Polisi kuna mfumo wameuanzisha sina hakika kama ni rasmi au sio rasmi, ni kuwa wakimkamata mtuhumiwa wa wizi wanamlazisha ataje na matukio ya wizi alioyafanya kwa muda fulani labda miezi mitatu nyuma au sita kulingana na wanavvyohitaji.
Na kila anapoataja tukio wanakusanywa wahusika wote kuanzia wezi, madalali na wanunuzi, na pia wanaenda hadi kulipofanyika tukio ili kuwapa taarifa na wafuatilie kesi yao.
Katika kipindi hiki wahalifu wote wanawazuia kuwaona na ndugu nadhani wanahofia labda ndugu wakikkutana na wahalifu wanaweza kuharibu upelelezi.
Hivyo ukienda kituoni utaambiwa eidha ndugu yenu hayupo hapa au kesi hii haipo, ukiuliza yupo wapi watasema hawajui.
Kuna rafiki yangu alinunua TV ya wizi ndio alionipa ushuhuda huu, kuhusu mateso aliniambia wanateswa wezi tu ili kutaja zaidi matukio nyie madalali na wanunuzi mnatishwa tu kama ulishawahi kununua mali nyingine ya wizi ukiacha hiyo.
Nilivyoona huyo jamaa aliekamatwa alikuwa fundi simu hisia zangu zinaniambia labda alinunua simu ya wizi ambapo kuna matukio mengine makubwa wamefanya hao wezi waliouza hiyo simu ndio wapo kwenye huo mfumo nilioutaja.
Maana kazi ya ufundi simu na kuuza simu za wizi ni vitu vinavyoendana sana japo sio wote ila wengi wao, simu nyingi zikiibiwa zinapitia kwa mafundi kwa ajlii ya kutoa lock, kuchange IMEI NO. na mambo mengine ambayo wezi hawayajui.
Kwa vile hizo huduma zina gharama na mwizi ana shida ya haraka ya pesa anaona bora amuuzie simu fundi simu yeye asepe zake.
Ushauri wangu, huyo mke wa jamaa aende kwa OCD amuelezee hiyo shida yake anawweza kupata msaada, nina uhakika wa 90% kuwa jamaa bado yupo hai ila tu hayupo sehemu salama.