Naomba tuongee UHALISIA kuhusu biashara ya Real Estate kutumia mfano HAI

Sijui kwa nn Bank hazijaona hii fursa.
 
Sijui tuwaambie mara ngapi kwamba hii ni biashara kichaa. Unless uwe unaitumia kama security au hizo hela umeziiba ila kama ndio biashara ya kukufanya ufanikiwe my friend hapo umefeli tiyari.

Uliwahi ona mtu kajenga nyumba ikazalisha hela ya kujenga nyumba nyingine ndani ya miaka kumi? Sasa tafuta biashara kama spare parts, electronics, vyakula, retail stores uone nyingine ndani ya miaka mitano inazaa biashara nyingine kama hiyo. Wewe hapo unataka umiliki nyumba nyingi kwa kutumia nyumba hiyohiyo nakuhakikishia utasubiri mpaka miguu iingie tumboni.

Yani bora umiliki bodaboda nyingi nitakuelewa kuliko kumiliki nyumba. Bodaboda inataka kitu kimoja tu, ROHO NGUMU basi. Nyumba ina forces ambazo ni gharama kuzipa control na return yake ndogo.

Yani hata ufanye nini, hutokaa uwe tajiri wa kwanza wa real estate hapa Bongo. Tunao matajiri wa mabasi, madini, mazao, kilimo, usafirishaji, n.k. Tajiri specifically wa biashara za nyumba ni nani hata mmoja tu? Kwanini asiwepo, ni kwa sababu biashara hiyo hailipi wala sio kuwa watu hawaoni fursa
 
Kama eneo ni zuri na nyumba ni ya kisasa,kama ulivyosema ni vyumba viwili ulitakiwa upate 450,000/- kwa mwezi...

Kama kiwanja unacho tayari hiyo 450,000/- unaweza kuanza ujenzi kidogo kidogo tena isiwe nyumba kubwa iwe tu chumba na choo chake na jiko dogo ndio nyumba zinazopata wapangaji kwa haraka...

Hakikisha hiyo kodi sio ya matumizi yako ya kilasiku haitoweza kukuzalishia nyumba nyingine..

kama huna kiwanja napo ni changamoto ,maana itabidi u save ununue kiwanja uanze kujenga ni mlolongo...
 

Mbona kama umeongea kwa hasira sana mkuu shida nini? Kama boda boda inahitaji roho ngumu kwanini isiwe nyumba? Je biashara haikosi kua na changamoto na changamoto hizo uzitafutie ufumbuzi...Halafu pia tuulizane biashara unafanya ili uwe tajiri tu? Na kama kweli hailipi, kwanini kuna kampuni kubwa za real estate afrika zinazofanya vizuri, je wao waliamka asubuhi wakajenga magorofa na apartments? Tunaona project kubwa kubwa za nyumba sehem mbalimbali kama ni mfuatiliaji, je wao kwanini wanafanya kitu ambacho hakilipi?
 

Unadhani good investment of the life ilipaswa kua nini bosi kwa milioni 70...

Ingekua mimi mtu amekuja kwangu anaomba ushauri on present situation kwamba nina hiki, nitafanyaje niongeze kingine kwa kutumia nilichonacho, au kubadilisha kuongeza kingine, ningelimshauri kulingana na alichonacho, na sio kuanza kumlalamikia kwamba alichofanya hakikua sawa.
 
Na asset inaongezeka thamani.
 
Wazo zuri...Mimi kwenye hizo ngazi ulizoweka naangukia kwenye hilo kundi la wadogo.
USHAURI:
*Kwa kuanza lazima uwe na shughuli nyingine sambamba hadi hapo utakapoimarika..Fedha inayopatikana hapa kiuchumi inaitwa passive income..inapatikana kidogo kidogo.
  • Hujasema uko wapi lakini nakushauri ujenge kwa kuzingatia mtindo wa maisha ya sasa..watu hawakai na familia kubwa kwa muda mrefu..watoto wanasoma shule za bweni hivyo vyumba viwili na ukumbi tosha sana.
  • Angalia Mji uliopo kwa mfano Dodoma wafanyakazi wengi wako bado na familia zao Dar na maeneo mengine .hivyo rudia ujenzi niliokueleza hapo juu..vyumba viwili toshaa kwa maana ukubwa wa familia ni mdogo.
  • Watu hawataki shida ya kuchangia vitu .hivyo ingia gharama za kila mpangaji kujitegemea kwenye huduma za maji,umeme nk
*Kuwa mbunifu kwenye ujenzi wa majengo yako na eneo ulilokuwa nalo..acha kujenga vyumba vikuubwa ambavyo vitakuchua eneo kubwa.
* Kuwa na mpango mzuri wa ujenzi .mfano eneo lako linatosha kujenga majengo manne..Anza kwanza na moja likamilishe hadi liishe na lianze kutoa huduma halafu fedha kidogo utakazokuwa unapata endelezea ujenzi wa sehemu inayofuatia .hapa wapo ambao wanaanzisha ujenzi wa majengo yote kwenye eneo na kuishia njiani kwa Fedha kwisha.
*Hakikisha eneo linakuwa na faragha na usalama kwa kujenga uzio ..
Kwa Leo hayo yanatosha kwa kuanzia.
Land Lord.
 

