Naomba tafsiri ya ndoto ya kuachwa na ndege kisa kusahau passport

Kusema kwamba mawazo yetu tu tunayoyawaza ndio hufanya kuota ndoto katika kutaka kuonyesha kwamba ndoto hazina maana ni mawazo tu, hoja hiyo ndio mimi naipinga kwa sababu hata kama mtu kaota jambo ambalo ni katika mambo anayoyawaza bado huwezi kusema kuwa hiyo ndoto haina maana hasa ukiangalia mfano wa Elias Howe unaonyesha ameota ndoto katika mambo aliyokuwa akiyawaza ila kupitia hiyo ndoto imekuwa msaada wa kutatua jambo lililokuwa likimtatiza.
 
Kuna ndoto huwa natulia/napotezea,

Hii nilivyoamka imenitatiza sana rohoni
Nikasali, imeniliza na sijui kwa nini
Umeshasema una OCD. That explains a lot juu ya ndoto yako.
Ni kwamba wewe king'ang'anizi hadi kitu kinakuwa hard coded kwenye brain. Unaota kitu inayosumbua ubongo wako.
Hiyo ndoto haina maana yeyote.
 
Nina changamoto ya mahusiano ila ndoto ni safari ya kikazi
Ndio maana nilikwambia ndoto hutumia metaphor hivyo unaweza kuona ndoto inaelezea masuala ya kikazi ila hiyo ikawa ni metaphor tu, moja ya ugumu wa kutafsiri ndoto ni kujua hiyo ndoto itakuwa inahusu upande gani kwenye maisha yako. Ila uzuri wewe umesema ulikuwa ukimuomba Mungu akueleweshe sehemu ulipo kimaisha hivyo mpaka hapo unajua ndoto imegusia jambo.
 
Mbona hapo juu nimesema si kweli kwamba ndoto hazina maana kabisa, kwa sababu, hata kama zinatokana na mawazo yetu tu, kuna mawazo fulani yanaingia katika subconcious mind. Hilo linaweza kutusaidia kujua, kwa mfano, what are we anxious about. Kwa hiyo ndoto zinaweza kusaidia kujua na kutibu anxiety.

Kwa hivyo sijasema ndoto hazina maana kabisa.

Nilichosema ni kwamba, kwamba ndoto zinapewa umuhinu ambao hazina na tafsiri za uongo na hizi habari kwamba ndoto zinatabiri yajayo, zinatuonesha vitu vya mbali etc, hizi ziko largely exaggerated.
 
Hiyo ndoto hakupitia terminal 3 document check? Pole hebu Ona maana hii harafu husianisha na maisha yako kwa mtiririko wa miez 3 nyuma. Ipo hvi
Kuota ndoto ya kuachwa na ndege kwa sababu umesahau passport kunaweza kuwa na maana ya kushindwa kufikia malengo yako au kukosa fursa muhimu maishani. Katika tafsiri ya ndoto za kisaikolojia, passport inawakilisha vibali, haki, au uwezo wa kusafiri, kufikia au kufanikiwa katika mabadiliko fulani ya maisha. Kusahau passport kunaweza kuashiria hofu ya kutokuwa tayari au kupoteza fursa muhimu, pengine kutokana na kukosa maandalizi au kuwa na wasiwasi.

Pia, ndoto kama hii inaweza kuonyesha hali ya kutokuwa na uhakika au kujisikia umeachwa nyuma au kupuuziliwa mbali kutokana na vikwazo au changamoto zinazokuzunguka.

Hata hivyo, tafsiri za ndoto ni za kibinafsi na zinaweza kutofautiana kulingana na muktadha wa maisha yako. Kujitahidi kuwa na uhakika na maandalizi katika hatua zako za maisha kunaweza kuwa na manufaa.
 
Kwahiyo kwa mfano nikikuuliza ni benefits zipi tunazipata endapo tuki pay attention ndoto zetu?

Na unajuaje kuwa ndoto hazina umuhimu huo unaopewa? Nakubali kwamba kuna tafsiri ambazo si sahihi na kuna mtazamo wa watu wengi kuhusisha sana ndoto na utabiri wa mambo yajayo kitu ambacho naona si sahihi, ila nachofahamu si rahisi kuweza kujua ama kutafsiri ndoto inayohusu tukio lijalo mara nyingi baada ya kutokea hilo tukio ndio mtu anaweza kujua tafsiri ya ndoto aliyoota ambayo ilihusu hilo tukio.
 
Kuna ndoto ni matokeo ya mtu kufikiri kitu tu, sasa ntu atataka kusumbuka sana kutafuta tafsiri, ndoto ina maana gani, unnecessarily.

Mtu kaota amechelewa kupanda ndege, kwa sababu ni mtu wa kufikiria safari sana na anataka awe tayari nuda wote, au kaona movie ya safari, sasa hapo atataka kujua ike ndoto maana yake nini, inatabiri ni i, ina maana gani.

Unnecessary anxiety.
 
Hicho ndio ambacho mimi nakipinga, hata kama mtu anawaza sana jambo fulani ila kuota kwake hilo jambo inaweza ikawa kuna maana kwenye hiyo ndoto hivyo si sahihi kuchukulia kwamba kuota ndoto ya mambo tunayoyawaza sana kuwa hizo ndoto ni mawazo tu kwamba imetokea kwa sababu ya kuwaza sana ila haina maana. Vp ikiwa hiyo ndoto ina msaada au ndani yake kuna jibu fulani katika hicho unachokiwaza sana? Huu mtazamo wa kwamba ni mawazo ndio maana pale mtu akiota mtu au kitu ambacho hakuwa akikiwaza anaanza kujiuliza kwanini ameota hicho kitu au huyo mtu.

Ila nakubali kwamba si kila ndoto inahitaji tafsiri, zipo ndoto haziitaji kutafsiriwa ila lakini zikawa na sababu nzuri tu inayofanya uote.
 
Kwanza unaelewa kuwa hatuelewi vizuri mambo yote tunayowaza, kwamba kuna levels nyingi za kuwaza na mawazo hayo hayaji manifest kwa namna moja yote, mengine yapo wazi sana, mengine hayapo wazi sana, mengine yapo kwenye subconscious level, na mengine ndiyo hayo yanajiweka katika ndoto, yote ni mawazo.

Unakubali hilo?
 
Umeshasema una OCD. That explains a lot juu ya ndoto yako.
Ni kwamba wewe king'ang'anizi hadi kitu kinakuwa hard coded kwenye brain. Unaota kitu inayosumbua ubongo wako.
Hiyo ndoto haina maana yeyote.
Si tulikubaliana huu mwaka wa kufosi😃au?,
 
Tafsiri ya hiyo ndoto ni kwamba kuna soku utapaa na ungo na kuingia rasmi kwenye uchawi Mkuu
 
Good analysis
Katika safari nimekosa kibali na juhudi za kutafuta kibali zimekwama
Dahh my Jesus help me Lord🙌🏽🤲🏽🙏🏽
 
Be careful cause no body give a sh**t about you . Your surrounded with wrong dudes so choose wisely
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…