajinga hawakurupuki.

Mpaka polisi wakufate nyumbani usiku wa manane maana yake wameshakujua tabia zako. Mnunuzi wa kawaida angepigiwa simu tu afike kituoni. Ndio angekamatwa..ila wa kufatwa usiku wa manane ujue ni mtu wa matukio.

Kununua simu ya wizi sio sababu kuu

Mimi nilivyoona mkazi wa mburahati na mambo ya simu ya wizi. Akili yangu inaniambia mumewe ni mwizi mtu wa matukio. Kuna maeneo dar es salaam yamejaa watu wa matukio ndio wanaishi. Mojawapo ni kigogo mburahati, tandika kwa kindande, yombo taa nyekundu, chanika. Hayo maeneo yamejaa vibaka na majambazi

Nahisi Huyo mumewe ni mwizi na polisi huwa hawawacheleweshi wezi.
sawa hata kama hivyo usemavyo ndivyo basi wamwambie mkewe kuwa mumeo ni mwizi na aliuawa au kafungwa
 
Wamempgia amewaelekeza waende kituo cha polisi mburahati,wamefika wamesikilizwa na wameambiwa kwa kuwa hii ni kanda nyingine na chanika alikopelekwa ni kanda nyingine waende wakaonane na RPC
Walipata nafasi ya kumjua huyo askari wa Mburahati aliyewapa hayo majibu? Kama walimjua (kama hawakujua siyo mbaya), warudi kupiga kwenye ile namba ili wampe hayo majibu.

Bila shaka atawaambia kingine cha kufanya, hana shida atalimaliza tu hilo, liko ndani ya uwezo wake.

Ova
 
Hayo maelezo. Kuna vitu binti anaficha.

Polisi sio wajinga hawakurupuki.

Mpaka polisi wakufate nyumbani usiku wa manane maana yake wameshakujua tabia zako. Mnunuzi wa kawaida angepigiwa simu tu afike kituoni. Ndio angekamatwa..ila wa kufatwa usiku wa manane ujue ni mtu wa matukio.

Kununua simu ya wizi sio sababu kuu

Mimi nilivyoona mkazi wa mburahati na mambo ya simu ya wizi. Akili yangu inaniambia mumewe ni mwizi mtu wa matukio. Kuna maeneo dar es salaam yamejaa watu wa matukio ndio wanaishi. Mojawapo ni kigogo mburahati, tandika kwa kindande, yombo taa nyekundu, chanika. Hayo maeneo yamejaa vibaka na majambazi

Nahisi Huyo mumewe ni mwizi na polisi huwa hawawacheleweshi wezi.
Kwanini unagenelorize kwamba watu wote wanaoish hapo ni wezi na ni vibaka
. Kwamba mtuhumiwa akikamatwa auwawe na polisi?
 
Tazara mpwa hicho kituo soo
Pale wanapelekwa manunda tu
Pale mtu akipelekwa shuguli anayo
Alafu ukipita hapo pako kimya huoni hekqheka 😄

Ova
Tulienda mtoa mtu katokea.mbwenj.yaliyomkuta napitampwaa
 
Walipata nafasi ya kumjua huyo askari wa Mburahati aliyewapa hayo majibu? Kama walimjua (kama hawakujua siyo mbaya), warudi kupiga kwenye ile namba ili wampe hayo majibu.

Bila shaka atawaambia kingine cha kufanya, hana shida atalimaliza tu hilo, liko ndani ya uwezo wake.

Ova
Asante wanamjua na wanawafahamu wahusika wote hata maaskari waliokuja kumkamata waliacha namba zao kwa mjumbe ,pia wanaonekana sehemu zao za kazi ushirikiano tu ndio imekuwa hakuna
 
Mkuu mke wake hajui kitu Bali tukio halisi liko Ivo na wao ndio wanautaka huo mwili Kama familia wakazike Kama binadam wengine wanavyozikwa kwani mambo ya kuuwawa si jambo geni.tuwaelekeze wakaufate wapi?

Kama alikuwa jambazi mwili wa jambazi ni Mali ya serikali.
Kama alinunua TU simu ya wizi bila kujua ipo siku atarudi tu.
 