Kwani yafaa jamii forum kuuliza maswali yapi yanayotakiwa kuulizwa?

Anyway japo umeruka ruka, kama msomi unatakiwa kujibu kulingana na ulichoulizwa na sio kukejeli kwamba nimeuliza swali lisilopaswa kuulizwa, mtu anakuja kwako anakuuliza nina duka la mpesa tigo pesa , napata kamisheni ya laki 2 na 50 kwa mwezi, anaomba ushauri atainukaje kwenda juu zaidi kuongeza mradi au miradi mingine, unamwambia "tafuta fedha kwa kufanya kazi kwa bidii ukiwa na nidhamu ya matumizi na mipango thabiti" uhalisia hapa upo wapi? Mbona ni kama maneno ya wale motivation speakers?
 
hii pia ni kichaa kuandika ni rahisi lakini kwenye uhalisia ni tofauti labda uwe dereva mwenyewe ukiwapa madereva wakuletee hesabu utajuta

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Na asset inaongezeka thamani.
Inflation inaongezeka kwahiyo hiyo future value ya asset sio halisi sana. Bado nyumba inafanyiwa ukarabati kila baada ya miaka kadhaa ili iende na wakati na kuvutia wateja, bado ukarabati kutokana na kupasua mabomba, vyoo kuziba, kuvuja (assumptions tu ila ni vizuri utarajie worst case scenarios). Na kuna muda mpangaji atatoka kisha ukose wa kuishi immediately
 

Bado hujanijibu swali langu, kwamba kama ni biashara isiyokua na faida yoyote , project kubwa na makampun ya real estate yapo na yanafanya kazi kwa saababu gani? Sina haja ya kutaja kampuni mana ziko nyingi, na usianglie tanzania tu , panua akili pia angalia afrika huko ..

Shida moja ya sisi watanzania tunapenda kua wajuaji sana na pia wengi wetu tuna selfish attitude, nikiwa na milioni 20, nikitaka kufanya biashara ya kuuza viatu, utani crush na kutaka nifanye biashara unayotaka wewe, nisipofanya unayotaka wewe unatoa conclusion kwamba biashara uliyochagua kufanya haina faida yoyote, kwanini kama msomi unayejielewa, mtu huyo unamuambia sasa sababu biashara umeifanya au kuianza na inakuletea kias hiki kwa muda huu, sasa unatakiwa ufanye moja mbili tatu nne tano, either uongeze biashara kama hio au kubadilisha, lakin sisi baadhi ya watanzania utasikia aaah wewe unafanya biashara kichaa, wewe umepotea, wewe this, wewe that, !!
 

Asante mkuu, atleast wewe umeweza kunielezea kulingana na kilichopo mezani. Haswa point ya kwanza inayosema kuwepo na shuhuli nyingine hadi hapo kuimarika kutakapokuwepo..
 
Kwani ndugu ukiwa unafanya kazi au kustaafu huwezi fanya biashara na ukawa na malengo ya kuongeza miradi mingine zaidi , nadhan ni tanzania tu wastaafu wanaonekana ni.kama.watu ambao hawajui biashara au kuna mentality kwamba wanafanya biashara ili waishi tu na kupata hela ya kula tu, na sio ndoto za kujenga empire kubwa kibiashara
 

Nakushukuru mkuu kwa mchanganuo wako, fikiria hela hio ingeisha yote kwa kufanya ufuska, au kuifanyia starehe pombe na wanawake, yote ikaisha,,nadhan ningekua nimeshaoga matusi mengi hadi sasa, lakin sio kwamba cash haipo, ipo lakiin sasa iko katika mfumo wa nyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…