Hakuna hata milimita moja ya JMT iliyouzwa!.
P
Kaka P
Huko kuonekana kuna milimita za JMT zimeuzwa kunatokana haya;
1. Mkataba wa DPW na TZ hausemi ukomo. Hii maana yake, eneo lililotajwa kwenye mkataba lipo mikononi mwao milele.
Hapa nina swali hili;
- Wewe unajua mkataba huo mwisho wake lini?
2. Mkataba wa DPW na TZ, unasema kama kuna yeyote anataka kuendeleza eneo lililotajwa kwenye mkataba, inabidi TZ iwaambie DPW.
Hapa nina maswali haya;
- Hivi kwanini mpaka tuwaambie wao kama kweli eneo ni letu?
- Je! wakiambiwa na wakikataa tuna la kufanya? Na huku tumekikubali kipengele hicho?
- Tukitaka kuendeleza sisi wenyewe napo tunatakiwa kuwapa taarifa, na wanaweza wakasema HAPANA. Hivi hapa kwa kipengele hicho, huoni kwamba DPW ndo mmiliki wa eneo tajwa?
3. Mkataba wa DPW na TZ, hauvunjiki hata kutokee ugomvi wa kidiplomasia.
- Hapa ikitokea vita kati yetu na Dubai, eneo tajwa bado linakuwa lao.
Kifupi, kaka
Pascal Mayalla hayo maneno yenu ya kwamba bandari haijauzwa, mnapoyatamka, huwa hamuweki vipengele vinavyosapoti muyasemayo. Mnaishia kutaja maneno tu na kuleta habari za kuaminiana na usikivu wa serikali.