Naomba tuongee UHALISIA kuhusu biashara ya Real Estate kutumia mfano HAI

Anza tu kidogo kidogo..jiwekee mpango mzuri..ukianza kila kitu kinakuwa rahisi..jiwekee kuanza kuona kile ulichoweka kuanzia miaka mitano angalau.
Asante mkuu, ila nikuulize mkuu je kuna hasara kua na asset?
 

Thank you for this, atmost nimeelewa natakiwa nianzie wapi na kuishia wapi na kipi nirekebishe
 
Kama anapata kodi nzuri inawezekana kabisa

Mimi hapa ndio plan yangu na nimeshajenga na ina wapangaji tayaru yote na mwaka huu nakula kwanza kodi kidogo

Mwakani naanza rooms zangu hapo hapo za self eneo ambalo zinaweza toka rooms 7 bei ya chini ni 90k per room.

Na zitajengwa kwa mixing ya ile ya kwanza na salary yangu
 
Infact katumia hela sana kwa ukubwa wa hio nyumba
 
Real estate inafanywa na MAKAMPUNI makubwa Mkuu au yakati.

Iweke Nyumba ya vizuri.
Anya Nyumba yako iwe Kwa ajili ya Waswahili au wageni kutoka nje!
Hapo ndipo biashara ilipo.

Waswahili hawana hela hiyo uweke akili ingawaje ndio wengi. Pesa zao ni pesa madafu.

Kama solo lako ni wageni kutoka nje tafuta MAKAMPUNI ya utalii uingie nayo mkataba, au MAKAMPUNI ya Real estate kubaliana nayo, alafu waachie hiyo kazi wao.
Wewe wekeana nao bei Kwa kadiri watakavyoiona Nyumba yako, kazi ya kutafuta wateja na kuendesha biashara waachie wao wenyewe.

Wewe chukua pesa yako kila baada ya mwaka au miaka.

Ukifanya mwenyewe utafanya Kwa waswahili watakaokusumbua Kodi na bado wataiharibu Nyumba yako
 
To the best of my knowledge real estate inafanywa na watu walio na exess au surplus income , these can range from big corporates toddies to drug dealers

Nyumba ya kupata 450000 kwa mwezi ni nyumba ya thamani karibu 70 plus millions au zaidi. Hakuna biashara unaweza kuifanya kwa mtaji mkubwa halafu utegemee faida kiduchu na ku survive
 
Ungesema nyumba ilipo atleast ungeshauriwa kulingana na uhalisia wa jambo husika.
 
Hauna knowledge na hii biashara ndio maana unaona ni upuuzi

Kabla hujajenga nyumba kwa hii investment lazima ufanye research

Sasa mleta mada alijijengea tu.

Alijenga nyumbs ya milioni 70 mbezi beach na aliejenga kwa gharama hizo kule mbagala maji matitu hawawezi lingana kwenye returns

So mleta sijui kama alifanya calculation kabla hajaanza ujengi au ndio anaanzs sasa piga hesabu.

Real estate sio lazima uwe kampuni au drug dealer ndio uingie maans kuna kampuni kibao wana flop market inawaacha nje sababu hasakupiga hesabu zao vizuri.

Angali tu tale magorofa marefu dar pale mengi yako empty vumbi limejaa hakuja wateja serikali imekimbilia dodoma.

so hii kitu nachopendea mimi ni generational wealtg utskula wewe ns vizazi vyako.

Na jua kuwa thamani ya nyumba viwanja inapanda daily.

2004 kuna mzee mmoja alinunua eneo la hekari 4 hivi goba kwa milioni 5 tu wakati goba pori hakuna nyumba wals barabara

Lakini leo lile eneo lake akitaka kuuza hakosi 200+ m maans pakubwa sana

Tatizo mnataka faida za fasta fasta kafungue biashsra some upate faida ya Milioni moja siku ukifa na biashara hufa.

Wekezeni kwenye sure investment.
 
Kama utafanikiwa kuuza kwa 70; tafuta viwanja 5 @3,000,000=15,000,000/=; Jenga viwanja 3@18,000,000= 54,0000,000; Jenga kwa awamu awamu; Lot: chumba na sebule na choo ndani; malengo kiwanja kiwe na lot 4, ila utaanza kwa lot moja moja kwanza
Sasa kiwanja kinachopatikana kwa 3m kama ni Dar si anapata bagamoyo hiyo au kisarawe ndani ndani au karibu na mkuranga huko?? Sasa akijenga nyumba huko kodi si itakuwa 50k kwa mwezi na pengine pia asipate mtu wa kumpangisha. Elewa kwamba watu wanapenda kupanga karibu na mjini ambapo kwa mawazo yako kama unataka anunue kiwanja...ni bei kubwa.
 
Nyumba ya 70 milkions mbezi beach inakaa kwenye kiwanja cha hela ngapi?
 
Asante mkuu kuna mambo nimeypata toka kwako
 

Dah asante mkuu, atmost nawe pia kuna kitu umeniongezea, haswa hapo kutafuta makampuni ya utalii na kuingia nayo agreement, nilikua sijaliwaza hili sababu nina marafiki wengi wako kampun za utalii na wengine ni wamiliki.
 
Nmekuelewa mkuu
 
Yaani utumie mtaji wa milioni 70 kwa kuingiza laki na nusu kwa mwezi!?seriously hivi kichwa umepewa ili unyoe kiduku tu ama ufikirie vizuri?
 
Yaani utumie mtaji wa milioni 70 kwa kuingiza laki na nusu kwa mwezi!?seriously hivi kichwa umepewa ili unyoe kiduku tu ama ufikirie vizuri?
Ati kisa security!
Nilifatilia sana hii biashara ya real estate , in a nut shell inaonekana biashara nzuri na yenye ulinzi wa pesa , ila kiukweli wengi wanaofanya hii biashara hawana uhalisia wowote wa pesa waliyoingiza kwenye uje zi na mapato wanayopata ,
Kuna dots nyingi sana na haziconnect, utaiskia tu fulani ana appartmet dola 2000 kwa mwezi masaki ! Ukiuliza unakuta property ina thamani ya dola laki kadhaa
 
ceteris paribus

#MaendeleoHayanaChama
 
Mimi nimejenga nyumba bila hata kupiga hesabu,nina nyumba ina sebule tu kubwa,vyumba viwili kimoja master,jiko,public toilet..na veranda mbili.

Means gharama itakuwa imefikia huko kwenye mil 70.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…