Naomba mwenye akili timamu anieleweshwe nielewe vizuri the logic behind ya kutoshiriki uchaguzi.
Je CHADEMA expectations zao ni zipi?
Yaani wata achieve kitu gani kwa wao kususia uchaguzi?
'
Wewe mwana CCM una ndugu wa kwenda kuuwawa wakati wa uchaguzi au unasubiri wale wa chadema wauawe kila uchaguzi ukifika na hawashindi .?
Una ndugu wa kwenda kupigwa mabomu na kuvunjwa miguu ?
Nendeni na huyo mungu Samia labda ataishi nilele na kuwapa uzima wa milele na nyie .
Mafwere yupo na amepandishwa cheo ,Awadhi yupo na anategea kuwa IGP Samia akishinda uchaguzi, Wambura mwenye historia ya kutisha yupo , Kingai ,Yupo, Mulilo yupo .
Makonda yupo Arusha ya Chadema na alishaambiwa amepelekwa kwa kazi maalumu na kupewa pesa za kufanya anachotaka .
CCM nendeni peke yenu ili mpate msipate mpinzani wa kumsema mama bungeni .
Hofu ya nini ?
Mafisadi siku zote hofu yao ni umoja wa watu maskini .
Hicho chama ni kwa sababu bado kina itikadi za kibepari lakini kinauwezo wa kukusanya pesa nyingi na hata kuwaajiri wenyeviti wote nchini na kuwalipa mishahara.
Umoja ni nguvu kubwa sana.
Tatizo mabebebru wamewajaza watu ubinafsi wakati wao wanatumia nguvu za maskini kutajirika .
Bado Chadema hakijawajia mamluki ndani ya chama lakini kinauwezo wa kukusanya kila mwezi bil.1 na zaidi .Ruzuku ya serikali ni danganya toto ya kupandikiza watu .
Angalia jinsi Bakwata na KKKT wanavyodhibitiwa na Serikali kwa sababu ya pesa toka serikalini .
Watu wanapinga foleni wanataka wapewe tiketi ya kwenda hija. Wanapewa na mkuu wa nchi watampnga vipi ?
Miradi ya kanisa wanataka wapewe msamaha wa kodi na Ruzuku watapinga vipi uovu wa serikali .
Chadema nje ya Ruzuku watajijengea heshima kubwa na kukifanya chama kuwa cha umma.
Miaka mitano itaiua CCM kabisa kabisa maana watakua hawana cha kujitetea 2030 . Vijana wataongezeka na wazee wa CCM watakua wamechoka sana .
Tatizo la ajira litakua ni kubwa sana . Kwa sababu awamu hii haina mradi mpya wala Wazo jipya zaidi ya kuwaza uchaguzi na kutumia gharama kubwa sana matokeo yake Uchaguzi hauna mpinzani mwenye nguvu . Aibu kubwa . Mabango nchi nzima na pikipiki nchi nzima halafu hakuna chama chenye nguvu ya kushindana na dola .