Naomba tafsiri ya ndoto ya kuachwa na ndege kisa kusahau passport

Hatutakiwi kusema ndoto hazina maana kabisa na tuzipuuze, kwa sababu ndoto ni aina fulani ya mawazo, ni mawazo yanayoturudia tukiwa tumelala. Kuna mawazo mengine kuja wakati tyko macho ni vigumu, tukilala ni rahisi.

Lakini hilo pia halimaanishi tuzipe ndoto umuhimu wa juu sana kama njia ya kuona yake yasiyooneakana, kutabiri yajayo etc.

Hakuna wakati ambapo utaota mambo ambayo hukuwahi kuyawazia kabisa, hata mtu ambaye hujamfikiria muda nrefu, ushawahi kumfikiria, hata ukiota kitu abstract, ushawahi kuwa na hilo wazo abstract.

Ndiyo maana ni vigumu mtu kuota yupo katika dunia ya science fiction ya string theory yenye dimensions 10 za space, hizo dimensions 10 za space hata kuzifikiria hawezi, ndiyo maana hawezi kuziota.
 
Yes nimesali na kufunga cz nilipata kiu ya kujua zaidi
Mana nilitamani kuota nielewe zaidi maisha/changamoto yangu
Mmenipa mwanga inatia moyo

Naaamini ndoto zinazoeleweka kama hii zingine napotezea,
 
Jaribuni kua na koromeo sio kila kitu cha kupost humu kwaio na abiria wa boda akiota kakimbiwa na boda wake aje kupost?

Ndoto tu hizo zinatokana na pirika zako hmna jipya
Ukiota umelewa chakari wakati we sio mnywaji hutajiuliza.?
 
Labda useme tunaota vitu na mazingira tunayoyajua ila sio kusema kwamba ndoto ni mambo tunayoyawaza.

Kwanini unaona hatupaswi kuzipa ndoto umuhimu sana? Ni kwamba hazina huo umuhimu au ni vp?

Inasemekana Abraham lincoln aliyewahi kuwa rais wa Marekani aliota ndoto siku kadhaa ya kabla ya hajafanyiwa assasination, na ndoto yenyewe aliona rais kafa. Lakini pia kuna documents zenye kueleza experience walizopata baadhi ya watu kupitia hunches na dreams kabla ya kutokea kwa kuzama meli ya Titanic, hata september 11 pia ni ilitokea hivyo.
 
Watumishi husema hivi ukiota ndoto ikakupa mashaka,, iandike ilinusisahau Kisha omba Toba huenda kina.mlango upo wazi shetani kapitisha hapo mambo yake, baada ya mwambie MUNGU akupe tafsiri yake au airudishe upya lakina fanya maombi yanguvu usipuuzie.

Hapa ni mie mambo yako ya kitaifa utapoteza , usipuuze.
 
Kwa nini unataka kutenganisha mazingira tunayoyajua na mawazo tunayoyawaza? Mawazo tunayoyawaza yanatokana na mazingira tunayoyajua, hatuwezi kuwaza mawazo ambayo hayatoki kwenye mazingira tunayoyajua.

Mfano wako wa Abraham Lincoln ni mzuri sana. Mimi napenda kusoma. Hapa nasoma vitabu viwili. Nasoma kitabu kipya cha Abdulrazak Gurnah "Theft" kilichotoka jana. Lakini pia nasoma kitabu cha Jon Meacham, mwanahistoria maarufu wa Kimarekani. Mshindi wa nishani ya Pulitzer. Kitabu kinaitwa "And There Was Light : Abraham Lincoln And The American Struggle".

Lincoln alikuwa anaishi katika vitisho vya kuuawa muda wowote. Huyu ni rais wa wakati wa vita aliyeongoza majeshi ya Kaskazini mwa Marekani walivyopigana na majimbo ya Kusini katika Civil War. Alitishiwa sana kuuawa akakubali kuwa akifa ni sawa tu.

Kifo cha kuuawa kilikuwa kwenye mawazo yake muda wote. In fact February 23 1861 walinzi wa Lincoln waligundua mpango wa kumuua wakaepusha mauaji hayo.

Sas mtu mwenye mawazo ya kuuawa hivyo ni ajabu gani akiota anauawa hata kila wiki?
 
Nakupa ushuhuda mara moja!

Kuna Ndugu yangu yeye ni Auditor! Alikua ananisimulia mwaka Jana kuwa; TRUE STORY

Aliota ndoto Yupo Airport anasubiri ndege Sasa kuna dada mmoja anafanya nae kazi ofisi moja(Naijua ofisi yao maana huwa naenda naenda) Alikua anamsubiria ili wasafiri Pamoja!

Sasa Muda ukawa unaenda yule dada anachelewa kufika pale Airport na muda wa ndege kuondoka umefika Kila akijaribu kumpigia simu yule dada anamwambia nipo njiani.

Jamaa mwisho akasema mimi naondoka mwenyewe namwacha. Akaenda akapanda ndege mwenyewe akaondoka!

Nataka nikuambie jamaa akawa ananishuhudia kuwa haikupita WIKI akapokea barua ya Kupandishwa cheo na Kuongezewa mshahara ofisini!

Siku alipopokea hiyo promotion akamfata yule dada akamsimulia ndoto hiyo pia kuwa alitaka kumcheleweshea mambo mazuri!

Ndoto Ndugu zanguni ni Halisi ni Taarifa katika ulimwengu wa Kiroho japo zingine huwa zinakuja kimafumbo mafumbo kwahiyo ni juhudi yako kutafsiri na kujua zina maana gani.!
 
Au siyo.

Ngoja niishie hapa tu.
 
Hii ndoto yako inafanana na ndoto ambayo mimi huwa naota mara kwa mara.. Ninakuwa nimeenda mahali ninaporudi siwezi kuikuta gari yangu au nakuwa natafuta au sikumbuki wapi niliacha gari langu ..


Nilipofuatilia juu ya maana ya ndoto hii nikafafanuliwa ni kuacha njia au kukata tamaa ndani ya jambo ninalolifanya ... Na hii inanitokea mara kwa mara, nafungua biashara lakini ile biashara haifiki mwisho inashindakana nafungua nyingine..

Sasa tafsiri ya ndoto yako, inaonekana umekwama kati kati au kupoteza mlengo katika jambo ulilokuwa unafanya ... Kuna vizuizi aina mbalimbali visivyooneka , vinakukwamisha kwenye maisha yako... Kwani kwa kutegemea akili zako, inaonekana uko vizuri na mambo yako huwa yanaenda vizuri tu bila shida ...

Maana nyingine, basi ni tunaonyeshwa tusitegemee akili zetu au ufahamu wetu kwa mambo yetu , kwani vitu vyote ambavyo huwa vinakusaidia vilikwama...


Chunguza ni jambo gani kubwa au maamuzi gani makubwa unataka kufanya , na pengine kuna ujumbe unafikishiwa ...

Asante mimi ndivyo nilivyoona kwa ufahamu wa kawaida ...
 
Kuna mahali unatembea katika njia isiyofaa umeacha kumtegemea Mungu umeacha kutenda mena mambo yako yataanz kukuharibikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…