Naomba tuungane kuanzisha Vitabu vya Dini ya Waafrika

Sema siyo jambo dogo kwako wachina,wahindi,wakorea,warusi,wahindink waliwezaje?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kasome historia ujue kuwa haya unayoyaona ni matokeo ya mchakato wa miaka mingi hata kabla YESU (as) wala Muhammad (saw) wala Ibrahimu (as) (inakadiriwa) hawajazaliwa
We kaa pembeni Waafrika tufufue dini zetu kwani wewe ni mzungu au mwarabu na dini yako.
Na waafrika kwa zama hizi? Uanzishe dini leo? Utamchagua mungu gani? Tanzania pekee tuna zaidi ya makabila 140 na kila moja lina mungu wake

Sikwambii kuhusu AFRIKA sasa

Kijana kabla hujalivamia hili swala hebu vuta karatasi na usome utulize kichwa kabisa
 
Kuna mtu nilimpa hili wazo tena msomi, kasema mimi ni mshamba kwa kuwa nataka nirudi kwenye mambo ya zamani. Eti wao wanaenda na wakati kwa kutumia huu utamadumi wa kizungu. Nilimuambia tu kwa upole kuwa "aliyedharau utamadumi wake ndio mshamba".
 
Hakuna ulipostudy sema umefundishwa na wazungu na wazazi wako maisha ya wazungu na hujawahi kutafakari iwapo wazungu au warabu walikuwa sahihi kwa wao kueneza dini zao Afrika na kuua dini za Kiafrika
Kinyonge ufa,mbona dini za Wahindi na wachina hazijafa hali nao walitawaliwa
 
Kuna mtu nilimpa hili wazo tena msomi, kasema mimi ni mshamba kwa kuwa nataka nirudi kwenye mambo ya zamani. Eti wao wanaenda na wakati kwa kutumia huu utamadumi wa kizungu. Nilimuambia tu kwa upole kuwa "aliyedharau utamadumi wake ndio mshamba".
Utamaduni duni udumaza maendeleo
 
Mleta mada nakuunga mkono,ila unafahamu ili waweze kututawala walianza na kuziharibu imani zetu na kuleta zao,mbaya zaidi dini zetu hazikuandikwa ila zilikua za maneno na vitendo,kama hili lipo la kuanza kuandika imekaa sawa.
Hicho ndicho ninachoeleza humu,ukifanya utafiti wazungu na baadhi ya Waafrika wanaojitambua waliandika vitabu vya kila kabila i.e waha,wacjaga,wamasai,nk ndani ya Afrika hasa hapa kwetu Tz vitabu hivyo vipo ambavyo vilianza kupotea baada ya wazungu kuona vinawafumbua akili wazungu na pia wasomi kama Ngugi,Wole Soyinka,Rodney baada ya elimu zao kutoka kwa wazungu walianza kuielemisha Afrika kufuata mila na dini zao kwa uonesha jinsi wazungu walivyoua dini na desturi zetu i.e things fall apart,the river btn,nk lakini kwa ugumu wa fikra Waafrika waliwapiga vita hata kuwaua!!
 
Ndio Mungu ni mmoja lakini hata ndani ya waafrika wa kale kuna waliompatia na wengine wengi waliishia kuabudu viumbe tu kama majini nk. Mungu hujifunua kwa wanadamu polepole na inweza kuchukua mamilioni ya miaka kufunuliwa kuhusu Mungu. Wazungu walishaupata ufunuo ulio wa juu zaidi yetu kuhusu Mungu. Na ujue sio wazungu wote. Sasa kwanini kurudi nyuma?
 
Kipi kilichoanzishwa na Mwafrika kikafaulu, pan africanism imefeli, imani ya rastafari imefeli. Kabla ya kuanzisha jambo angalia asili ya watu hao ipoje
 
Yani kitu pekee kingetuletea dini ni Kinjekitile kushinda ile vita ya maji maji

Mussa (as) na Muhammad (saw) wenzake walishinda vita zao yeye alifeli
 
aliekudanganya ukimfata mzungu utakua kama yeye kakuingiza chaka.........mzungu alikupa maarifa na hata hizo imani ili akutawale milele tukishindwa kujiongeza wenyewe tutaendelea kua na mawazo ya kiutumwa kama hayo miaka na miaka
 
Yani kitu pekee kingetuletea dini ni Kinjekitile kushinda ile vita ya maji maji

Mussa (as) na Muhammad (saw) wenzake walishinda vita zao yeye alifeli
Shida huku machief walikua wanazungukana hawa wanalamba miguu ya wazungu hawa wanapigana nao
 
Wewe umewaza uganga tu ndiyo akili yako ilipoishia kwa kuwa ulishakaririshwa kuwa mila za desturi za waafrika ni "wichcrafts" pasipo kujiuliza witch inamaana gani na craft ina maana gani.

Ujinga ulionaonao wewe siyo wa kuisha leo
Dini tuliyonayo waafrika by nature ni ipi?

Ukijibu hilo swali nitakubaliana na kauli yako ya kuniita mjinga
 
Dini tuliyonayo waafrika by nature ni ipi?

Ukijibu hilo swali nitakubaliana na kauli yako ya kuniita mjinga
Muafrika hakua na dini(religion), muafrika alikua na "spirituality " kama wahindi na wale budha, hizo sio dini
 
Lazima tuwe na belief yetu kwanza ndipo tuweze kuwa na vyakwetu huwezi kuwa na gari la mzungu lugha ya mwarabu imani ya muhindi
c"mon, you do not have to invent the wheel! Kote kwanini huko. Wajapan walichukua technology toka magharibi na wakasonga mbele. Yote yanaweza kufanyika kwa wakati mmmoja ila hili la dini ni ujinga maana ni mambo ya kufikirika. Why waste time on mambo ya kufikirika kuwa yapo?
 
aliekudanganya ukimfata mzungu utakua kama yeye kakuingiza chaka.........mzungu alikupa maarifa na hata hizo imani ili akutawale milele tukishindwa kujiongeza wenyewe tutaendelea kua na mawazo ya kiutumwa kama hayo miaka na miaka
Wewe hapa sasa hivi una enjoy technology ya simu ya wazungu na mambo mengi mengine ya wazungu, sio kufuata mambo ya wazungu huko? Fuata yale yote mazuri ya wazungu utaendelea kama wao.
 
Muhindi na mchina je?? Ishu ni kufata kama zombi,,,hizo teknolojia na maarifa mengine pia mzungu alichukua kwa wengine sio vyote vya kwake,,,kakopi ila kabaki na asili yake kama walivyo wahindi na hata hao wachina na wenzao, we mtu mweusi unataka kukopi na ku paste kila kitu hadi asili yako unaisahau ,huo sasa ndo utumwa na ndo maana pamoja na kukopi kote huko bado afrika na mtu mweusi amebaki kua masikini na mtu wa mwisho karibia kwenye kila kitu duniani tofauti na wenzie waliokopi ya wazungu na wakafika mbali kama wahindi, wachina na hata waarabu.........watu wanakopi ila hawazifuti asili zao kama mtu mweusi anavyofanya kwa upumbavu wake
Wewe hapa sasa hivi una enjoy technology ya simu ya wazungu na mambo mengi mengine ya wazungu, sio kufuata mambo ya wazungu huko? Fuata yale yote mazuri ya wazungu unaendelea kama wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…