Asante wanamjua na wanawafahamu wahusika wote hata maaskari waliokuja kumkamata waliacha namba zao kwa mjumbe ,pia wanaonekana sehemu zao za kazi ushirikiano tu ndio imekuwa hakuna
Kama hawatoi ushirikiano saikolojia huyo jamaa hakuwa mtu mzuri,ingekuwa TU ununuzi wa simu wasingewanyima ushirikiano.
Kama mnawatambua tafuteni wakili muwafungulie mashtaka wawape ndugu yenu
 
Wanamficha tu wangetaka kumuua wasigekuja ata na uyo mjumbe, alishawahi dakwa mdogo angu alikuwa amejichanganya tu bila kujuwa na wezi wa kutumia mapanga walifanya matukio sehemu tofauti wakaja kujifucha pale mtaani alipo dogo, sasa wakaja dakwa na askari wa oysterbay na noah walivyobebwa watu waljuwa hawa hawatorudi

Kwenda kuuliza tunaambiwa hamna vijana walioletwa tukaenda vituo vyote vikubwa. Kuna jamaa mmoja ndo alitusanua kazeni madogo wapo suspended washachokwa na wapo kituo fulani matukio yao ni makubwa sana, dogo ye hakuwa anajuwa lolote wala hawajuani nae ila tu kukutana eneo moja vijana na bangi zao na dogo alikuwa 17yr, ikapigwa simu moja pale ndo dogo kupepetwa ila alikaa mwezi alitoka kawa kama moja sidhani kama atasahau iki kitu maishani mwake wale wezi nafikiri walipelekwa mahakamani kula robari
 
Daah pole sana kwa huyo dada na familia.

Kuna moja kama hiyo manzi yake na mshikaji wangu alishikwa na simu ya wizi, mbaya aliyeibiwa alipigwa napanga na wezi mpaka kufa.

Oyaaa hadi Cheni nzima inapatikana yule manzi alisota sana, na majibu ya kituo kikubwa cha huku kwetu majibu yalikuwa kama hayo yako mtoa mada kwamba kesi haipo, ila upelelezi unaendelea kwani alieuwa ni kama mtu wa saba au sita na aliyezuiwa simu (tulijua baada ya mnyororo mzima wa kuuziana simu ulipopatikana).
Sishauri sana mtu kununua simu mkononi hasa hizi simu janja labda kwa mtu unayemjua na una uhakika amenunua dukani.
 
Hayo maelezo. Kuna vitu binti anaficha.

Polisi sio wajinga hawakurupuki.

Mpaka polisi wakufate nyumbani usiku wa manane maana yake wameshakujua tabia zako. Mnunuzi wa kawaida angepigiwa simu tu afike kituoni. Ndio angekamatwa..ila wa kufatwa usiku wa manane ujue ni mtu wa matukio.

Kununua simu ya wizi sio sababu kuu

Mimi nilivyoona mkazi wa mburahati na mambo ya simu ya wizi. Akili yangu inaniambia mumewe ni mwizi mtu wa matukio. Kuna maeneo dar es salaam yamejaa watu wa matukio ndio wanaishi. Mojawapo ni kigogo mburahati, tandika kwa kindande, yombo taa nyekundu, chanika. Hayo maeneo yamejaa vibaka na majambazi

Nahisi Huyo mumewe ni mwizi na polisi huwa hawawacheleweshi wezi.
Taratibu za kumkamata mtu ziko wazi,mpaka kumfikisha mahakamani na ikithibitika kuna makosa basi gereza litamhusu,ila wewe umeandika kwa kukariri kuwa maeneo fulani yana tabia za hivyo,
Angekua ni nduguyo mwizi na usiyejua kama ni mwizi anaishi maeneo hayo na ndie aliyefanyiwa hivyo pengine ungekuja na stori inayofanana na ya huyo dada.
Tusiandike kwa mihemko

Pole sana kwa huyo dada,
Aende kuonana na yeyote katika kamati ya ulinzi na usalama mkoa,
Ikishindikana atumie vyombo vya habari mpaka watakaposema mumewe alipo
 
Back
Top Bottom